Shaka: Uthubutu wa Rais Samia unaifungua nchi kiuchumi na kimataifa

Shaka: Uthubutu wa Rais Samia unaifungua nchi kiuchumi na kimataifa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
SHAKA: UTHUBUTU WA RAIS SAMIA UNAIFUNGUA NCHI KIUCHUMI NA KIMATAIFA

Katibu wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akitoa salaam za Chama Cha Mapinduzi wakati wa uzinduzi rasmi wa kiwanda cha kuzalisha vifaa vya umeme kilichopo kata ya Kisarawe II wilaya ya Kigamboni mkoa wa Dar es Salaam amesema, Uongozi ni kitu cha ajabu sana, lakini kiongozi ama uhalisia wa uongozi hutangulizwa na uzalendo, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan uzalendo wako kwa Taifa hili sio wa kutiliwa mashaka si wakutilia mashaka ni wa asilimia mia moja, Mungu akubariki sana.

Lakini kiongozi ni ujasiri, kiongozi ni utayari, kiongozi ni karama na kiongozi ni uthubutu, Mheshimiwa Rais Samia umethubutu kuitekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa weledi, kwa ufanisi na kwa mafanikio makubwa, Hongera sana.

Shaka ameeleza Kumekuwa na maswali, watu wanajiuliza kwanini Mheshimiwa Rais amekuwa akisafiri sana Nje ya Nchi? Mheshimiwa Rais amepewa baraka na amepewa kibali na ilani ya uchaguzi ya CCM ibara ya 132, 18, 22, 32 na 46 vyote vinazungumzia namna ambavyo serikali ya CCM katika kipindi Cha miaka mitano kitakwenda kuhuisha na kusimamia diplomasia ya uchumi ndani ya Nchi yetu.


Shaka amesisitiza Kwenye hili Rais Samia umefanya vizuri sana na sasa unaipeleka nchi kule ambako wengi tunarajia kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika katika uchumi unaokua siku hadi siku na kuwafanya watanzania sasa kujivunia nafasi yao ya kijiografia, Mheshimiwa Rais hongera sana.

Aidha Shaka amewahakikishia watanzania utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ifikapo 2025 utakuwa zaidi ya asilimia mia moja Nichukue nafasi hii kwa niaba ya chama niwahakikishie watanzania kwa kasi hii anayokwenda nayo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan tunakwenda 2025 penye uhai ilani ya Chama Cha Mapinduzi itakuwa imetekelezwa kwa zaidi ya asilimia mia moja inshallah kwa umoja wetu na mshikamano wetu.

Katika kipindi kifupi cha Rais Samia uwekezaji mkubwa Tanzania imefanyika wa Dola bilioni 3.5 ambapo kwa haraka haraka ajira ya zaidi ya 35,543 zimekwenda kuzalishwa. Mheshimiwa Rais endelea kuupiga mwingi, kiwanja umekimiliki. Asante sana.
 
Halafu kuna watu wanapinga ooh Tanzania haiwezi kufananishwa na Marekani kwa chochote. Kuna machache tunaweza tusifananishwe na Marekani kama kuua watu Japani kwa bomu la nyuklia, kushiriki mauji ya ya Saddam kwa sababu za uongo eti ana silaha za maangamizi!

Lakini haya utawala wa demokrasia tuna fanana nao.
 
Halafu kuna watu wanapinga ooh Tanzania haiwezi kufananishwa na Marekani kwa chochote. Kuna machache tunaweza tusifananishwe na Marekani kama kuua watu Japani kwa bomu la nyuklia, kushiriki mauji ya ya Saddam kwa sababu za uongo eti ana silaha za maangamizi!

Lakini haya utawala wa demokrasia tuna fanana nao.
Umenena ya kweli mkuu
 
Back
Top Bottom