Shaka Zulu alichinja zaidi ya watu 7000 ndani ya mwaka mmoja tu

Robot la Matope, Shaka Zulu nijuavyo mama yake alitengwa hapo kijijini na kwenda ufalme wa jirani siyo kwa sababu Mfalme Senzangakhona alimuoa Nandi ( mama yake Shaka) kuwa kabila tofauti na Wazulu, bali kwa sababu Mfame alimpa ujauzito Nandi kwenye sherehe za mavuno zilizokuwa zinafanyika usiku.

Na kwa mila za Wazulu za wakati huo, mwanamke akibeba mimba kabla ya kuolewa anauawa, kabla ya kuuawa kwanza amtaje aliyempa hiyo mimba naye auawe! Sasa aliyevunja sheria hiyo ni mfalme Senzangankhona mwenywe!

Ili kuepusha aibu hiyo, mfalme aliongea na mfalme mwenzake wa jirani Nandi akatoroka kijijini akamzalia huko Shaka. Lingine, Shaka mwisho wake haukuwa mzuri kutokana na mama yake kumfundisha ushirikina toka akiwa mdogo, ambapo alichanjwa madawa ya ushujaa vitani, madawa ambayo muda wote yalihitaji kuua, yalihitaji damu. Kutokana na hilo, Shaka aliongoza mapambano mengi ya kivita, na furaha yake ilitimia pale anapoua. Falme jirani zote zilikimbia zisikiapo jeshi la Shaka Zulu, Shaka akakosa maadui wa kupigana nao.

Kwa kuwa dawa zake zilikuwa na masharti ya kuua kila wakati, Shaka akaanza kuumwa, kuumwa kwa kukosa wa kuua! Ikafikia sasa Shaka akaanza kuua watu wake, na anapoua kwa mkono wake watu wanne au watano, afya ya mwili wake inarejea bukheri wa afya! Moja ya mbinu aliyoitumia kuua kwa urahisi anapohisi kuumwa kwa kuteswa na madawa ni kuitisha sherehe ya vyakula na pombe ambapo wanakijiji hulewa na kuimba nyimbo, ndipo Shaka huinuka na kuagiza aletewe watu wanaoimba vibaya na hutumia mwanya huo kuwaua, na anapoua afya yake inarejea!

Mwisho Shaka aliuawa na ndugu zake wawili wa mama wengine lakini baba mmoja waliomtembelea na akawaamini kuongea nao kwenye ikulu yake huku walinzi wakiamini mfalme yuko na ndugu zake!
 
JamiiForums ni jamvi ambapo tunajifunza mengi kutokana na hadithi au historia.

Uzi huu una mafunzo mengi ambayo hatupaswi kuyapuuza maana historia huwa na kawaida ya kujirudia.

Ndiyo maana jamii zilizotunza na kuenzi mafundisho kupitia hadithi au historia huweza kujiepusha na mambo mengi mabaya kupitia kumbukizi kama hii ya Shaka Zulu.
 
Ombeni nice kabla ya mamangu mtatabika na msije sema sikuwaambia. Nitawatumia in peace mpaka mchakae
 
Huyu jamaa alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kurusha mkuki wake na kwenda masafa marefu
Na ndo mana ingawa alikuwa ni mtoto wa njee wa kimada wa chief ambaye ni baba ake alipewa uongoz huo sabb alikuwa na kipaji na nguvu nyingi mnoo
 
Uongo
 
Umetoa wapi hizi Data Mkuu!!!! Angalia sana mkuu haya mambo mengine ndio yanasababisha Waafrika wajichukie na kutojiamini mpaka leo!!!! Wenye chuki na Waafrika ndio huwa wanapika Data za namna hii wakijua wapo wenye akili ya kushikiwa wanaamini cho chote hata kinachotoka kwa adui yetu!!! Mbona hawamtukuzi Chaka (Shaka) kwa mafanikio yake ya kuweza kuunganisha makabila ya Waafrika kusini ambayo mpaka leo mabaki yake tunayoona ( Kabila la Wazulu ndio kabila kubwa Zaidi kuliko yote Afrika Kusini). Kama angefanikiwa kwenye ndoto yake Chaka ndio angefanikiwa katika juhudi zetu tukuka za kuunganisha Afrika kuwa mmoja. Bila msaada wa mitandao au teknolojia Chaka aliweza kujenga taifa kubwa sana ambalo cheche zake zilifika mpak huku Tanzania!!! Hebu angalia unajua Eswatini ni nchi ya ambayo pia ilikuwa sehemu ya Ufalme wa Wazulu. Zimbambwe kuna Wamatebele ambao pia ni tawi la Wazulu achilia mbali kwetu huku Wangoni!!!!! Niambie kiongozi mwingine Afrika aliefanikiwa kiasi hiki!!!!

Tuamke Waafrika!!!!! Usingizi gani huu tumelala karne na karne…..
 
Siri iliyopo nikuwa shaka zulu aliambiwa na mganga wake kuwa atakapokufa mamayake basi na yeye hana muda mrefu atakufa. Ndo hasira zikaanzia hapo
 
Ni mada iliyokosa ukweli hasa huyu mtawala Shaka alivyoishi,jitahidi uangalie movie yake shaka zulu angalia series zote,jisomee vitabu na kama unauwezo tembelea pale Urundi kupata ukweli wa upande wa pili wa story hii.
 
Mmmmmmmmmh huyo tumewahi kumuona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…