Shaka Zulu alichinja zaidi ya watu 7000 ndani ya mwaka mmoja tu

Shaka Zulu alichinja zaidi ya watu 7000 ndani ya mwaka mmoja tu

Akili za Kiafrika zimekaa hovyohovyo tu, kuna mfalme mwingine wa Afrika kusini alikulia katika mazingira ya umasikini basi akaamuru raia wake wote nao pia wawe masikini, na ole wako ujifanye tajiri atahakikisha unaishi kama mashetani.

Maendeleo hayana chama
... ili kila mtu asikie maumivu ya umaskini aliokulia kama naye alivyokuwa ana-feel!
 
Usitudanganye wewe, unadhani sote ni dot com hatusomi vitabu eeh!Amazulu=Zulu ni neno lililobuniwa na Shaka baada ya kupigana na kushinda Vita nyingi. Sasa mama yake angeitwaje mzulu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hata hiyo story ya kuwa alikuwa anauwa wanawake waliojifungua na wajawazito imekaa kifitina fitina tu. Yeye alikuwa muuaji hasa kwa wale ambao alikuwa anapigana nao vitani. Ziko documentaries za Shaka Zulu.
 
Mkuu kastory kako kana ukweli mtupu nimeingia Wikipedia ndipo napo wameeleza hivyo na ndicho kifo cha Mama yake Mzazi (hapo ndipo nduguze Shaka Dingane and Mhlangana, Shaka's half-brothers, wakamuua)
Shaka had made enough enemies among his own people to hasten his demise. It came relatively quickly after the death of his mother Nandi in October 1827, and the devastation caused by Shaka's subsequent erratic behavior. According to Donald Morris, Shaka ordered that no crops should be planted during the following year of mourning, no milk (the basis of the Zulu diet at the time) was to be used, and any woman who became pregnant was to be killed along with her husband. At least 7,000 people who were deemed to be insufficiently grief-stricken were executed, although the killing was not restricted to humans: cows were slaughtered so that their calves would know what losing a mother felt like.[11]
Ila huyu jamaa kichwani hakuwa sawa. Alikuwa ni mental case.
 
Jina lake kamili anaitwa 'Shaka kaSenzangakhona' alikua maarufu kwa jina la 'Shaka Zulu'. Alizaliwa mwaka 1787 huko Kwazulu-Natal Afrika Kusini na kufariki mwaka 1828 akiwa na miaka 41. Alikuwa mfalme wa himaya ya Wazulu huko Afrika Kusini kuanzia mwaka 1816 –1828 akichukua Ufalme kutoka kwa baba yake 'Senzangakhona kaJama' aliyefariki.

Shaka Zulu alikua anampenda sana sana mamayake mzazi 'Nandi kaBhebhe' kiasi kwamba mamayake huyo alipofariki October 10, 1827, Shaka akaanza kufanya mauaji!

Inaelezwa kuwa kila asubuhi alipokua anaamka alikua anawachinja wanawake waliojifungua siku za karibuni pamoja na waume zao, anawachinja wanawake waliokua na ujauzito, anawachinja watu waliokua hawaoneshi huzuni/hawasikitiki juu ya kifo cha mama yake, hata ng'ombe aliyeonekana mjamzito au alitejifungua hivi karibuni allikua anachinjwa!.

Lengo kubwa la kufanya hivyo lilikua ni kutaka pia watu wapate maumivu/uchungu aliokuwa anaupata yeye kwa kumpoteza mama yake mzazi.

Zaidi ya watu 7,000 waliuwawa kwa kuchinjwa na Shaka Zulu ndani ya mwaka mmoja tu, lakini pia licha ya kuuwa kiasi hicho, Shaka pia alipiga marufuku mtu yeyote wa Himaya ya Wazulu kupanda zao lolote shambani kwa mwaka huo.

Mama yake alizaliwa 1760 na kufariki October 10, 1827 kwa matatizo ya utumbo na katika maisha yake yote alimzaa mtoto mmoja tu ambaye ndiye Shaka Zulu.

Shaka Zulu alikua na uchungu sana kwa mama yake kwasababu mama yake alikuwa wa kabila lingine la 'Langei' na baba yake alikua kutoka katika kabila la Wazulu.

Baada ya ujauzito mamayake alitotoka nyumbani na kwenda kuishi milimani/porini pekeake kwani iliamriwa mtoto akizaliwa auwawe kwasababu iliaminika kuwa angekua mkosi katika kabila lao kutokana na baba yake kuwa kabila tofauti.

Baadae jambo hilo liliisha kwa baba yake Shaka Zulu kulipa faini ya mifugo 50.

Shaka zulu aliwahi pewa amri na wakoloni kwamba aachane na mila/tamaduni na aipokee dini vinginevyo atachomwa moto akiwa hai!, shaka akwajibi tuu kwamba "huku kwetu tunakula moto".

Shaka Zulu naye aliuawa mwaka mmoja tu baada ya mama yake kufa, kwasabababu tangu mamayake afariki alianza kufanya mauwaji hayo kila siku hadi siku ya mwisho naye anauwawa bado alikua anachinja watu tu.

Tufollow Instagram @fm_facts



Sent using Jamii Forums mobile app
achene kuchafua heroes wenu. wazungu hawajawahi kuchafua heroes wao, instead huwa wanadiliki hata kudanganya historia ili waonekane bora, ila waafrika hata kile kidogo kizuri tulichonacho bado tunaponda, tuna nn sisi.
 
Makaburu walikua sahihi kuinyoosha South Africa, Watu weusi ni watu wa ajabu sana
 
Back
Top Bottom