Shakira alianza kushtuka Pique alikuwa anamcheat sababu ya Jam kwenye fridge

Machame Juu

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2013
Posts
1,514
Reaction score
3,363
1694622299289.png

Mwanamziki maarufu kutoka Colombia Shakira ambaye walitengana na mpenzi wake aliyekuwa beki wa timu ya mpira Barcelona pique machale yalimcheza pique alikuwa anamcheat baada ya kukuta Strawberry Jam kwenye fridge imeliwa.

Wambea wanadai Gerald Pique hapendi na hajawahi kula Iyo strawberry Jam ni Shakira pekee yake ndo alikuwa akiitumia.

Shakira alishanga Aliposafiri na watoto wake nakumuacha Gerald Pique peke yake nyumbani na aliporudi kufungua fridge akakuta kopo la Strawberry Jam limefunguliwa na kutumika.

Na ndio hapo machale yakamcheza na kushtuka.

Shakira kuachana na Gerald Pique imemuuma sana. Wanoko wanadai anamuombea mabaya sana Pique kwenye uhusiano wake mpya na kabinti kadogo.

Pique naye anamuoneshea madharau hata kwenda Miami marekani kutembelea watoto wake hataki.

Shakira ameshaweka wazi hataki Pique alipe hata senti ya child support na yuko tayari hata kumlipia ticket ya ndege aende Miami kuwatembelea madogo.

Shakira ameweka wazi bado inamuuma sana kutengana na Pique. Anapitia wakati mgumu na kiza nene sana katika maisha yake ukizingatia haya yote yametokea baba yake akiwa ICU. Anasema anapiga picha jinsi wanawake wengine duniani wanaopitia mateso kama yake anabaki kulia

Licha ya utajiri wa dollas za kimarekani million 400 bado tu hana furaha.

Shakira ana asili ya Lebanon. Mababu zake ni kati ya wale waarabu walioamia mwishoni mwa karne ya 18 na mwanzoni karne ya 19 kwa wingikama wafanya biashara (merchants) Marekani, central na south America ambao vizazi zao ni maarufu kama Steve Jobs Syria, Carlos Slim billionaire mexico Syria, Bella Hadid Palestina na Rais wa El Salvador Nayib Bukele Palestina.

Source Gazeti la udaku The Sun Uingereza
 
Mapenzi ni utapeli.
Oh! Nakupenda wewe tu, Mungu ni mwema ametukutanisha. Nakupenda sana. Simu kama zote, i love you nyingi.
Mwisho wa siku mnachukiana, ukimuona mwenzako unabadilisha njia, wengine wanalala mzungu wa 4.
Mwisho wa siku, tukagawane mali, mnapelekana polisi, mahakamani hata kutishiana kuuana.
Mapenzi ni utapeli
 
Mwanamziki maarufu kutoka Colombia Shakira ambaye walitengana na mpenzi wake aliyekuwa beki wa timu ya mpira Barcelona pique machale yalimcheza pique alikuwa anamcheat baada ya kukuta Strawberry Jam kwenye fridge imeliwa.

Wambea wanadai Gerald Pique hapendi na hajawahi kula Iyo strawberry Jam ni Shakira pekee yake ndo alikuwa akiitumia.

Shakira alishanga Aliposafiri na watoto wake nakumuacha Gerald Pique peke yake nyumbani na aliporudi kufungua fridge akakuta kopo la Strawberry Jam limefunguliwa na kutumika.

Na ndio hapo machale yakamcheza na kushtuka.

Shakira kuachana na Gerald Pique imemuuma sana. Wanoko wanadai anamuombea mabaya sana Pique kwenye uhusiano wake mpya na kabinti kadogo.

Pique naye anamuoneshea madharau hata kwenda Miami marekani kutembelea watoto wake hataki.

Shakira ameshaweka wazi hataki Pique alipe hata senti ya child support na yuko tayari hata kumlipia ticket ya ndege aende Miami kuwatembelea madogo.

Shakira ameweka wazi bado inamuuma sana kutengana na Pique. Anapitia wakati mgumu na kiza nene sana katika maisha yake ukizingatia haya yote yametokea baba yake akiwa ICU. Anasema anapiga picha jinsi wanawake wengine duniani wanaopitia mateso kama yake anabaki kulia

Licha ya utajiri wa dollas za kimarekani million 400 bado tu hana furaha.

Shakira ana asili ya Lebanon. Mababu zake ni kati ya wale waarabu walioamia mwishoni mwa karne ya 18 na mwanzoni karne ya 19 kwa wingikama wafanya biashara (merchants) Marekani, central na south America ambao vizazi zao ni maarufu kama Steve Jobs Syria, Carlos Slim billionaire mexico Syria, Bella Hadid Palestina na Rais wa El Salvador Nayib Bukele Palestina.

Source Gazeti la umbea The Sun Uingereza
Shakira na mauno yake, uzuri wake, na pesa zake anapigwa chini. Wewe Kiberenge ni nani hadi uanze kupekua simu yangu?
 
Pique kidume Shakira kamwimba, mwamba kakaa kimya,hajajibu wala kufanya intvw yoyote. Japo ukimya wa mwanaume huwaga unaonyesha yy anamakosa,ila hatuwezi fahamu yaliyo kifuani mwa Pique,wanawake wanapenda sana kuonewa huruma,mbele za watu.
Ila Pique strong kamzidi hata kukomaa kiakili japo Shakira kamzidi umri kwa miaka kumi pique wa 87 Shakira 1977.
 
Wanawake ni wapelelezi sana na kila jambo ulifanya kwa hisia, nilipigiwa simu mara 4 usiku sikupokea mtoto wa watu kawasha gari yake saa 11 kasoro alfajiri toka Mbweni mpaka Kibada kapaki gari nje ili aje kufumania tu ile nafungua geti naona mtu kanuna ananiangalia usoni wa macho makali. mapenzi haya!!!
 
Back
Top Bottom