Machame Juu
JF-Expert Member
- Jul 25, 2013
- 1,514
- 3,363
Mwanamziki maarufu kutoka Colombia Shakira ambaye walitengana na mpenzi wake aliyekuwa beki wa timu ya mpira Barcelona pique machale yalimcheza pique alikuwa anamcheat baada ya kukuta Strawberry Jam kwenye fridge imeliwa.
Wambea wanadai Gerald Pique hapendi na hajawahi kula Iyo strawberry Jam ni Shakira pekee yake ndo alikuwa akiitumia.
Shakira alishanga Aliposafiri na watoto wake nakumuacha Gerald Pique peke yake nyumbani na aliporudi kufungua fridge akakuta kopo la Strawberry Jam limefunguliwa na kutumika.
Na ndio hapo machale yakamcheza na kushtuka.
Shakira kuachana na Gerald Pique imemuuma sana. Wanoko wanadai anamuombea mabaya sana Pique kwenye uhusiano wake mpya na kabinti kadogo.
Pique naye anamuoneshea madharau hata kwenda Miami marekani kutembelea watoto wake hataki.
Shakira ameshaweka wazi hataki Pique alipe hata senti ya child support na yuko tayari hata kumlipia ticket ya ndege aende Miami kuwatembelea madogo.
Shakira ameweka wazi bado inamuuma sana kutengana na Pique. Anapitia wakati mgumu na kiza nene sana katika maisha yake ukizingatia haya yote yametokea baba yake akiwa ICU. Anasema anapiga picha jinsi wanawake wengine duniani wanaopitia mateso kama yake anabaki kulia
Licha ya utajiri wa dollas za kimarekani million 400 bado tu hana furaha.
Shakira ana asili ya Lebanon. Mababu zake ni kati ya wale waarabu walioamia mwishoni mwa karne ya 18 na mwanzoni karne ya 19 kwa wingikama wafanya biashara (merchants) Marekani, central na south America ambao vizazi zao ni maarufu kama Steve Jobs Syria, Carlos Slim billionaire mexico Syria, Bella Hadid Palestina na Rais wa El Salvador Nayib Bukele Palestina.
Source Gazeti la udaku The Sun Uingereza