- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Mwaka 2010 FIFA walimpatia nafasi Shakira ya kuandaa na kuimba wimbo maalumu kwa ajili ya michuano ya kombe la Dunia ya mwaka 2010 iliyofanyika Afrika ya Kusini. Kwa taarifa za juu ni kwamba Shakira Isabel Mebarak alitupiga na kitu kizito kwani alifanya sampling na kuiba melody ya wimbo wa "Zangaléwa" uliokuwa ni utunzi wa Kundi kutoka Kameruni la Golden Sounds, na kutuletea Waka Waka.
Sijajua kama ni kweli ila nahitaji kupata ufafauzi kidogo kutoka kwa Jamii Check.
---
Video yenye ufafanuzi wa Asili ya ala za muziki zilizotumika kwenye Waka Waka (This Time for Africa)
- Tunachokijua
- Shakira ni mwanamuziki maarufu kutoka Colombia anafahamika pia kwa kuwa na sauti ya kipekee na uwezo wake wa kucheza wa kipekee wa kucheza dansi." Jina lake kamili ni Shakira Isabel Mebarak Ripoll, na alizaliwa mnamo 2 Februari 1977. Shakira alianza kupata umaarufu duniani mnamo miaka ya 1990 kupitia albamu zake za Kihispania kama "Pies Descalzos" na "Dónde Están los Ladrones?"
Aidha, Umaarufu wake uliongezeka zaidi alipoanza kuimba kwa lugha ya Kiingereza, na albamu yake ya "Laundry Service" ya mwaka 2001 ilifanikiwa sana. Anajulikana na wengi kwa nyimbo kama “Hips Don’t Lie,” “Waka Waka (This Time for Africa),” na “Whenever, Wherever.”
Ipi historia ya wimbo wa Wakawaka?
Waka Waka (This Time for Africa)" ni wimbo ulioimbwa na Shakira kwa kushirikiana na kundi la muziki la Afrika Kusini, Freshlyground. Wimbo huu ulitolewa mnamo mwaka 2010 na ulikuwa wimbo rasmi wa Kombe la Dunia la FIFA 2010 lililofanyika nchini Afrika Kusini.
Baada ya kutolewa kwa "Waka Waka (This Time for Africa)," kulikuwa na madai kwamba Shakira aliiba wimbo huo kwa kutumia wimbo wa "Zangaléwa" bila kutoa heshima ya kutosha kwa chanzo
Ipi asili ya madai hayo?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa Madai kwamba Shakira aliiba wimbo wa "Waka Waka" yanatokana na ukweli kwamba sehemu ya kionjo chake (Kiitikio) kimeundwa kupitia wimbo wa asili wa Cameroon uitwao "Zangaléwa," ulioimbwa na kundi la Golden Sounds, uliotolewa mwaka 1986 na ukawa maarufu sana barani Afrika. Zangalewa unaelezwa kuwa ulikuwa wimbo wa kijeshi wenye lengo la kuhamasisha na kufurahisha wanajeshi, lakini pia ulipendwa na raia wengi wasio Wanajeshi. (Tazama video hapo juu)
Utata huu ulichochewa na mahojiano aliyoyafanya Shakira (haya hapa) kuelezea namna alivyoutunga wimbo huo kwa muda mfupi bila kutaja mchango na uhusika wa Kundi la Golden Sound kwenye wimbo. Akisimulia namna alivyotunga wimbo huo Shakira anasema
"Nilitoka kwenye ghala hadi nyumbani, na katika matembezi hayo, ghafla! Wazo likanijia," Shakira alisema huku akicheka, akielezea kwamba alirekodi mara moja kwa kutumia gitaa la akustiki. "Ndipo nilipotambua kwamba wimbo huo ulikuwa na nguvu wakati wimbo unaposikika vizuri tu na gitaa la kawaida na sauti."
Ukweli upoje
JamiiCheck imefuatilia vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa baada ya mjadala huo, ilifahamika kwamba Shakira hakuiba wimbo huo bali alipata ruhusa ya kutumia kionjo hicho kutoka kwa kundi la Golden Sounds na waandishi wa asili wa wimbo wa "Zangaléwa."
Aidha, Jarida la Bakwa Magazine lilinukuu mahojiano yaliyofanywa na Tribune kwa kiongozi wa kundi la Golden Sounds aitwaye Ze Bella ambaye alifafanua kuwa pamoja na kundi lako kutoshirikiswa mwanzoni wakati wa utoaji wa wimbo huo lakini baadaye walipokea fidia ya kifedha na waliridhika na jinsi suala hilo lilivyoshughulikiwa.