Mwanamuziki maarufu duniani kutoka Colombia, Shakira (49), ametangaza kuwa hana matumaini ya kuingia tena kwenye ndoa au kupata mwenza sahihi wa kuanza naye maisha mapya, akitaja umri wake kuwa miongoni mwa sababu kuu zinazofanya jambo hilo kuwa gumu kwa sasa.
Shakira, ambaye ni mama wa watoto wawili, amefunguka kuhusu hisia hizo wakati akizungumzia maisha yake ya kimapenzi na changamoto za kupata mwenzi anayemfaa katika hatua aliyonayo sasa kiumri.
Mama huyo wa watoto wawili alipata wanae katika uhusiano wake wa baadaye, baada ya kumalizika kwa uhusiano wake mrefu wa miaka 10 bila mtoto na Antonio de la Rúa mtoto wa aliyekuwa Rais wa Argentina, Fernando de la Rúa uhusiano uliodumu kuanzia mwaka 2000 hadi walipotengana rasmi Januari 2011.
View attachment 3677384
View attachment 3677385
View attachment 3677386