Shamba la bibi

Mkuu unaandika kama vile mgeni wa Siasa. Kwanza Kikatiba ni kosa.kubwa sana kumtambulisha rais wa nchi kama MAMA. Na kosa hili lina impact kubwa kwa sababu Mama hakosolewi, Mama anaheshimika hata kama akikosea ni Mama yako!

Pili, wewe unampimaje Kiongozi? Unaposema Mama anafanya vizuri ni uzuri upi? Ikiwa kutwa Waziri Mkuu anakamata watu wamefisadi fedha za Umma!

Acha report ya CAG ambayo mimi naona bado ina mapungufu mengi tu, pitia magazeti na ziara za Waziri Mkuu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa katika miradi yote! Ni wizi kila kona! Mradi gani ulokamilika leo na kwa kiwango cha juu?

Rais anajitahidi sana lakini baadhi wasaidizi wake wanamuangusha! Kwa nini wanamuangusha? Kama kuna watu wanamuangusha, yeye anafanikiwa wapi?

Na unapozungumzia system ni system ipi hiyo ikiwa mkuu wake hajali! Kama unavyozungumzia vyama vya Siasa ndivyo System ilivyo -The back stop at the President. Sema ukweli rais Samia anawajali na anawalisha wanawe vema wanenepe. Kama Mama atawalinda wanawe hata kama wamekosea. Mama hamtupi mwanae, nanyi bado mnataka nyonyo za chupa! Hili ni kosa kubwa sana litatugharimu. It's about time someone raise a voice, ujinga wa kula mpaka mbegu sii Ujanja hata kidogo..
 
Itakuwa walimnukuu vibaya tu kwamba kila buzi ale kwa urefu wa kamba yake๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
Ukitaka kurahisisha, then utawalaumu tu wale walioitwa stupid. Lakini ukitaka kuwa mkweli na muona mbali, then utaangalia ruzuku kwa vyama pinzani waliyofikia makubaliano na kulipwa kimya kimya, kuwa nayo ni aina ya rushwa ya kuwalainisha.

 

Ibeni tu
 
Hawawezi kutumia neno la "Serikali ya Raisi Samia" imeshindwa kufanya hivi na vile kwa sababu huo ndo mkakati wao kuhakikisha kila mtu aiba atakavyo na hakutakuwa na wa kusema vinginevyo.
 
Mama as Mama, she is doing great, ila bado kuna baadhi ya wasaidizi wake wanamuangusha, hao watupishe!.

Kwahiyo unamaanisha kuwa Mama hawajibiki na mapungufu yoyote ya kwenye awamu yake kwa sababu hayuko directly involved?


Ushamba una ubaya gani kama uko effective kutatua matatizo na kujenga uwajibikaji? Mbona nchi zilizo mbele kidemokrasia wanatajana magazetini, redioni na kwenye TV?

Kufoka ni jambo jema sana kwa kiongozi anayejenga tabia kwa jamii. Lee Kuan Yew alikuwa ni mfokaji na mkali na hatimaye Singapore wakajenga discipline kama yake.

System unayoitaka wewe haiibuki tu, inahitaji kujengwa kwa kuwafundisha watu, na sio kwa kuwaambia watumishi WALE KULINGANA NA UREFU WA KAMBA.



Kama hatujaweza kuwa na multi party system, tunawezaje kuwa na system ya kuwajibishana isiyomhusisha raisi mkali? Maendeleo yote nchini kwa sasai yanahitaji raisi mkali, mtendaji na sio raisi mkaa pembeni na kuja kwenye TV kulalamika juu ya aliowateua bila kuchukua hatua.

Kwanza kwenye ripoti ya CAG, kila ubadhirifu unaotajwa wa fedha za umma, sio lazima fedha hizo ziwe ni zimeibiwa!. Fedha nyingine ni matumizi mabaya tuu lakini hakuna fedha yoyote iliyoibiwa!.
P

Hii sio kweli Pascal, DSM peke yake zimeliwa 896m zilizokuwa ziende kwa vijana wa Bodaboda.

Mama inabidi abadilike na kuwa mkali na hands on kama alivyokuwa JPM. Bila hivyo 2025 anaweza akakosa kura nyingi sana na kuhatarisha uraisi wake.

Template ya JPM imeonyesha wazi mafanikio. Inabidi iendelezwe minus kukufokea wewe ๐Ÿ˜€ na kuwabana upinzania by 100%.
 
Hawawezi kutumia neno la "Serikali ya Raisi Samia" imeshindwa kufanya hivi na vile kwa sababu huo ndo mkakati wao kuhakikisha kila mtu aiba atakavyo na hakutakuwa na wa kusema vinginevyo.
Utawasikia wakisifiana kwa ile misemo yetu ya jando na unyago; Kwamba "ukila na kipofu usimshike mkono".....Huu utamaduni wa kudhurumu hata vipofu umejengeka na unatekelezwa huko Serikalini tena bila hata aibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ