- Thread starter
- #21
Mkuu unaandika kama vile mgeni wa Siasa. Kwanza Kikatiba ni kosa.kubwa sana kumtambulisha rais wa nchi kama MAMA. Na kosa hili lina impact kubwa kwa sababu Mama hakosolewi, Mama anaheshimika hata kama akikosea ni Mama yako!Mama as Mama, she is doing great, ila bado kuna baadhi ya wasaidizi wake wanamuangusha, hao watupishe!.
Mambo ya kutajana tajana kwa vyeo na majina ni mambo ya kishamba!. Wastaarabu hawataji taji majina, ndio maana niliwahi kushauri we don't need strong leaders wa kufoka foka, tunahitaji an effective system, you mess, no one tells you ume mess, system ina ku detect na kuku eject, rais hana haja ya kuhangaika kutumbua tumbua, you mess today, kesho rais unajikuta resignation letter yako mezani kwake!
Kwani Tanzania tuna vyama vingi in a real sense of multi party?. Tanzania tuna jina tuu la nchi ya multi party but the reality ni tuna chama kimoja tuu, the one and only, kiki play the game of politics na mfano vyama, au vyama makapuku!, hivyo hakina mshindani wala mpinzani!.
Kwanza kwenye ripoti ya CAG, kila ubadhirifu unaotajwa wa fedha za umma, sio lazima fedha hizo ziwe ni zimeibiwa!. Fedha nyingine ni matumizi mabaya tuu lakini hakuna fedha yoyote iliyoibiwa!.
P
Pili, wewe unampimaje Kiongozi? Unaposema Mama anafanya vizuri ni uzuri upi? Ikiwa kutwa Waziri Mkuu anakamata watu wamefisadi fedha za Umma!
Acha report ya CAG ambayo mimi naona bado ina mapungufu mengi tu, pitia magazeti na ziara za Waziri Mkuu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa katika miradi yote! Ni wizi kila kona! Mradi gani ulokamilika leo na kwa kiwango cha juu?
Rais anajitahidi sana lakini baadhi wasaidizi wake wanamuangusha! Kwa nini wanamuangusha? Kama kuna watu wanamuangusha, yeye anafanikiwa wapi?
Na unapozungumzia system ni system ipi hiyo ikiwa mkuu wake hajali! Kama unavyozungumzia vyama vya Siasa ndivyo System ilivyo -The back stop at the President. Sema ukweli rais Samia anawajali na anawalisha wanawe vema wanenepe. Kama Mama atawalinda wanawe hata kama wamekosea. Mama hamtupi mwanae, nanyi bado mnataka nyonyo za chupa! Hili ni kosa kubwa sana litatugharimu. It's about time someone raise a voice, ujinga wa kula mpaka mbegu sii Ujanja hata kidogo..