Shamba langu. Bustani ya ndoto zangu

Shamba langu. Bustani ya ndoto zangu

Je wajua ya kwamba ndoto zaweza kuwa kweli? Wazungu wanasema dreams can come true...

Fanya yote maishani.. Pambana sana lakini usiache kumwomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema zote akujaalie mwisho mwema, uzee uliojaa fanaka na baraka.. Tele.. Wanazengo wanasema fainali uzeeni.. Basi Mwombe sana Manani akutunuku fainali ya ushindi.. Sio ya kutoa suluhu wala kufungwa..!

Pamoja na yote utakayojaaliwa pata walau hekari moja ukikosa kabisa basi walau nusu yake .. Kishapo
Jenga kajumba kako kazuri sana.. Huhitaji ghorofa wala nyumba kubwa utafuga majini na mashetani bila

kutaka na bila kujua
Fuga mifugo yako michache
1. Ng'ombe wa maziwa mmoja wakizidi wawili
2. Kuku wawili watatu wa mayai wa kienyeji
3. Ukiweza na ukipenda fuga na bata au sungura
4. Bwawa dogo la samaki
5. Fuga njiwa ukiweza na kasuku na ndege wengine wa leisure
Hii mifugo yote
Hawa wote watakusaidia sana kwenye ishu ya mbole
Kuzunguka nyumba una bustani zako za maua, garden na miti ya vivuli
Huko shambani sasa unatenga eneo la shamba dogo mazao mixer miti ya matunda.. Eneo lililobaki bustani za mbogamboga..
Utahitaji kisima pia
Pengine utahitaji vijana wawili watatu wa kukusaidia
Utahitaji chumba/ghala lenye vitendea kazi vyote...
Eat well.. Eat fresh.. Na kamnywesho kidogo😀😀😀View attachment 3261641View attachment 3261642View attachment 3261643View attachment 3261644
Hapa kwangu Nina kuku wachache
Sunugura3
Njiwa8 .
Bustani ya mbogamboga

Kijijni ndo Nina kuku wengi na mashamba ya bustani

Hakika uliyonena ni kweli na hakika
 

Attachments

  • IMG_20230612_182337_703.jpg
    IMG_20230612_182337_703.jpg
    291.3 KB · Views: 0
Back
Top Bottom