VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kuna habari kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameshambuliwa na 'watu wasiojulikana' jijini Dodoma alipokuwa akirejea nyumbani kwake usiku wa kuamkia jana. CHADEMA, kupitia kwa Katibu Mkuu wake John Mnyika, wakatoa taarifa ya awali kwa umma juu ya shambulio hilo la Mwenyekiti na kingozi wao huyo wa juu kabisa kwenye chama chao.
Nilipata faraja nilipokuona Kamanda Muroto ukijitokeza mbele ya wanahabari na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kutoa kauli ya Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma kuhusu shambulio la Mbowe. Kwa umakini na ustadi mkubwa Kamanda Muroto ukauambia umma wa watanzania mambo makubwa matatu. Kwanza, uchunguzi dhidi ya tukio hilo umeanza na unafanywa na jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama.
Pili, tukio la Mbowe lisitumike kisiasa na kama mtaji wa kisiasa na yeyote. Na tatu, ni kupiga marufuku mtu yeyote kulizungumzia jambo hilo kwa minajiri ya kuingilia uchunguzi wa kipolisi. Nilikuelewa sana. Nilitamani na ninatamani kuona ukisimamia kauli zako juu ya shambulio dhidi ya Mbowe. Nikupe taarifa au nikukumbushe kama tayari unajua kuwa jana Bungeni Mbowe alikuwa gumzo kwenye mjadala wa kupitisha Azimio la kumpongeza Rais Magufuli.
Kiti cha Spika wa Bunge kikikaliwa na Job Ngugai mwenyewe kiliruhusu mjadala wa tukio la shambulizi la Mbowe. Wachangiaji walipangwa kimkakati ili kutimiza azma yao. Kuanzia kwa Spika Ndugai, Silinde, Lijualikali, Musukuma na hata Lusinde, wote walikejeli tukio hilo na kulihusianisha na ulevi. Walihitimisha kwa kusema kuwa Mbowe alikuwa amelewa na aliteleza kwenye ngazi zake na kuvunja/kutegua mguu wake. Tena akiwa na 'kimada'.
Wabunge hao niliowataja walikebehi na kumkejeli vya kutosha Mbowe na kulikejeli shambulo lake. Tayari wameshaingilia na kuvuruga uchunguzi wa Polisi kwenye tukio hilo. Wanaachwaje bila ya kukamatwa katika kutekeleza kauli ya kamanda Muroto? Wanaopaswa kukamatwa ni Spika Ndugai na Wabunge Silinde, Lusinde, Musukuma na Lijualikali. Wameshaingilia uchunguzi wa Polisi. Wameshakiuka marufuku ya Muroto.
Tunajua kuwa Mbowe anaponzwa na Lissu. Ukifika muda tutayasema yote. Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020. Kwanza tumalize hili la Mbowe.
RIP Pierre Nkurunzinza, mwanamichezo uliyeichezea hadi katiba na sheria!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)