Shambulio dhidi ya Mbowe: Kamanda Giles Muroto (RPC Dodoma), umewaona wa kuwakamata? Nakutajia...

Shambulio dhidi ya Mbowe: Kamanda Giles Muroto (RPC Dodoma), umewaona wa kuwakamata? Nakutajia...

Mkuu hapa mantiki yako siioni kabisa. Kama wamemvamia hawakumvamia kama KUB bali kama M/Kiti wa CDM ambaye ndiye anaetegemewa kuiongoza CDM kwenye mchakato wa uchaguzi 2020. U-KUB wake au kurejea bungeni siyo hoja hapa. Tafakari tena.
Ujawaza kwamba anaweza akawa pia anakwepa kupanda na chama chake Jukwaani?? .....kwa Kashfa za Rushwa ,Ngono,ubinafsi/umwamba na zote zimekuja dk za lala salama...ingekuwa ni wewe unatamani tena Siasa?
 
ALi Kessy na Spika kauli zao za kuongeza muda wa rais ni hatari sana!!

Suala la Magufuli kutaka kuongezewa muda wa kukaa madarakani halikuanza jana na kauli za Keisy na Ndugai, hayo ni matamanio ya Magufuli toka mwanzo alipowatuma kina Juma Nkamia na wanaharakati wengine. Wanachofanya kina Ndugai hivi sasa, ni kuhalalisha tu mpango ambao tayari uko jikoni. Kitakachofanyika uchaguzi huu, ni kuchezea box la kura kwa kiwango cha juu, ili bunge lijae wanaccm maalum walioandaliwa na kamati ya uteuzi, na wabunge kadhaa wa upinzani toka kwa Mbatia na Lipumba, ili ajenda hiyo ikiletwa ipitishwe kwa asilimia 100. Hakuna mwanaccm yoyote awe mstaafu au mwingine yoyote atakayeweza kupinga hilo.

Wananchi wenyewe ndio wanaweza kupinga hilo, ila ili hilo litimie, tujiandae kushuhudia mauji ambayo hayajawahi kutokea hapa nchini. Je watanzania watakuwa na uwezo wa kulinda katiba yao? Hilo ni suala la muda.
 
WASIO JULIKANA...MTUHUMIWA NO 1.
images (13).jpeg
 
Mkuu hapa mantiki yako siioni kabisa. Kama wamemvamia hawakumvamia kama KUB bali kama M/Kiti wa CDM ambaye ndiye anaetegemewa kuiongoza CDM kwenye mchakato wa uchaguzi 2020. U-KUB wake au kurejea bungeni siyo hoja hapa. Tafakari tena.
Ina onekana exposure yako ni ndogo na huyu alivyo vamiwa ilikuwa issue ya kisiasa???

on the beat to deter such attacks,' he said ( PA )
A Labour MP was attacked and mugged by a group of up to six people on his way home from Parliament.

Adrian Bailey, MP for West Bromwich West, had his wallet and phone stolen in the attack, which took place in Westminster.
 
Rpc mwenyewe ana wafahamu maana aliona jinsi wanavyo mkanyaga miguuni kutokana na maelezo yake
 
Mzee wangu leo umeamua kutupa kweli Kama jina lako linavyo shabihisha. Sitomkebehi wala kumkashifu bali nitajitahidi kuhoji;

1. Kiongozi Mkuu wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni saa 6 - 7 ulikua wapi bila ya kuwa na ulinzi wa ainayoyote?

2. KUB ni nani aliyemkimbiza hospitali baada ya shambulio?

3. Kauli za kujikanganya za John Mnyika Katibu Mkuu, taarifa ya kwanza hakujibu hoja ya pili taarifa ya pili katuambia wakati anashamvuliwa hakuwa peke yake!

A. Umeongozana na mtu anavamiwa na kuvunjwa mguu usipigwe hata kofi?

B. Aliongozana naye au huyu mtu wa pili alikua mbali na eneo la tukio hivyo washambuliaji hawakumuona?

IWAPO B NDIVYO ILIVYOKUA;
i. Maneno ya kwamba unaisumbua Serikali hayana ushahidi kwakua yanaweza kuwa ya kupika

ii. Hatuna shida ya kukuua ila kukuvunja mguu ili tuone kampaini zako utafanyaje?

Tuna muda gani umebaki kabla ya kuanza kampeini? Mguu unapona baada ya muda gani? Jinsi alivyoonekana jana hakupigwa antena bali POP ambalo hufungwa kwa kuteguka na si kuvunjika?

YOTE TISA KUMI DHANA YA KWAMBA SERIKALI IMEHUSIKA KWENYE TUKIO

Ni upuuzi au mpuuzi kiasi gani anayeweza kumvamia KUB ambaye muda wake uko ukingoni na kurejea ni majaaliwa?

Serikali imvamue Mbowe kwa lipi hasa? Miezi michache iliyopitwa walikua na Golden chance ya kumfunga si wangemalizana naye kule?

MUDA NI RAFIKI MWEMA, IWAPO HOJA HIZO ZITAPATIWA MAJIBU NA AFANDE MUROTTO HIYO NDIO ITAKUA PONA PONA YAKE NA IWAPO MATOKEO YATATHIBITISHA KWAMBA ALITELEZA TU!

MUNGU NDIYE AJUAYE HATIMA YAKE
Umemaliza mkuu
 
Wewe ndo unapaswa kukamatwa kwa kulisingizia Bunge kwamba lilipanga wazungumzaji. Hivi unajua kwamba Mbunge ana kinga na akishaongea ndani ya Bunge hakuna chombo chochote chenye mamlaka ya kumhoji isipokuwa Kamati za Bunge kama kuna haja ya kufanya hivyo?
 
Ujawaza kwamba anaweza akawa pia anakwepa kupanda na chama chake Jukwaani?? .....kwa Kashfa za Rushwa ,Ngono,ubinafsi/umwamba na zote zimekuja dk za lala salama...ingekuwa ni wewe unatamani tena Siasa?
Ina onekana exposure yako ni ndogo na huyu alivyo vamiwa ilikuwa issue ya kisiasa???

on the beat to deter such attacks,' he said ( PA )
A Labour MP was attacked and mugged by a group of up to six people on his way home from Parliament.

Adrian Bailey, MP for West Bromwich West, had his wallet and phone stolen in the attack, which took place in Westminster.
Someni tena ninaemjibu aliandika nini. Na mimi namjibu ya kuwa kuna sababu za anaesemekana amevamia kuvamiwa kisiasa. Yeye alikazia kwa kuwa U_KUB wa mwathirika unafikia tamati karibuni na kwamba kurejea kwake ni hakutarajiwi basi ni upuuzi kumvamia, na hicho ndio nilichomjibu. Sijasema hakuna sababu nyingine yeye kuvamiwa. Nilichambua logic/mantic ya statement yake.
 
Back
Top Bottom