Shambulio dhidi ya Mbowe: Kamanda Giles Muroto (RPC Dodoma), umewaona wa kuwakamata? Nakutajia...

Shambulio dhidi ya Mbowe: Kamanda Giles Muroto (RPC Dodoma), umewaona wa kuwakamata? Nakutajia...

Suala la Magufuli kutaka kuongezewa muda wa kukaa madarakani halikuanza jana na kauli za Keisy na Ndugai, hayo ni matamanio ya Magufuli toka mwanzo alipowatuma kina Juma Nkamia na wanaharakati wengine. Wanachofanya kina Ndugai hivi sasa, ni kuhalalisha tu mpango ambao tayari uko jikoni. Kitakachofanyika uchaguzi huu, ni kuchezea box la kura kwa kiwango cha juu, ili bunge lijae wanaccm maalum walioandaliwa na kamati ya uteuzi, na wabunge kadhaa wa upinzani toka kwa Mbatia na Lipumba, ili ajenda hiyo ikiletwa ipitishwe kwa asilimia 100. Hakuna mwanaccm yoyote awe mstaafu au mwingine yoyote atakayeweza kupinga hilo.

Wananchi wenyewe ndio wanaweza kupinga hilo, ila ili hilo litimie, tujiandae kushuhudia mauji ambayo hayajawahi kutokea hapa nchini. Je watanzania watakuwa na uwezo wa kulinda katiba yao? Hilo ni suala la muda.
Umeongea Ukweli 100% ila hata bunge likipitisha kwa kishindo na wapinzani FEKI kina mbatia na Lipumba wakaunga mkono sisi wananchi hatutakubali kamwe!!! Lazima tuliamshe DUDE ......JMK na BWM wametufanyia vitu vya ajabu sana,hivi kwani JK na BM hawajataka kuongeza muda ,why JPM ndio atake? Mtu anajenga ikulu ya kufa mtu ukiangalia unaona huyu mtu hana nia ya kutoka.
 
Mungu atupe atusaidie kujua kuwatendea mema wengine, Maisha yetu ni mafupi sana, Kwa nini kumtesa mwinzio! Kwa nini kusababishia wengine kifo! Kwa nini kuwasemea na kuwazushia wengine uwongo!

Mimi, namwamini Sana Mh Mbowe ni mtu mwenye Hekima Sana, mvumilivu sana, pia mnyenyekevu Sana, ninaamini atasema Yale yaliyomtokea


Na Kwa Wakati wa usiku wa manane alikuwa wapi, atasema

Na kwamba, Kwa nini hakutembea na walinzi wake siku hiyo, Atasema

Na Kwa nini baada ya kauli Ile kipindi Mh Lisu anapigwa lisasi, Chadema Chama makini kilisema kitajilinda chenyewe, viongozi wake watalindwa na vijana shupavu waliopikwa kijeshi huko Chadema, ilikuwaje tena wakaanza kutegemea ulinzi walioukataa kama Chama' bila Shaka pia atalitolea ufafanuzi,

Hawezi kusema Uwongo
hii kesi imeisha kabla haijaanza.





Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama alilewa, watu wasiseme?!
Tatizo sio kusema Bali tatizo ni kuwa Kamanda alikataza na kuonya atakaeingilia ataruka nae Sasa tunashangaa inekuwaje kashindwa kuruka nao kina Lusinde, Ndugai na Msukuma

Wakati ni dawa ya tatizo lolote ... tunasubiri wakati ufike tupate dawa ya tatizo la CCM bahati mbaya hamkawii kusingizia wale Mbuzi Dume lakini mnasahau mnapoyakoroga Mbuzi Dume hawahusiki hata kidogo
 
Naomba kufahamu kama ukiwa mlevi huwezi vamiwa, that kulewa kwako kunakuwa kinga ya kutovamiwa. Naona issue imekuwa kwamba alionekana anakunywa mpaka muda huo wa usiku na kwa hiyo kama alilewa watu wasiojulikana wasingemvamia na kumdhuru bali alianguka kwa ulevi!!.

Ni vizuri tuviachie vyombo vya usalama vifanye upelelezi na kuonesha ni nini kilimtokea mhanga wa aidha kupigwa au kuanguka.
 
Umeongea Ukweli 100% ila hata bunge likipitisha kwa kishindo na wapinzani FEKI kina mbatia na Lipumba wakaunga mkono sisi wananchi hatutakubali kamwe!!! Lazima tuliamshe DUDE ......JMK na BWM wametufanyia vitu vya ajabu sana,hivi kwani JK na BM hawajataka kuongeza muda ,why JPM ndio atake? Mtu anajenga ikulu ya kufa mtu ukiangalia unaona huyu mtu hana nia ya kutoka.
Kwani ikulu ni nyumba yake binafsi
Pili umeambiwa itakuwa kama dsm sasa kufa mtu imetoka wapi.
Naona uelewa wako wa taarifa una shida.
Na hili la kuongezewa muda mbona bado hata mayai hayajatagwa muenza kuzozana na atakuwa anazoa maji ya kuku
 
Kuna habari kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameshambuliwa na 'watu wasiojulikana' jijini Dodoma alipokuwa akirejea nyumbani kwake usiku wa kuamkia jana. CHADEMA, kupitia kwa Katibu Mkuu wake John Mnyika, wakatoa taarifa ya awali kwa umma juu ya shambulio hilo la Mwenyekiti na kingozi wao huyo wa juu kabisa kwenye chama chao.

Nilipata faraja nilipokuona Kamanda Muroto ukijitokeza mbele ya wanahabari na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kutoa kauli ya Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma kuhusu shambulio la Mbowe. Kwa umakini na ustadi mkubwa Kamanda Muroto ukauambia umma wa watanzania mambo makubwa matatu. Kwanza, uchunguzi dhidi ya tukio hilo umeanza na unafanywa na jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama.

Pili, tukio la Mbowe lisitumike kisiasa na kama mtaji wa kisiasa na yeyote. Na tatu, ni kupiga marufuku mtu yeyote kulizungumzia jambo hilo kwa minajiri ya kuingilia uchunguzi wa kipolisi. Nilikuelewa sana. Nilitamani na ninatamani kuona ukisimamia kauli zako juu ya shambulio dhidi ya Mbowe. Nikupe taarifa au nikukumbushe kama tayari unajua kuwa jana Bungeni Mbowe alikuwa gumzo kwenye mjadala wa kupitisha Azimio la kumpongeza Rais Magufuli.

Kiti cha Spika wa Bunge kikikaliwa na Job Ngugai mwenyewe kiliruhusu mjadala wa tukio la shambulizi la Mbowe. Wachangiaji walipangwa kimkakati ili kutimiza azma yao. Kuanzia kwa Spika Ndugai, Silinde, Lijualikali, Musukuma na hata Lusinde, wote walikejeli tukio hilo na kulihusianisha na ulevi. Walihitimisha kwa kusema kuwa Mbowe alikuwa amelewa na aliteleza kwenye ngazi zake na kuvunja/kutegua mguu wake. Tena akiwa na 'kimada'.

Wabunge hao niliowataja walikebehi na kumkejeli vya kutosha Mbowe na kulikejeli shambulo lake. Tayari wameshaingilia na kuvuruga uchunguzi wa Polisi kwenye tukio hilo. Wanaachwaje bila ya kukamatwa katika kutekeleza kauli ya kamanda Muroto? Wanaopaswa kukamatwa ni Spika Ndugai na Wabunge Silinde, Lusinde, Musukuma na Lijualikali. Wameshaingilia uchunguzi wa Polisi. Wameshakiuka marufuku ya Muroto.

Tunajua kuwa Mbowe anaponzwa na Lissu. Ukifika muda tutayasema yote. Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020. Kwanza tumalize hili la Mbowe.

RIP Pierre Nkurunzinza, mwanamichezo uliyeichezea hadi katiba na sheria!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)
Ipo siku watalipa tu [emoji2955]
 
Hayo ni maoni yako japo ni ya kipumbavu sana; serikali inaweza kukudhuru au kukutoa uhai ata kama wewe siyo Mbunge au KUB.

Suala la Mh Mbowe kutorudi Mbungeni ni baada ya uchaguzi wewe kuisemea utadhani kura imeshabigwa unaonesha ushaidi wa ujinga kwenye hoja yako.

Kumbuka pia serikali isiyolinda raia wake na kutopata wale wote wanaousika kwenye matukio yenye nia ya kuondoa uhai wa raia wake basi yenyewe ndiyo inakua inahusika kuyaratibu hayo matukio.

Kwaushauri japo siyo lazima uipokee; punguza ujinga kwani unaelekea kwenye upumbavu.

ruhi,
Huyu Cheranganya mbona tayari Ni MPUMBAVU alishapita kwene ujinga kitambo Sana.
Unajua Kuna tofauti kubwa sana kati ya MPUMBAVU na MJINGA. Mpumbavu ni mtu ambaye hawezi kuelimika lakini mjinga anaweza kuelimika!
 
Hivi mlimuelewa katibu mkuu Jana wakati anazingumza na waandishi wa habari? Nakumbuka alisema kuna clip ya mtu mmoja hivi siku chache zilizopita ilikuwa inaonyesha kuwa Kuna tukio la shambulio kwa viongozi wa upinzani linaenda kutokea siku chache
Sasa cjui Ni kweli Mnyika alikuwa anamaanisha mi cjui
 
Namsikitikia sana Ndugai

Spika Ndugai ni bonge la MNAFIKI kuwahi kutokea hapa Tanzania na dunia mzima.
Niliona wakti anaingia hospitali kumpa pole Mhe.Mbowe!
Nikasema....huyu?
Aliporudi Bungeni nikamsikia akiongea na Wabunge WANAFIKI wenzake wa CCM akiponda na kusemasema hovyo ati...."nasikia sikia kuna hadithi nyingi kuhusu tukio hilo...! Nikasema....huyu?
Halafu akamwlizia kwa kusema ati,"Waheshimiwa Wabunge Dodoma iko salama.." Non-sense!
Hivi Spika mzima unasemaje Dodoma iko salama wakti Wabunge na Viongozi wake CHADEMA wanaumiza na kukoswakoswa risasi kiasi cha kutishiwa maisha? Hawa watu wasiojulikana ni kina Nani na wako wapi? Ni miaka zaidi ya 2 Polisi hawajakamata hata nzi was kusingizia....! Kwa Hali hii unawezaje kusema Dodoma iko Salama?
 
"---uncharted waters"
Mimi siishi England na sio Mzungu

Ni Mzaliwa wa wilaya ya Moshi Mjini......na SIJAWAHI kutoka nje ya nchi hii ......

Anyways.......thanks. Nadhani simu ilijichanganya
 
Back
Top Bottom