Shame on Efm radio kwa kudhalilisha CEO wa Simba SC

Shame on Efm radio kwa kudhalilisha CEO wa Simba SC

Soon nitaongea na vyombo vya habari nitajaza nafasi ya wazi kwa kusema kosa la Mkude maana hyo nafasi ipo Wazi kabsa.
 
bro namuongelea Barbra siadhani kama dada yako akidhalilishwa utafurahia..itukaneni simba mnavyotaka hata mkitaka kachomeni jengo moto lakini dada wa watu kumdhalilisha kwenye platform kama Efm ni very wrong
Uhuni wa facebook na instagrama unauleta pale?
Akidhalilishwa dada angu ntaumia mm na kulalamika mimi sababu ni dada yangu je we Barbra una uhusiano nae upi? Na ndio maana nikakuambia unachokilalamikia hakina mashiko.
Tafuta pesa ndugu yangu hayo mambo mengine yatakusababishia ugonjwa wa moyo.
 
afadhali kama uli notice hilo ndugu yangu,halafu wanamuita pisi kali huku wanacheka imeniuma sana namuonea huruma sana Barbra she is dedicated lakini. mazingira ya mfumo dume ni magumu sana
watu wana chuki zao na Mo na simba zinamuanguki huyu dada,wampe ulinzi tu kuna siku atadhalilishwa hadharani yule na watu watatetea wakidai ni pisi kali
Uko sahihi mkuu na simamia kile unachokiamini, kwa mtu yoyote mwenye heshima kwa mwanamke haijarishi atakuwa yanga au lipuli lazima ataungana nawewe kwenye hili swala, achana na hawa wakosoaji ndio wanafanya dunia iendelee kuzunguka kwenye muhimili wake
 
Akidhalilishwa dada angu ntaumia mm na kulalamika mimi sababu ni dada yangu je we Barbra una uhusiano nae upi? Na ndio maana nikakuambia unachokilalamikia hakina mashiko.
Tafuta pesa ndugu yangu hayo mambo mengine yatakusababishia ugonjwa wa moyo.
we inakuuma kuona kuna wanaomtetea Barbra asidhalilishwe? udhalilishaji wa barbra uliofanywa na katanga na francis mhando umekusaidia nini?
Huu muda unaopmbania Barbra asitetewe ungekuwa unatafuta hela na kuniacha nipate magonjwa ya moyo
 
Uko sahihi mkuu na simamia kile unachokiamini, kwa mtu yoyote mwenye heshima kwa mwanamke haijarishi atakuwa yanga au lipuli lazima ataungana nawewe kwenye hili swala, achana na hawa wakosoaji ndio wanafanya dunia iendelee kuzunguka kwenye muhimili wake
ndiyo maana hata mwanamke akibakwa utasikia agh alikuwa amevaa nguo ya kubana shauri yake,huko zanzibar mtoto wa miaka 13 kabakwa hakimu anamzodoa kwamba kazoea hakuna hukumu kwa mbakaji
Hapa andhalilishwa Barbra watu wansema agh Mo ni tapeli sana,simba hawajiheshimu ndo maana hawaheshimiwi
 
Kuna msemo kwamba watu wanakuchukulia kwa jinsi unavyojichukulia.

Simba na Yanga zimeamua kuendesha taasisi zao kihuni, hivyo hata hao watangazaji watazichukulia kihuni hivyo hivyo.

Nimezungumzia recruitment criteria ya CEO hapo, ilikuwa ya kihuni.

Tukija kwenye tatizo la Mkude, unapotoa press release ya utovu wa nidhamu kwenye sports, unakuwa obliged kutaja kosa husika kwa uma. Otherwise angepewa adhabu kimya kimya.

Kutotaja kosa unatengeneza mazingira ya uma kujaza kosa wao wenyewe.

Acheni kujiendesha kihuni ili mpewe heshima stahili.
Wanajua kuna mashabiki wahuni pia wanoweza kutoa sababu zao kihuni na zikawa halali
 
we inakuuma kuona kuna wanaomtetea Barbra asidhalilishwe? udhalilishaji wa barbra uliofanywa na katanga na francis mhando umekusaidia nini?
Huu muda unaopmbania Barbra asitetewe ungekuwa unatafuta hela na kuniacha nipate magonjwa ya moyo
Kelele zako zote ni sababu ya Simba wala sio Barbra, kwani ni wanawake wangapi wanadhalilishwa hata kwenye jamii inayokuzunguka na hukuifungulia uzi hapa?

Au hakuna dada yake aliye-date na mwanaume alafu hakuolewa nae? Au unahisi huo sio udhalilishaji?

Utapoteza nguvu nyingi kumtetea mtu ambaye level aliyoko kuna gape kubwa sana mpka ulipo ww.
 
insaikitisha sana hayo mambo kupelekwa redioni kigogo kila siku twitter anaongea kuhusu DC fulani kwamba ni kina fulani lakini hawasemi redioni au wanaogopa?kuna mengine ni ya kuyaacha mtandaoni sababu mitandao ni vurugu kubwa kama kilabu cha pombe ila kwenye redio tena inayosikika mikoa mingi kuongea upuuzi kama huo?

YAANI CEO WA SIMBA ANAITWA PISI KALI CHOMBO YA FUNDI?(MO DEWJI) anyway fani yenyewe ya uandishi wa habari ishakuwa takataka siku hizi
Hizi tafsiri ni za kwao au zako binafsi?
 
Kuna issue ya mchezaji Jonas mkude kusimamishwa na team yake ya simba kwa utovu wa nidhamu, sababu haijatajwa hadi leo.

Lakini kama kawaida ya mambo ya mtandao kuna speculations ikawa inasema MKUDE ALIMTONGOZA CEO WA SIMBA aitwaye Barbra Gonzalez

Huwezi epuka maneno kama hayo mtandaoni lakini dakika 3 zilizopita kwenye kipindi cha sports headquarters amcho bado kipo hewani kina Francis mhando na imma kapanga wamefanya JAMBO LA KISHENZI SANA, naomba ninukuu.

"Nasikia Mkude kakitokea chombo cha fundi, si unajua ni pisi kali ile" aisee kwanza ni dharau sana kwa wanawake wanachokionyesha hawa jamaa sana kwa wanawake. Na hapo wakisema chombo cha fundi wanamaanisha Mo Dewji

Tunajua kuna kampeni kubwa sana ya kuivuruga Simba kupitia media na it is well organised, ila makanjanja kuweni na heshima, Barbra siyo pisi kali ni mwanamke msomi na mchapakazi

Ukisikia mfumo dume ndiyo huu sasa wa jamii yetu, Barbra Gonzalez haangaliwi usomi wake na uchapakazi wake anaangaliwa kama chombo cha starehe na urembo wake ndiyo unamponza zaidi.

Shame on you Efm sikutaraji kusikia ujinga huo redioni
Kutongozwa atongozwe barbara kuumia uumie wewe!
 
Laiti Barbara angekua na sura ya kazi kama ya Ndalichako au Mama Makinda angepewa heshima. Wanawake warembo hawapewi heshima wanayostahili hasa sehemu za kazi.
 
NDIYO MAANA NIMEWAKUMBUSHA KUNA "PISI KALI MKUU WILAYA"kigogo huwa anasema ni CHOMBO YA FUNDI siyo mbaya wakarusha na hayo maneno hapo EFM.

Sasa redio kubwa kama ile inakuwa kama watoto wadogo bana unaokota uchafu wa mtandaoni unauleta redioni kweli?dah ndo maana mwakyembe alikuw anakazania hawa watu wakasome ethics za utangazaji.
Hapa sasa unaanza kuongea kizalendo. Eh! Wilaya ipi ina Pisikali chombo ya Fundi?
 
Iko hivi
Mo anafanya utapeli..
Na watu njaa ndo wanamfagilia..

Tangu lini mwenye hisa 49 anateua CEO?

Kaambiwa Lete bilion 20 hataki

Anatumia club kutangaza bidhaa zake bure

Huyu Barbara alikuwa kwenye kampuni zake..
Kamleta pale aendeleze utapeli wake

Sasa ana Mo foundation ..ili asilipe na kodi kupitia foundation...
Uko sahihi, wacha Mkude ajengewe sanamu pale Msimbazi.... Muddy kazidi utapeli...[emoji41]
 
fungu limetoka kubwa sana ku demonise simba kwa kila hali kwenye media za makanjanja mmekula hela lakini kuweni na mipaka MTUNZIENI BARBRA HESHIMA YAKE KAMA MWANAMKE MSOMI, msitengeneze mazingira ya nchi hii kwamba Mwanamke ni malaya na hawezi kushika cheo kikubwa bila kulalwa.
Huu umbea sasa, yaani mtu atoe hela kuidhalilisha Simba kwa tukio lililoamriwa na Simba? Weka ushabiki pembeni ongea kinachoeleweka.
 
Kuna msemo kwamba watu wanakuchukulia kwa jinsi unavyojichukulia.

Simba na Yanga zimeamua kuendesha taasisi zao kihuni, hivyo hata hao watangazaji watazichukulia kihuni hivyo hivyo.

Nimezungumzia recruitment criteria ya CEO hapo, ilikuwa ya kihuni.

Tukija kwenye tatizo la Mkude, unapotoa press release ya utovu wa nidhamu kwenye sports, unakuwa obliged kutaja kosa husika kwa uma. Otherwise angepewa adhabu kimya kimya.

Kutotaja kosa unatengeneza mazingira ya uma kujaza kosa wao wenyewe.

Acheni kujiendesha kihuni ili mpewe heshima stahili.
Wanatoa hundi ina jina la mlipwaji lakini kiasi anaachiwa mlipwaji ajaze mwenyewe.?
 
Back
Top Bottom