Shamim Mwasha, mumewe mbaroni Dar kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya

Shamim Mwasha, mumewe mbaroni Dar kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya

Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA) imemkamata mfanyabiashara, Abdul Nsebo maarufu Abdukandida na mkewe, Shamim Mwasha kwa tuhuma ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin.

Wanandoa hao wanadaiwa kukutwa na dawa hizo zenye uzito wa zaidi ya gramu 400 nyumbani kwao Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa operesheni wa DCEA, Luteni Kanali Fredrick Milanzi amelieleza Mwananchi kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa Mei Mosi mwaka huu.

Amesema kukamatwa kwa Nsebo na mkewe kumekuja baada ya kukamatwa kwa mtandao mkubwa wa dawa hizo hivi karibuni.

Amesema maofisa wa DCEA baada ya kupata taarifa walienda nyumbani kwa watuhumiwa hao na kufanya upekuzi na kubaini mfuko ukiwa na dawa hizo za kulevya na nyingine zilikutwa katika siti ya nyuma ya gari.

"Tulifanya upekuzi kuanzia saa 8:00 usiku hadi saa 1:00 asubuhi na tulizibaini dawa hizo zikiwa zimefichwa na matokeo ya awali kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali yameonyesha ni dawa za kulevya aina ya heroin.”

“Vitu vingine tulivyomkuta navyo ni simu tano, kadi za benki, hati ya kusafiria pamoja na nyaraka mbalimbali ambavyo vyote tumevichukua,” amesema Luteni Kanali Milanzi

Amesema watuhumiwa hao wana mtandao mkubwa wa kimataifa na kwamba wana majina ya watu wanaoshirikiana nao kutoka nchi mbalimbali ikiwamo Brazil.

Amesema wawili hao bado wanashikiliwa na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Upelelezi kuhusu nini tena hapo?!
 
huu msimu kupata mdhamana tu ni msala hasa kwa dili hizo na uhujumu uchumi

Namkumbuka mwanangu Emba bortion
Mama yake yuko ndani na siku ile emba anakamatwa sisi tulikuwa pembeni tunakunywa pombe
Emba ndy alimponza mama yake
Mama alingilia kuzuia emba asidakwe
Ndy varaganti ikatokea
Mama na mwana wote wakangolewa
Sisi tulitulia tuli tunaendelea na kinywaji
Walipigwa sana mama na mtoto
Ila kuna watu wakasema sijui nani alishuka kutoa amri wakamatwe lkn syo kweli
Ule mchezo mwanzo mwisho tulkuwepo
Na wiki nzima walikuwa wanafatiliwa
Ndomana pale saloon kuna mpaka madem walikuwa wanajifanya Kuja Sukari kmbe wanawasoma tu
So mama na mtoto wako ndani mpaka sahv

Ova
 
Mahita alikuwa anawaambia kabisa kuwa ishakuwa mbaya. Mara nyingine naskia aliwatafutia zengwe na kuwamaliza na ushahidi wote unaishia. Na hapo ni baada ya baadhi ya wakubwa kuanza kulalamikia ujambazi wake nk.
Omary Mahita huyu tunayeambiwa kuwa ni raia mwema?
 
Mama yake yuko ndani na siku ile emba anakamatwa sisi tulikuwa pembeni tunakunywa pombe
Emba ndy alimponza mama yake
Mama alingilia kuzuia emba asidakwe
Ndy varaganti ikatokea
Mama na mwana wote wakangolewa
Sisi tulitulia tuli tunaendelea na kinywaji
Walipigwa sana mama na mtoto
Ila kuna watu wakasema sijui nani alishuka kutoa amri wakamatwe lkn syo kweli
Ule mchezo mwanzo mwisho tulkuwepo
Na wiki nzima walikuwa wanafatiliwa
Ndomana pale saloon kuna mpaka madem walikuwa wanajifanya Kuja Sukari kmbe wanawasoma tu
So mama na mtoto wako ndani mpaka sahv

Ova
we jamaa na uhakika ntakuwa nakumanya sjaanza Leo kuwa na wasiwasi na ID yako salute sana
 
Emba bortion ndo nani tena?
 
Huyu dada aliolewa ndoa ya kwanza na mwanaume mmoja mstaarabu sana. Walibahatika kupata mtoto wa kike. Yeye ndiye chanzo cha ndoa kuvunjika.

Sasa mwana kulitafuta mwana kulipata.
Kila mchuma janga hula na wakweze
 
we jamaa na uhakika ntakuwa nakumanya sjaanza Leo kuwa na wasiwasi na ID yako salute sana
Hamna si unajua ukiwa mzee wa resi nyingi
Lazima ukutane na matukiooo mjini
Mbona sahv ndomana resi za mituko tume punguza maana kukutana na majanga kawaida tu

Ova
 
Sisi wenyewe tuliambiwa tutulie tusiguse sim Dah si unajua wajanja wa kusoma mchezo tukashtuka kuwa hapa ni ambush wanapigwa mtu

Ova

Mpaka uwe karibu ya tukio...lazima ulikuwa ba scanner😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom