Shamim Mwasha, mumewe mbaroni Dar kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya

Nakumbuka Shamim Zeze alianza na Mtaji wa Elfu 10 tu ,akawekeza kidogo kidogo kwenye kibubu akafungua 8020 Fashion baada ya muda akaanza kutembelea Range Autobiography ,Discovery 3 ,kumiliki nyumba mbezi etc

Aisee jela ni chuo cha mafunzo ,washajifunza aiseee waachiwe wakalee watoto wao ,mbona mtoto wa Liyumba alikamatwa na gunia la "BWIMBWI" lakini alitoka?
 
Hivi umeamua kukubali kabisa kuwa bila kuitaja Chadema basi unakuwa huna hoja yoyote yenye mashiko?

Hivi umeamua kukubali kabisa kuwa bila kuitaja Chadema basi unakuwa huna hoja yoyote yenye mashiko
Ndege john alishaokoka hiyo imebaki historia
 
Saf sana haya Mambo ndio napenda kuyasikia...chadema watapinga watasema anaonewa au serikali inataka kick
Hivi umeamua kukubali kabisa kuwa bila kuitaja Chadema basi unakuwa huna hoja yoyote yenye mashiko?
Saf sana haya Mambo ndio napenda kuyasikia...chadema watapinga watasema anaonewa au serikali inataka kick

Ndege john alishaokoka hiyo imebaki historia
Mshauri bas awe anafanya yake Chadema awaachie wenyewe pamoja na machawa wa Ccm wakiongozwa na Lucas mwangomola
 
Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA) imemkamata mfanyabiashara, Abdul Nsembo maarufu Abdukandida na mkewe, Shamim Mwasha kwa tuhuma ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin.

Wanandoa hao wanadaiwa kukutwa na dawa hizo zenye uzito wa zaidi ya gramu 400 nyumbani kwao Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa operesheni wa DCEA, Luteni Kanali Fredrick Milanzi amelieleza Mwananchi kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa Mei Mosi mwaka huu.

Amesema kukamatwa kwa Nsebo na mkewe kumekuja baada ya kukamatwa kwa mtandao mkubwa wa dawa hizo hivi karibuni.

Amesema maofisa wa DCEA baada ya kupata taarifa walienda nyumbani kwa watuhumiwa hao na kufanya upekuzi na kubaini mfuko ukiwa na dawa hizo za kulevya na nyingine zilikutwa katika siti ya nyuma ya gari.

"Tulifanya upekuzi kuanzia saa 8:00 usiku hadi saa 1:00 asubuhi na tulizibaini dawa hizo zikiwa zimefichwa na matokeo ya awali kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali yameonyesha ni dawa za kulevya aina ya heroin.”

“Vitu vingine tulivyomkuta navyo ni simu tano, kadi za benki, hati ya kusafiria pamoja na nyaraka mbalimbali ambavyo vyote tumevichukua,” amesema Luteni Kanali Milanzi

Amesema watuhumiwa hao wana mtandao mkubwa wa kimataifa na kwamba wana majina ya watu wanaoshirikiana nao kutoka nchi mbalimbali ikiwamo Brazil.

Amesema wawili hao bado wanashikiliwa na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Aise maisha haya,Mungu atusaidie
 
Hivi walifanikiwa kutoka?
 
Back
Top Bottom