Naandika ukweli kuhusu Mola wangu.
Nimekufatilia huko juu ukituelezea habari za Malaika, ukaja kwa Wanadamu na Hayawani,mengi umeandika ya uongo isipokuwa machache sana,nikavumilia sana nikasema nikupuuze. Ila hili ka kuhusu Mola kupata kisa amemchoma Mwanadamu mmoja, uzalendo na uvumilivu ukanishinda,nikasema kwanini unamsemea UONGO na Kumzulia Mola wangu, Mola wa Ulimwengu na vyote vilivyomo.
Hasara ni katika hali dhaifu na mapungufu , Mola wetu ni MKWASI wala hapungukiwi na chochote wala hazidishiwi kitu, kwani vyote ni vyake na vipo katika milki yake. Mola wetu ametakasika na udhaifu.
Nasaha zangu kwako na kwangu na kwa wengine tusiwe tunaandika mambo tusiyo kuwa na elimu nayo, na hii ni katika tabia Njema.
Ahsante.