Strictly Syrup
JF-Expert Member
- Aug 4, 2013
- 1,227
- 1,818
Ukiona hivyo ujue hawakuwa na pesa ya dhamana.Kuna madogo wiki iliyopita wamehukumiwa miaka 30 kwa kesi ya bangi...walikamatwa na misokoto mia mbili ya bangi huko babati. (hii ujazo wake ni kama packet kumi tu za sigara)
Vipi kuhusu YANGA OMARY na KIBOKO hio sheria mpya kwanini kwao haikutumika ?Niliona video moja baada ya hukumu dada huyo aliangua kilio balaa ila mshikaji akawa anasema yy alijua yatatokea yaliyo tokea na anasema watakata rufaa kwa kuwaaamuzi ni ya jaji mmoja
Duh nikasema huenda watu wanafanya ma dili bila kujua sideeffect endapo ukitiwa mikononi mwa dola
Sheria mpya inasema mtu akikutwa na madawa kiwango cha gramm 200 + adhabu yake ni jela maisha
Na mtu akikutwa na madawa kiwango cha gram 200 (kushuka chini) jela miaka 30.
Hapa kweli serikali imeamua kutokomeza biashara hii haramu
Hivi insta anatumia jina ganihuyu dada alikua na kamsemo kake
ni bora kulia kwny range kuliko kulia kwenye bodaboda
aisee hakujua yajayo mtoto wa watu
Umemalizaaa....!!!!Nilichogundua huu uzi umeingiliwa na watumiaji wa hizo madawa wengi wanasapoti uuzwaju wa haya madawa bila kujua athar ambazo wameachan huku mtaani
Kama madawa haya n mazuri basi wangetumia wao wenyewe na kuwapa watoto wao lakn hukuti wakifanya haya wanataka familia za wengne ziangamie kwa kigezo cha kutafuta pesa
HALAFU Kuna hili swala wengi wanadai SHAMIMU alikuwa mtu poa usichojua wauzaji wengi wa hiz mambo hujifanya watu poa wenye huruma Sana na wanatoa misaada mingi had unashangaa siku mtu akikamatwa majiran wote wanakuwa upande wake sababu hakuonesha tabia au viashiria vya uuzaj wa ngada kitaalam tunaita kujivika ngoz ya KONDOO wakat wewe n CHUI
Kwa sisi tuliobahatika kuish maeneo yenye changamoto hizi tunajua uhalisia wa haya mambo na jins vijana wanavyoteseka tembelea SOBER HOUSE waulize waathirika wa madawa watakuambia mtiti wa kuachana na madawa ulivyo mgumu
Msidanganyike na sura upole na misaada wanayotoa hao watu mkadhan kwamba wao n wema hiyo n zuga tu wanawabrain wash ili muamini kuwa n watu salama CHONCHI alienda mbali akawa ananunua magar ya vituo vya polisi na kujaza mafuta magar yao unategemea polisi gan angeweza kumkamata kiurahis kwa network aliyokuwa nayo
Ndio maana mm namkubali Rais wa PHILIPPINES HON DUTERTE yeye n mwendo wa shaba tu hana mzaha wamexico waliiteka Philippines Kama yao kwa usambazaji wa ngada nasisi tulikuwa tunaelekea huko
Kiukwel nilipingana na the late Magufuli kwa mambo mengi ila kwenye hili la ngada nilimuunga mkono kwa asilimia zote namuomba na madam president naye akomae na biashara hii had kieleweke
AminNaandika ukweli kuhusu Mola wangu.
Nimekufatilia huko juu ukituelezea habari za Malaika, ukaja kwa Wanadamu na Hayawani,mengi umeandika ya uongo isipokuwa machache sana,nikavumilia sana nikasema nikupuuze. Ila hili ka kuhusu Mola kupata kisa amemchoma Mwanadamu mmoja, uzalendo na uvumilivu ukanishinda,nikasema kwanini unamsemea UONGO na Kumzulia Mola wangu, Mola wa Ulimwengu na vyote vilivyomo.
Hasara ni katika hali dhaifu na mapungufu , Mola wetu ni MKWASI wala hapungukiwi na chochote wala hazidishiwi kitu, kwani vyote ni vyake na vipo katika milki yake. Mola wetu ametakasika na udhaifu.
Nasaha zangu kwako na kwangu na kwa wengine tusiwe tunaandika mambo tusiyo kuwa na elimu nayo, na hii ni katika tabia Njema.
Ahsante.
Kabisaaaunamjua abdul vizuri ndugu yangu???
kama umewahi kuwajua hata kwa bahati mbaya wauza ngada wa town wa miaka 10 iliyopita jina la abdul nsembo haliwezi kuwa geni masikioni mwako
huyu na wenzake kina rumishael shoo wamepiga sana dili za ngada wenzake walistuka mapema wakakimbilia south na wengine kuwa low key baada ya gwiji lao shkuba kubebwa na DEA sema huyu abdul alijiona yeye ana mbinu kama za medelin cartel akaendelea kuflex
makonda ana mabaya yake lakini kwenye hili la abdul mtakuwa mnamuonea tu
shamimu kapigiwa kelele sana mitandaoni miaka ya nyuma sana n kina mange kuwa aache kuwadanganya wadada wa mjini kuwa biashara inalipa wakati fika anajua hela anazoflex nazo zinatokana na ngada
adhabu waliyopewa wanastahili kabisa bora mtu akupe ukimwi utakula ARV's kuliko kukufanya uwe adict wa cocaine, meth, au heroine hii kitu mbaya sana
Hahaaaa dahWakipeana mimba
Kama alikuwa anauza kweli,Basi hata Kama aliwekewa madawa ni sawa tu,kufungwa kwake maisha ni faida kwa Taifa,kwani cargo za madawa mtaani zitakuwa zimepungua kiasi fulani.Makonda na team yake waliwaekea Madawa ya kulevya kweli nsembo alikuwa anauza Unga na sio shamimu Sema nsembo hakuwa na Unga ndani kawekewa na kina makonda na team yake inauma sana na Mungu atamlipa makonda na uzao wake
Kweli kabisa mkuu. Na hu ndiyo msiba mkubwa zaidi tulio nao kwa sasa kama taifa.Tatizo misemo ya "woga wako ndio umaskini wako" siku hizi wadada wanaishadadia sana.
Msichana yuko tayari kukuona hata unaua ili mradi uwe na pesa,na utapendwa kama malaika.
Thamani ya utu wa mwanamke imeshuka kwa sababu ya wao kujifanya bidhaa inayoweza kununuliwa kwa pesa bila kujali ni za majini,mizimu au za damu.
Kesi ya uhujumu uchumi haina dhamana mzee babaUkiona hivyo ujue hawakuwa na pesa ya dhamana.
Nina shuhuda nyingi watu wamedakwa na stick 300+ na bado wapo mtaani.Kesi ya uhujumu uchumi haina dhamana mzee baba
Hizo zinamalizwa polisi kiuungwana...ikienda mahakamani ni habari nyingine, hapo labda ushahidi usijitosheleze, kwahiyo bado huruma ya polisi inahusika...ila wakiamua kukukomalia, nyundo nyingi zitakuhusu...ila kiukweli kumfunga mtu miaka mingi kwa kesi ya bangi ni uonevu..hiyo sheria iangaliwe upyaNina shuhuda nyingi watu wamedakwa na stick 300+ na bado wapo mtaani.
Hiyo ni cocaine mwana. Heroine ni habari nyingineSema hapa tz tunaoneana tu huko mtu anakutwa na tani 2 na bdo anafungwa 11yrs na bdo anaweza kutoka kablaView attachment 1743042
Jela maisha kwa sheria za Tanzania maana Yake nn?"Kupanga nikuchagua" jiwe.
Hicho ndo walichokipanga na mahakama imeamua kuthibitisha uchaguzi wao.
Nawatakia maisha mema huko jera pia iwe fundisho wa waliobaki huku mtaani.
Indefinite sentence. Until death do you apart.Jela maisha kwa sheria za Tanzania maana Yake nn?
Dah, kwa hiyo unatala kusema ameonewa?Makonda na team yake waliwaekea Madawa ya kulevya kweli nsembo alikuwa anauza Unga na sio shamimu Sema nsembo hakuwa na Unga ndani kawekewa na kina makonda na team yake inauma sana na Mungu atamlipa makonda na uzao wake
Till death do you part [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] nimechekaIndefinite sentence. Until death do you apart.
Indefinite sentence. Until death do you apart.
Yaaaap. Nchi nyingine kaka Norway, life sentence has a maximum of 20 years. Na kwingineko 30 years. Hapa kwetu ni indefiniteKama ndoa [emoji3]