Shamimu Mwasha na Abdul Nsembo wahukumiwa kwenda jela maisha baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha Dawa za Kulevya

Shamimu Mwasha na Abdul Nsembo wahukumiwa kwenda jela maisha baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha Dawa za Kulevya

If you ask me to define Shamimu, I will tell you this; A home girl type with dreams to conquer the world!

Unfortunately she took it by hooks or crooks! Ikamponza!

Maisha ni Fumbo la Imani! Tulizingatie kabla ya tamaa zetu!
Tangu yupo kwenye kile kigari Cha blue alkuwa na dreams kubwa Sana kuliko alivyo na watu wanaomzunguka akiwaangalia mashost zake ndo kabisaa na jamaa dini ilvyoanza kuingia akaona sasa Mambo kwishne sema inaonekana kutokota anako tangu kitambo sema ikizid ndo watu huja kujua
 
Kama unamkumbula Shamimu hakuwa na makuu kabisa mwenyewe akipiga picha zake kwenye shughuli na kiblog chake maisha yanaenda na ustaadh wake yule baba Iqra,sasa dharau za kina Mange kumfanya kama housegirl fulani hivi na vile muda mwingi anapigana nao vikumbo na shetani akikuchagua huchomoki ila nimeumwa sana.shamimu kabla ya Abdul alikuwa na roho nzuri sana Mmungu amfanyie wepesi huko aliko
Kabisa aisee Shamim aka ZEZE alikuwa mtu safi sana na nina imani bado ni mtu safi mpk leo ni upepo mbaya (shetani) tu ulimpitia. Personally nafahamu sana Shamim tena toka enzi zile ndie mratibu wa Darhotwire. Alikuwa mpambanaji na kaduka kake kadogo pale Sinza 8020 fashion. Nakumbuka alikuwa akileta nguo ananijulisha nikamchagulie wife

Darhotwire ilivyokufa nilipoteana nae ila kuna siku from nowhere alinitumia e mail (simu nilibadili) nakuniambia anaolewa nikachukue kadi yangu pale 8020 Mapambano. Niliudhuria ile harusi na ilikuwa ya kubwa sana na ya kifahari.

Sikujua kama mwisho wake utakuwa hivi. Alipokamatwa niliwahi kuwaza niende kumtembelea Segadansi ila sikulifanikisha hilo. Nilikuwa najua kuwa haya matatizo yamemkuta ila hakuwa hivyo nadhani ali-team up na mtu asiye sahihi na akashindwa kujitoa na kuamua kumlinda. Hilo ndio lililom-cost.

Shamim ni dada mmoja mwenye roho nzuri na ya kipekee. Pia nakumbuka aliwahi kuwa judge kwenye kumsaka Mfalme wa Rhymes ambapo alishinda Afande Sele. Kila mwanadamu ana mapungufu na pia hatujui kesho yetu. Sijui kama ni kweli alikuwa anajihusisha na hayo madawa wala siwezi kusema alifanya.

Kwa roho yake, namwombea afanye toba kwa Mungu wake na nina uhakika MUNGU atatenda miujiza
 
Inauma na inachoma shamimu kufungwa maisha na dada wa watu hauzi Unga na aliewaekea Unga ni makonda huyu makonda huyu Mungu atamuonesha kabla hajafa na uzao wake ni Roho mbaya sana.

Duh kwani hawakufanya uchunguzi,na makonda mbona hana nguvu tena kisheria,kama unao ushaidi si na yeye mkakate rufaa aunganishwe kwenye Kesi?
 
Makonda na team yake waliwaekea Madawa ya kulevya kweli nsembo alikuwa anauza Unga na sio shamimu Sema nsembo hakuwa na Unga ndani kawekewa na kina makonda na team yake inauma sana na Mungu atamlipa makonda na uzao wake
Yan alipwe kwasababu gani? Hv mnajua madhara ya madawa ama mnasikia? Acha tu jaman wafungwe, hakuna kitu kinauma unapishana na vijana wadogo wanabembea mchana, Kama mumewe aliuza maana ake na mke anajua mume anauza wanahusika maana wao ni mwili mmoja.
 
Watu kama hawa ilipaswa Serikali iwaahidi adhabu kidogo kwa makubaliano ya hawa kuutaja mtandao wao woooote kuanzia huko nje na humu ndani. Kuwatupa ndani maisha bila kuwakamua information za kutosha haitoshi
Tatizo hawasemagi, wanajikuta wao ni wajanja, bado Muna nasikia nae mule mule
 
Kabisa aisee Shamim aka ZEZE alikuwa mtu safi sana na nina imani bado ni mtu safi mpk leo ni upepo mbaya (shetani) tu ulimpitia. Personally nafahamu sana Shamim tena toka enzi zile ndie mratibu wa Darhotwire. Alikuwa mpambanaji na kaduka kake kadogo pale Sinza 8020 fashion. Nakumbuka alikuwa akileta nguo ananijulisha nikamchagulie wife

Darhotwire ilivyokufa nilipoteana nae ila kuna siku from nowhere alinitumia e mail (simu nilibadili) nakuniambia anaolewa nikachukue kadi yangu pale 8020 Mapambano. Niliudhuria ile harusi na ilikuwa ya kubwa sana na ya kifahari.

Sikujua kama mwisho wake utakuwa hivi. Alipokamatwa niliwahi kuwaza niende kumtembelea Segadansi ila sikulifanikisha hilo. Nilikuwa najua kuwa haya matatizo yamemkuta ila hakuwa hivyo nadhani ali-team up na mtu asiye sahihi na akashindwa kujitoa na kuamua kumlinda. Hilo ndio lililom-cost.

Shamim ni dada mmoja mwenye roho nzuri na ya kipekee. Pia nakumbuka aliwahi kuwa judge kwenye kumsaka Mfalme wa Rhymes ambapo alishinda Afande Sele. Kila mwanadamu ana mapungufu na pia hatujui kesho yetu. Sijui kama ni kweli alikuwa anajihusisha na hayo madawa wala siwezi kusema alifanya.

Kwa roho yake, namwombea afanye toba kwa Mungu wake na nina uhakika MUNGU atatenda miujiza
Kabisa nashangaa watu wanamuongelea tofauti humu kama shetani fulani,kosa lake ni hilo tu kuolewa na shetani mwisho yeye nani asimlinde mume wake tuache kuhukumu tutahukumiwa....Mungu amfanyie wepesi Shamimu kwa kweli!
 
Niumie kwa lipi? Duniani kote huwa inajulikana.
Hao wanaosema vijana wameharibika kwa madawa (mateja) ndiyo nawashangaa. Kwani umelazimishwa ununue madawa ya kulevya ubugie?
Na wao kwani walilazimishwa wauze madawa...tit for tat
 
Hata yule Top, Mbunge wa Kinondoni alitajwa kuwa ndio muingizaji wa powder nchini na wenzake watatu, wote Waislam

Kifupi Uislam hauchukulii kuwa Kuuza au kutumia Heroine n.k ni dhambi wanaita Makurughu kama sigara tu

Yaani wanaipenda hii Biashara kuliko yoyote nyingine.
Hivi nyie mambo yenu ya udini si mkamzungumze inbox..mnataka kuharibu uzi ili mods waufunge
 
Nimewaza kuna watoto na vijana wangapi wamekua mateja, wamekufa, wameuwawa, wamebakwa na wengine kufungwa magerezani sababu ya biashara ya hawa watu wawili nikaishia kujijibu japo wana watoto wadogo wakapumzishwe tuu huko wanakopelekwa.
Na Mungu akawasamehe watoto wao kwa dhambi walizofanya wazazi hawa. Wakue wakiwa salama na wakiwa na amani ndani yao
 
Sheria zetu nyingi, nyuma yake watungaji na watia saini ili zitumike wamekuwa ni watu wenye roho mbaya na wabinafsi na wenye roho za kukomoa. Hawavai uharisia wa kile wanacho kipitisha, na hawana hofu. Nilikua najua mtu anaefungwa maisha ni yule alie tishio kwa nchi au dunia.. ila hawa adhabu hiyo ina chuki na roho mbaya.. Mungu afanye mioyo ya wahusika kuwa milaoni na yenye tumaini la kumtumaini zaidi Mungu, awaondolea uzito na mawazo mioyoni mwao, aweke peace, joy and love
Mimi nilijua madawa ya kulevya ni tishio kwa nchi na dunia pia. Objective is to deter or prevent that particular offender and other future criminals from committing further crimes.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
stori ya kitoto....askari walikwenda kusachi nyumba wasingeweza kuondoka kiboya namna hiyo
Kabisa ni stori ya uongo hiyon. Nanukuu ushahidi wa askari toka mahakamani "Tulivyoenda tulimkuta Shamimu mke wa Abdul Nsebo mtuhumiwa tukamuuliza mumewe yuko wapi akawajibu askari ana wiki mbili hayupo nyumbani sababu za ugomvi wao. Askari waliomba kupekua nyumba shamimu akawataka awasachi kwanza kabla hawajapmpekuwa

Baaada ya kumaliza kuwapekuwa askari , askari hao waliingia ndani na moja ya chumba chao waliona vipande vya Gympsum (sealing board) chini vimedondoka! Kuashiria kuna mtu alipanda darini!! Askari hao walipanda darini na kumkosa lakini baadae nyuma ya mlango wa Tank la maji walimuona Abdul Nsebo amejificha....na kumtia Pingu alikutwa na Passport za kusafiria na kiasi cha hela na drugs"
 
Back
Top Bottom