Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Baraka Shamte ni mwanasiasa nguli visiwani Zanzibar ambae pia ni mtoto wa Waziri mkuu wa Kwanza wa Zanzibar, Mohammed Shamte amesema Rais wa sasa wa visiwa hivyo, Hussein Mwinyi hatoshi kuendelea baada ya miaka yake mitano kwisha.
Shamte amesema miaka yake mitano inakwisha na kurudia kosa ni matatizo ilhali katiba ya chama na nchi hamna inayosema Rais lazima atawale miaka 10.
Shamte ameendelea kusema CCM kikiwa makini yatatokea kama ya Idriss Abdulwakil ambae baada ya miaka mitano akaambiwa apishe na kutafutwa Rais anaefaa. Shamte amesema yeye anasema wazi yeye kama Baraka na hata uchaguzi uliopita alikiheshimu chama.
Jana Shamte akafutwa Uanachama na kupata kipigo kutoka kwa watu wasiojulikana.