Shamte: Katiba ya nchi haijasema 'Head of State' atawale miaka 10, miaka mitano ikiisha tutafute Rais mwingine lakini siyo huyu

Pascal Mayalla, wewe ujiitaye "mwanasheria" uko wapi babu...?

Usi - like tu. Sema huu ni u - Kangaroo wa aina gani kweli uliofanywa na CCM chama chako..?

How come mwanachama wa CCM atoe maoni tu kisha afukuzwe bila hata kusikilizwa na zaidi sana apigwe na kujeruhiwa..?
 
Wazazi mzaapo tuleteeni WATOTO aina ya BARAKA. Amen
 
Huku mtaani tunajiuliza maswali kuwa:

Mzee wa Ruksa au yule wa msoga pekee ndo wana uwezo wa kuzaa Marais na mawaziri pekee?

Je yule CEO wa kwanza pwani watoto wake Wana akili kuizidi watoto wetu?

Swali lingine Rahisi ni kuwa Hivi pale Mwitongo, hakuna mtoto wa Nyerere hata mmoja anaequalify urais au hata UWAZIRI? Mf Madaraka!!

Je hakuna hata mjukuu mojawapo wa Nyerere mwenye dalili za kuja kuwa kiongozi?

Ni maswali tu mtaani, mnawaza yapuuza mkipenda.
 
Ndugu Pasco Mayala anasahau kuwa AKILI mtu huzaliwa akiwa nayo, Na ELIMU huja Kuongeza baadhi tu ya yaliyopo.
 
Mkuu

Yule madaraka NYERERE alikiri wazi kuwa marafiki wabaya walimuingiza mkenge!!

Yaani analaumu system haikumlinda na ubaya FULANI wa watu yaani alitegwa Sana asiwe mtu MKUBWA!

Tena anampa hongera Mwinyi kuwa aliepuka mtego wa marafiki wabaya Hadi akawa vile!

Ni kana kwamba kulikuwa na juhudi za dhati kabisa kuipoteza familia hii isichipue kwenye uongozi wa nchi yetu hasa wanamtandao ndio wamehusika kabisa Hawa jamaa wasichipue kwenye harakati za kushika hatamu wakijua fika watapata uungwaji mkono mkubwa na watu wengi na kuharibu wizi na UFISADI wao!!!


Labda vitukuu na vilembwe vitachomoza Baada ya katiba Mpya!!

TUSUBIRI
 
Makongoro ndiye aliongea hayo.
 
Alisema marafiki wabaya wamemponza Sana!na kumsifu Mwinyi kuepuka marafiki wabaya Hadi kufika alipo!!!!

Jiulize analaumu nani kama sio system!!?
Kama Nyerere kapotezwa hivyo, watoto wa Maagu ndo hutowasikia tena hata vijukuu.

Yule wa Lupaso ndo hakujaaliwa.

Ama Kweli: NI MASHAKA NA HANGAIKO, WEMA HAWANA MAISHA. Msanii mmoja aliimba enzi hizo.
 
Hapa hautamuona akisema chochote.
 
Kama Nyerere kapotezwa hivyo, watoto wa Maagu ndo hutowasikia tena hata vijukuu.

Yule wa Lupaso ndo hakujaaliwa.

Ama Kweli: NI MASHAKA NA HANGAIKO, WEMA HAWANA MAISHA. Msanii mmoja aliimba enzi hizo.
Kwani wewe ndiyo unapanga mafanikio ya familia ya Magu kwa taarifa yako watoto wa Magufuli ni vichwa Ndiyo maana siyo chawa.Chezea msukuma wewe, hawajikombi kwa mtu.Wale ni wafugaji na wakulima hawana shida.Watoto wa Magufuli wanalamba asali ya kutokana na ufugaji wao, siyo wengine kutwa nzima wanawaza kuwa Marais.Pathetic getegete
 
Yaani mnalea watoto trgemezi, baba akiwa mkurugenzi basi familia nzima ni wakurugenzi.Hongera sana Magufuli alilea watoto kwa mentality ya kujitegemea.Ndiyo maana Mzee akaja na slogan ya Hapa KAZI TU
 
Hakuna namna. Mzee ameshafunguka. Na inawezekana mzee anawawakilisha wengi wenye maoni kama ya kwake huko visiwani.
Wazanzibar wengi huko mitaani hawampendi kabisa mwinyi labda Kama wanaziba masikio au mashushushu hawampelekei ukweli Rais
 
Si tumeambiwa wasiojulikana hawapo awamu hii ya sita?
 
Huu ni Uongo wa hali ya juu. Hakuna ushahidi wowote na ni maneno tu kama yalivyo maneno mengine.
 
Rubbish 🚮🚮🚮🚮🚮
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…