Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I Got you mkubwa, nitaufanyia kazi ushauri wako! Kweli ndugu sometimes miyeyusho!afanye uamuzi kutokana na moyo wake unachotaka. Mwisho wa siku yeye ndo ataishi na mwanamke alomchagua c ukoo wala shangazi.Meanwhile amwambie shangazi arudi na huyo binti!Pia asimame kidete maana ana vita kali mbele yake.Halafu haya mambo mengine uduwanzi sana, raha ya maisha ufanye maamuz mwenyewe uanguke au kufanyikiwa mwenyewe sio watu watoke wanakotoka kuja kuharibiana maisha na taratibu!
Mila ni mila mkuu, we cant escape from our traditions. Nimekusoma vyema, sometimes we have to stay focused in what we believe to be right!Huyo rafiki yako atambue kuwa mke yeyote atakayeoa hataishi na shangazi yake, mjomba, wazazi au watu wengine wa ukoo. Ni yeye atakayeishi naye. Yeye ndiye atakayekabili uzuri na ubaya wa huyo mke. Kwa hiyo ni LAZIMA afuate chaguo la moyo wake hata kama sio chaguo la wazazi au ukoo wake kwa kuwa hayo ndiyo maisha yake yote yaliyobaki. Watu wa ukoo watapinga sana lakini baadaye watasalimu amri. Tusiendekeze vimila VILIVYOKAUKA tayari.
Hivi wazee wa zamani dhana ya mapenzi ya dhati iliwapita eeh?Moja ya mila potofu tunazopigania zitoweke nipamoja na hiyo!Mimi nadhani aende kule kijijini akawaelimishe wazee wa pande zote kwa hekima na ustaa! Huku akitumia mbinyo kuwa tayari anae mchumba ampendae kwa dhati! Asisahau kuwaomba watu wawili au watatu wenye hekima aambatane nao katika kuwaelimisha wazazi wake hii itaongeza uzito wa hoja zake!!
Shangazi anatekeleza maagiza ya kikao cha ukoo mkuu, that means kwamba ukoo ndio umeamua!Wala hakuna issue hapa. Ni kuoa mwanamke unayemtaka, wewe shangazi yako anakuhusu nini? At this age, shangazi yako atoke kijijini akupe mwanamke na wewe unakubali!You will need your head examined!
Nimekupata mkuu, hata mimi nilikua nadhani hivi bt sikua na uhakika kama nipo sahihi!ni rahisi sana.....kwa kifupi awambie kuwa yeye ni mtu mzima ana maamuzi yake katika maisha.kuhusu swala la kuoa aseme tayari amefanya maamuzi yake ana ana mchumba .....amshukuru shangaza na ukoo wote kwa kumchagulia mke lakini awambie hataweza kumuoa......maana si chaguo lake.......asiweke bla bla nyingi....
Najua anampenda sana mchaga bt shinikizo la ndugu ndio tatizo!
Ndio mkubwa nimekupata! Unajua mi naenda mbali nahis swala la ukabila linaingia hapa. Kwa anayejua wasukuma vyema anaweza tueleza tabia zao?Hakuna tatizo bana! Yeye ndiye muoaji na ndiye atakayeishi na mkewe na si nduguze. Haya mambo ya kuoa kwa kushinikizwa ndio baadaye ndoa ikishindikana unabaki na majuto makubwa kwanini niliamua kusikiliza shinikizo la ndugu. Mwambie awaambie nduguze kwamba tayari ana mchumba wake wanapendana yuko masomoni na akimaliza tu watafunga pingu za maisha. Asikubali ndoa ya kushinikizwa.