Majaji wa ukweli walikuwa akina Nyalali, Mzavas, Rugakingira, Korosso, Mroso, Kisanga nk.
Hao hawakujua cha rais wala cha nani, wao walikuwa wanakufa na kitabu tu kinasemaje, Nyerere alipoona hivyo akaanzisha sheria ya kuweka watu kizuizini bila kufikishwa mahakamani enzi hizo maarufu kama (Detention Without Trial).
Nyerere alichoka kwani alikuwa akimburuza mtu mahakamani kwa hizi tuhuma za kipuuzi majaji walikuwa wakiwaachilia huru kiulaini kwa madai ya kukosekana kwa ushahidi madhubuti.
Kwenye vyesi vya uhujumu uchumi mwaka 1984-1985 watuhumiwa waliachiliwa huru kwa kile majaji walichodai kuwa "Sheria ya uhujumu uchumi ilikuwa batili".
Wale ndio walikuwa majaji lkn hawa wa leo ni wachumia tumbo tu na makanjanja wa kisheria.