Shangazi: Tume ina majaji 4 lakini wote kama hawajui sheria na hukumu ipo kuwa Maandamano huwa hayahitaji kibali

Tuna majaji wa majina ambao kiuhalisia uwezo wao ni afadhali hakimu wa mahakama ya mwanzo mwenye weledi.

Majaji wetu wanaharibiwa weledi wao na ukada wao kwa CCM.

Kuna wajinga wengi tu unasikia eti ili uandamane unahitaji kibali cha Polisi! Unashangaa kama hawa watu huwa wanasoma sheria au ni tutusa wa kutenda lakini waliobeba vyeti vya usomi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa majaji wa awamu hii wamejishusha hadhi sana
 
Majaji wa ukweli walikuwa akina Nyalali, Mzavas, Rugakingira, Korosso, Mroso, Kisanga nk.

Hao hawakujua cha rais wala cha nani, wao walikuwa wanakufa na kitabu tu kinasemaje, Nyerere alipoona hivyo akaanzisha sheria ya kuweka watu kizuizini bila kufikishwa mahakamani enzi hizo maarufu kama (Detention Without Trial).

Nyerere alichoka kwani alikuwa akimburuza mtu mahakamani kwa hizi tuhuma za kipuuzi majaji walikuwa wakiwaachilia huru kiulaini kwa madai ya kukosekana kwa ushahidi madhubuti.

Kwenye vyesi vya uhujumu uchumi mwaka 1984-1985 watuhumiwa waliachiliwa huru kwa kile majaji walichodai kuwa "Sheria ya uhujumu uchumi ilikuwa batili".
Wale ndio walikuwa majaji lkn hawa wa leo ni wachumia tumbo tu na makanjanja wa kisheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…