Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Kuwa siriaz mkuu dude kubwa kam ilo unasahau vip ulikoweka?
 
Mimi naweka malengo account ya NBC Kila mwezi nakatwa direct kutoka kwenye mshahara kwa mwaka mzima imenisaidia sana.njia ya vibubu ilinishinda nilikua navunja kabla sijafikisha malengo.
Hebu tupe faida yake Mkuu, vipi kuhusu,

- Makato ya kila mwezi
- Account Maintainance Charges
- ATM charges PLUS Salio request charges
- Kodi
- Withdrawal charges
- Processing fees ?

Au ndo yale ya kuweka Tsh 100,000 baada ya mwaka unakuta kuna Tsh 75,000/- ???
 
Niliona nifungue 3 acc moja kama saving nyingine matumizi ya kawaida na nyingine dvt plus emergency
Unfortunately hiyo ya saving inaishia kwenye adventure tu
 
Mimi naweka malengo account ya NBC Kila mwezi nakatwa direct kutoka kwenye mshahara kwa mwaka mzima imenisaidia sana.njia ya vibubu ilinishinda nilikua navunja kabla sijafikisha malengo.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Kumbe tupo wengi?

Mimi nina idea nyngine ila ni kam kibubu

Ila ii ni kwa ajili ya kutunza sarafu

Usitupe kopo LA pafyumu ukishamaliza matumiz zen toboa tundu kwa juu la kuwezesha kupita sarafu na weka sarafu mpaka lijae na litajaa haraka natumai mpak linajaa basi kopo LA pili LA pafyumu litakua limeisha


Apo iyo hela ya kopo LA kwanza itakusaidia kweny matumizi madogo zen unaanza kuweka LA pili
 
Nitaijaribu hii mana nilikua naweka sarafu kwene mkoba mbona ilinishinda
 
mie nina mbinu ambayo naitumia katika kazi kama za ujenzi ambayo uwa sifanyi saving kama hizi mlizozizoea za kuweka fedha kwenye kibubu au mpesa. Nachofanya ni kuandaa ramani na kisha makadirio ya ujenzi (BoQs) kisha nongea na wauza vifaa nakuwa napeleka fedha kidogo kidogo zikikamilika nachukua vifaa kuanzia msumari, nondo mpk cement uwa nafanya hivi. Kwa kweli imenisaidia mpaka sasa nimekuwa kimasamaki Fulani hivi nyumba Zaidi ya nne
 
Malengo account haina makato yoyote ingawa sijafatilia wakati wa kutoa Pesa kama nilikatwa chochote.mara nyingi sms zinazoingia toka bank ni faida wanayoingiza japo ni ndogo
Mimi siweki kwa ajili ya faida isipokua kutunza hela tu kwa lengo la kufanya kitu kikubwa kwa wakati nilioupanga
 
Nitaijaribu hii mana nilikua naweka sarafu kwene mkoba mbona ilinishinda
Ii IPO San tena haina haja ya kuwa na haraka saan ,cha msingi unasubir mpak pafyumu iishe ndo unapasua ile ya kwanza zen inakua endelevu sas

Faida kubwa ni kuwa lile kopo sio kubwa saan so litajaa mapema tu
 
Sio salama pia, bank ikizingua utaambulia mil. 1.5 tu.
 
Hongera hujawahi kutana na changamoto zozote zile ?
 
kwa mfanya biashara au mjasiriamali hawezi weka pesa benki miaka mitano bila kutoa, huko ni kukosa akili ya fedha. Pesa inatakiwa izalishwe, hiyo hesabu uliyopiga ww kwa mtu smart ndani ya miaka mitano inatakiwa awe na shilingi 150M hadi 300M.

Kwa kuongea eti itafika 150m ni rahisi kishenzi,ingia kwenye utekelezaji ndo utaona mziki wake.

SMARTNESS IS OVERATED.
 
Tumeanzisha mfumo wa SILC( Saving and Internal Lending Community) ofisini..naweza kuweka hadi 250,000 kwa mwezi.. Pia mwanachama anaweza kupata mkopo na kurudisha kwa riba ambayo ni 5-10% kulingana na kiasi anachochukua na muda..Uzuri ni kwamba wote ni wafanyakazi hapa na ukishasave hela yako huna mwisho wa mwaka tunafanya share out, unapata hela yako yote uliyosave na ile riba iliyopatikana inagawanywa..Ingekuwa kibubu maana yake ile unayoweka ni hiyo hiyo haiongezeki
 
Hahah Aisee unaweza kushangaa hapo ndani umefungua kakiwanda kadogo kakukusanyia makopo ya pafyumu vyenye vitobo juu aisee.
 
NJIA NZURI YA KUHIFADHI PESA NI KUWEKEZA. Kila upatapo ziada wekeza kwenye biashara ndogo ndogo. Wahenga wa zamani wanasema ndo ndo ndo si chururu.

Mkuu kwa mazingira ya biashara kwa sasa ndani ya tz ni ngumu kuwekeza kwa mtaji mdogo. Kila leo biashara zinaporomoka kutokana na utitiri wa kodi ambazo hupukutisha mtaji zaidi.
 
Mshahara wako unaingilia bank hiyo hiyo ?

- Na Je, nikisema niweke miezi 6 inakubalika au ni kuanzia mwaka !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…