Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

Share Idea yako unayotumia kuweka akiba

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
Habar wana JF?

Msingi mkubwa wakufanikiwa katika maisha nikuweka akiba.

Kipindi nipo Shule nilikua na-save kiasi cha pesa ninacho pewa kwaajili ya matumizi ya shule kila siku nyumbani nilikua napewa TZS 2,000 kama matumizi ya kutwa nzima nikiwa shuleni kwani kutoka home hadi shule kulikua na umbali mrefu.

Toka hapo hadi leo bado nimeendelea kujiwekea akiba na nimeona ni njia salama sana kwani inakupa uhuru wa pesa.

Katika harakati za kueka akiba kila mtu huweka kulingana na kipato chake.

70cf8bfae9d105d762151afe6cf9965f.jpg


Nimeanzisha uzi huu ili kila mtu kushare Idea yake anayotumia kueka akiba- kwani akiba ndio njia salama ya kufikia malengo - na pia kuwakumbusha wale wasiokua na utaratibu wa kujiwekea akiba

Kama unandoto ya kumiliki gari,nyuma nzuri,nk anza leo kueka kidogo unacho kipata ndicho kinacho tengeneza kikubwa cha kesho

NB: sio lazima usave kwenye kibubu unaweza weka kwenye TIGO PESA , M PESA Bank Account Nk..

SHARE IDEA YAKO UNAYO TUMIA KUWEKA AKIBA [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Kibubu. I appreciate this petty box
Mkuu kibubu sitakaa nirudie! Kulikuwa na kibubu kinatolewa na NMB miaka ya nyuma. Kila siku nikawa naweka hela yoyote inayobaki kwenye matumizi ya siku na nikafanya kwa uaminifu kwa muda wa mwaka mzima. Siku moja nikakihamisha halafu nikasahau nilipokiweka, wee nusura nizimie! Sasa hivi jukumu hilo nimemwachia mama watoto amefungua akaunti ya malengo. Huko kila siku anapeleka elfu 30 kutoka kwenye Biashara! Hii ni njia salama kabisa!
 
Mimi na trace matumizi yangu na ninachoingiza kwa kutumia app ya monefy ambayo ipo playstore. Hii app inakufanya ujue kiasi ulichotumia kwenye chakula, malazi, gari, starehe n.k kila baada ya mwezi.

Kisha natunza bank kwenye akaunti ya saving kile kiasi nilichopanga. Hii ni hatua ya pili ya kusevu.

Mwisho Nasevu hicho kiasi kwenye kununua kiwanja, kufanya ujenzi wa jengo, kununua shamba, kupanda miti kwenye shamba n.k

Halafu ole wake mtu aje na sera zake za kimasikini miaka 3 ijayo ntakapokuwa naenda likizo ulaya na familia yangu.
 
Mkuu kibubu sitakaa nirudie! Kulikuwa na kibubu kinatilewa na NMB miaka ya nyuma. Kila siku nikawa naweka hela yoyote inayobaki kwenye matumizi ya siku na nikafanya kwa uaminifu kwa muda wa mwaka mzima. Siku moja nikakihamisha halafu nikasahau nilipokiweka, wee nusura nizimie! Sasa hivi jukumu hilo nimemwachia mama watoto amefungua ajaunti ya malengo. Huko kila siku anapeleka elfu 30 kutoka kwenye Biashara! Hii ni njia salama kabisa!
Hongera mkuu kwa uthubutu huo wa kuweka elf 30 per day si kitu kidogo katika hali hii ya vyuma kukaza

(30,000 x 365= 10,950,000 x 5 = 54,750,000)

Je unakumbana na changamoto zipi?
 
Mimi napata 250,000 kwa mwezi. Mwanzoni nilikuwa natumia kwanza afu ikibak ndo nasave unakuta mda mwngne hamna hela ya maana uliyosave. Nikabadilisha njia. Nikawa nikipata tu hela naweka 100,000 kamili bank alaf hyo 150 inayobak ndo nafanya matumizi. Namshukuru MUNGU na kipato changu kidg nimekaa mwaka na zaidi sasa nina akiba ya 1.2m
Hyo ndo njia ninayoitumia na sitoiacha. Naombea niongeze kipato ili kuongeza akiba yangu.
 
Back
Top Bottom