Share Nasi Hapa Cheat Code Ya Mazoezi Yoyote

Share Nasi Hapa Cheat Code Ya Mazoezi Yoyote

mtoa mada mi nimeanza juzi kukimbia kuzuka uwanja bt mapaja yote yanauma hatari VIP hii hali unaweza isha baada ya siku ngapi
 
mtoa mada mi nimeanza juzi kukimbia kuzuka uwanja bt mapaja yote yanauma hatari VIP hii hali unaweza isha baada ya siku ngapi
Yanauma yamechubuka au kama yameviza?

Kama ni kuviza, usiache endelea ila shuka spidi uliyotumia nyuma yake. Ndani ya siku nne unakua uko sawa.
 
mtoa mada mi nimeanza juzi kukimbia kuzuka uwanja bt mapaja yote yanauma hatari VIP hii hali unaweza isha baada ya siku ngapi
usiache kwa ajili ni kitu ambacho ulikuwa ukifanyi hivyo misuli inakuwa inapokea kitu kipya baada ya siku kama 5 na itakuwa ni kawaida
 
Ukimaliza kufanya zoezi la mkono yaani biceps au triceps, fanya shadow boxing kama kuna punching bag lipige hata ngumi kumi tu
 
Kitu poa kabisa baada ya kuanza mazoezi ni kupata matokeo ya zoezi lako, poa zaidi ni matokeo hayo yanapokuja kwa haraka.

Siyo kila mtu ana muda wa kufanya zoezi la masaa matatu, hell wengine hata saa moja kwao ni kupoteza muda.

Now uzi huu uwe special kwa ajili ya kugeana mbinu za kufikia malengo haraka, mbinu zitakazotolewa hapa ni za mazoezi yoyote.

Ni vizuri mbinu itakayotolewa iwe ambayo mtu ulishawahi kuitumia au kuiona mtu akiitumia ili likija swali unalijibu kwa uhakika.

Naanza na hizi.

1. Ukiwa unajivuta mikono usiitanue sana iwe na umbali wa usawa wa mabega yako.
Utatengeneza biceps, nguvu za mikono, mabega na 'mabawa' yatakuja kama kawaida.

2. Raundi zako ziwe 10 na seti 3 za mazoezi katika kila zoezi lako.

3. Kama unafanya zoezi la kifua anza na push ups, piga push ups za tambarare na miguu ikiwa juu ya kitu kisha nenda anza na incline bench press.

4. Ukiwa unakimbia usiteme mate na hema kwa kutumia pua, mdomo usiwe wazi. Utafikia levo ya juu kabisa ya kukimbia kwako pia utazuia kichomi.

5. Tafuta mwenza wa mazoezi.

6. Changanya juisi na peanut butter na itumie muda wote utakaokua ukifanya zoezi lako.

Zingine endeleeni wadau na mimi nitaendelea kutoa mbinu.
Mkuu asante kwa Mada nzur naomba msaada mazoez ya Tumbo
 
Fanya biceps curl kwa kutumia bar nene itakayozuia viganja vyako kuifumbata bar yote.
Hapa utatumia maximum effort ambayo itakupa matokeo faster ya unachofanya.

Usisahau kufanya shadowboxing au kulipiga ngumi punching bag.
 
Safi sana hii inatufaa wana mazoezi
ningependa kujua pia namna rahisi ya kuongeza protein ili niweze kugain more muscles na weight kwa yeyote anayejua atufahamishe

kuna kitu kinaitwa protein powder anayejua hii kitu atoe details
 
Protein powder ni supplement katika gym advanced unaweza ukakuta wanaziuza, kwa sisi Tanzania maarufu ni whey protein na protein shake.
Kwa kua mlo wako unaweza usifikie kiwango cha protein inayotakiwa hizi supplement kazi yake ni kuziba hayo mapengo.

Nimeshaona vidonge vyake na pipi pia.

Kiukweli namna rahisi ni kutumia hiz supplements, ila kama mfuko unaruhusu ni kupangilia mlo wako kwa vyakula vyote vyenye protini. Kama mfuko hauruhusu basi usikose peanut butter, maziwa, ndizi, samaki, mayai na juisi za matunda.
 
Safi sana hii inatufaa wana mazoezi
ningependa kujua pia namna rahisi ya kuongeza protein ili niweze kugain more muscles na weight kwa yeyote anayejua atufahamishe

kuna kitu kinaitwa protein powder anayejua hii kitu atoe details
Ila ukiamua kutumia supplements inabidi uwe serious na mazoezi na uende to the extreme.
Hii ni kwakua utakua una protein nyingi mwilini ambayo haina kazi na badala yake itasababisha tumbo kua kubwa na kuonekana mnene.
 
going to the extreme is not a problem asante kwa majibu yaliyojitosheleza mkuu
 
Ukiwa unataka kupiga flat bench.
Chukua uzito utakaoweza kupiga reps 30 bila kupumzika.

Piga reps 15 kwa kuanzia juu mpaka chini.
Kisha 15 zinazofuatia piga kwa kuanzia chini na kuishia kati.

Fanya hivyo kwenye zoezi la squats, mikono na mabega.
 
Back
Top Bottom