Share za ACACIA zazidi kuporomoka baada ya TRA kupeleka Tax Invoice

Ombeni madai yenu yawe ya kweli vinginevyo tutawafidia hiyo hasara.

Cha ajabu hata ripoti hamtaki kuwapa sasa sijui tutaaminika vipi..

Ndo maombi ya wanaCHADEMA siku hizi.
Wanatamani nchi ishindwe katika vita ya kutetea maliasili zetu.
Kweli LOWASA kaleta MABADILIKO ndani ya CHADEMA.
Tundu Lissu anawapigia magoti wazungu wasilete misaada kwa watanzania mpaka RAIS amruhusu kutukana na kuwagawa waTanzania kwa misingi ya Ukanda, Udini na UKABILA.
Hii ndiyo CHADEMA ya siku hizi.
Imekuwa ya HOVYO HAIJAPATA KUTOKEA!
 
You are right, there is a way craizyness is taking over in this country at a very high speed!
Noble people aren't noble anymore
 

Hivi ndo vitu watu hawataki soma wala sikia. lakin ndo ukweli. Acacia hawajaibia serikali. Serikali inajichanganya tu.
 
Makusanyo ya TRA kwa mwaka ulioisha kutoka VYANZO VYAKE VYOTE ni less than USD 7 bn/-. Leo wanaidai ACACIA 190/- about USD 19 b/- kwa mwaka. Hivi inaingia akilini mapato ya kampuni moja ni karibu mara tatu ya makusanyo yote ya kodi ndani nya nchi ile ile? Hebu tuacheni mizaha wajameni.
 
ushaambiwa from 2000-2017 plus penalties na malimbikizo yote kwanza kwa mtazamo wangu hzo ndogo sana wamewahurumia hao wezi
 
Hivi tutakuja kupata mwekezaji wa level ya Barrick tena kweli

Sijawahi kumsaport Dikitekta uchwara ila hawa Majizi Barrick nilianza kuwachukia tangu ile report ya mwaka 2001 ya mazingira na kuona watanzania wenzetu wanavyokufa kwa maji ya sumu.

Hawa sio wawekezaji, Barrick ni Majambazi yanayosaidiwa na CCM kuibia Tanzania rasilimali. Uwekezaji wa Baricck haunufaishi Mtanzania wa hali ya chini wala nchi. Watanzania wanaokaa karibu na huu mgodi hawanufaiki na huo mgodi. Bora ufungwe au wapewe Watanzania wenyewe wachimbe
 
Hivi ndo vitu watu hawataki soma wala sikia. lakin ndo ukweli. Acacia hawajaibia serikali. Serikali inajichanganya tu.
Mkuu ni vizuri kuuliza hiyo amount tunayowadai imepatikana kwa calculations zilizobase kwenye nini? Halafu wenye akili tuanze kuichallenge formular waliyoitumia kama siyo sahihi.
Ni ujinga kuamini data za wazungu pasipo kujua data zetu zinasemaje na kwa ushahidi gani.
 

Barick sio mwekezaji, barick ni mwizi na sio mlipa kodi. Tutayachimba wenyewe aondoke zake. Lazima uchumi wa nchi ushikiliwe na Watanzania wenyewe sio wageni. Wapo wawekezaji wa ukweli lakini sio Barick
 
Hivi ndo vitu watu hawataki soma wala sikia. lakin ndo ukweli. Acacia hawajaibia serikali. Serikali inajichanganya tu.
Mkuu ni suala la muda tu ila soon kuna mtu anaenda umbuka hapa! na ndo hapo hata usomi wake utakapodharaulika na pamoja na sifa nyiiiingi alizopewa atashaangaa upepo ushageukaa
 
Mkuu data nyingi za wazungu ziko wazi ukizitafuta utapata sasa hapa kwetu ripoti tumeambiwa ni ya rais!! hata anayetuhumiwa hajapewa huu si ujinga wa kiwango cha lami aka uzazwa!
 
We jamaa unadhani mgodi ni kama duka la mhindi! sio kwamba TRA ni wapuuzi au hawana akili, wanafanya kumridhisha mtu. Facts zinajulikana. kama umewahi fanya uhasibu kwenye kampuni popote pale tanzania utajua tu hili swala la acacia tumeingia chaka big time
 
Barick sio mwekezaji, barick ni mwizi na sio mlipa kodi. Tutayachimba wenyewe aondoke zake. Lazima uchumi wa nchi ushikiliwe na Watanzania wenyewe sio wageni. Wapo wawekezaji wa ukweli lakini sio Barick
Hao wawekezaji wa ukweli mbona hawakupewa hiyo migodi? Tumeshindwa hata viwanda vya toothpick tutaweza kuchimba madini na kuyauza wenyewe? kama uwezo upo why Magu alazimishe kwamba Barick watajenga smelter? si serikali ijenge
 
Mkuu tatizo kuna watu wana mahaba niue kwa mkulu na wameshikiwa akili zao na mtu mmoja!!!! ila tukumbuke aliyepita alisema za kuambiwa tuchanganye na za kwetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…