Sharks Vs Mombasa United: Penalty Yalipua Mechi, Refa Aokolewa

Sharks Vs Mombasa United: Penalty Yalipua Mechi, Refa Aokolewa

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
Mpango wa kupata timu itakayocheza FKF Premier League msimu wa 2026/27 umeishia kwenye vurugu baada ya mechi ya marudiano kati ya Kariobangi Sharks na Mombasa United kusitishwa katika Uwanja wa Ulinzi Sports Complex.

Sharks walikuwa mbele 2 - 1, matokeo yaliyofanya jumla ya mechi mbili kuwa 3 - 3, baada ya Mombasa United kushinda mechi ya raundi ya kwanza 2 - 1 Jijini Mombasa.

Lakini mambo yalibadilika kipindi cha pili. Refa John Sulwe aliwapa penati Mombasa United baada ya kudaiwa kutokea kwa kuvutwa kwa jezi ya mchezaji ndani ya boksi kufuatia corner. Uamuzi huo ulipingwa vikali na wachezaji wa Sharks na baadae baadhi ya mashabiki wakaingia uwanjani.

Hali ilizidi kuwa mbaya kiasi kwamba refa alilazimika kukimbia kuelekea kwa walinzi, huku taarifa zikisema alishambuliwa kabla ya kusindikizwa mahali salama.

Penalty yenyewe haikupigwa na Mechi ilisitishwa.

LAKINI HII SI PENALTY TU.
Kilichotokea Ulinzi Sports Complex kinakuja baada ya wiki kadhaa za mvutano kuhusu playoff hii. Kariobangi Sharks na Mombasa United walikuwa wamekwama kwenye mgogoro kuhusu kanuni za kupandishwa na kushushwa daraja, suala ambalo hata liliingia Mahakamani na kuchangia kuchelewa kwa kuanza kwa msimu mpya. FKF baadaye ilisaidia timu hizo kukubaliana kumaliza suala hilo kupitia playoff ya mechi mbili.

Kwa hiyo, mechi ambayo ilipaswa kumaliza mgogoro uwanjani nayo imeishia kusitishwa, na sasa FKF ina kazi nyingine ya kuamua hatima ya mechi hii na timu gani itapata nafasi hiyo ya Premier League. FKF bado haijatoa uamuzi wa mwisho, huku suala likitarajiwa kufikishwa kwenye kamati husika kwa kuangalia ripoti za refa, match commissioner, usalama na maafisa wengine waliokuwepo.

Tukio hili linaibua swali pana zaidi kuhusu uaminifu katika officiating, uteuzi wa waamuzi, usalama viwanjani na namna FKF inavyoshughulikia migogoro ya mashindano.

Kwa mfano, kabla ya mechi, baadhi ya wadau walikuwa tayari wameuliza maswali kuhusu uteuzi wa Sulwe kama refa pamoja na msaidizi wake refa Jane Cherono. Hayo yalikuwa maswali ya wadau, si ushahidi kwamba matokeo yalipangwa.

Sasa, baada ya mechi kuishia hivi, FKF haiwezi tu kutafuta nani atapanda Premier League. Inabidi pia iulize kwa nini mechi muhimu kiasi hiki haikuweza kufika dakika 90. Kwa sababu kama playoff yenyewe iliundwa ili kumaliza mgogoro wa muda mrefu, lakini ikaishia kwenye pitch invasion, vurugu na refa kuondolewa kwa usalama, basi tatizo la soka letu ni kubwa kuliko penalty moja.

Je unadhani hii ni hasira za mchezo wa presha tu au ni ishara kwamba Kenya bado ina tatizo kubwa la uaminifu kwenye officiating, usimamizi wa mashindano na nidhamu ya viwanjani?
 
Back
Top Bottom