TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

amepata ajali ya gari huko mkoani tanga Muheza usiku huu source eatv breaking news RIP Sharo milionea
 
Bado moyo umegoma kukubali.... Mpaka sasa hakuna habari toka chanzo cha uhakika
 
Msanii wa filamu za vichekesho sharomilionea amefariki kwa ajali mkoani tanga eneo la muheza

Sina uhakika sana na taarifa yako sijaona kituo chochote cha TV kilichotoa Breaking News juu ya hilo hususani EATV, tunaomba kupata chanzo cha hiyo taarifa yako.
 
Polisi Tanga wamethibitisha kuwa sharo milionea kafariki.

Mpoki amepigiwa simu na rafiki ake polisi kuwa jamaa kafariki -twitter

Tundaman amesema alipigiwa kutumia simu ya sharo na jamaa wa hospital akaeleza
 
Nae tunaweza mzika kama Kanumba kamati ya mazishi msinisahau R. I. P Sharo
 
Kina Steve nyerere na Ruge naskia washaanza kupigiana simu kuunda kamati ya mazishi..soon watatoa namba za mpesa na tigopesa...rip shalo
 
jaman tanzania imeondokewa na wasanii wawili muhimu sana MUNGU MLAZE MAHALI PEMA AMINI
 
Dah! Kifo kipo karibu sana..kama mshumaa kwenye upepo..tunajisahau sana,tuko busy na dunia na kusahau kama mwisho wa siku tunarudi kwenye udongo! Iko haja ya kujifunza mapema kumpa Mungu cheo ili kesho atupokee vizuri! Kama ndivyo R.I.P SHARO..
 
Sina uhakika sana na taarifa yako sijaona kituo chochote cha TV kilichotoa Breaking News juu ya hilo hususani EATV, tunaomba kupata chanzo cha hiyo taarifa yako.

Wabongo kwa utomaso ndo maana mnabaki masikini licha ya kukalia utajiri.
 
Very sad!
Roho ya marehemu ipumzike kwa amani.
 
Back
Top Bottom