Pumzika Kwa amani Sharo
Leo nimesikiliza radio tokea asubuhi mpaka sasa hivi, channels tofauti tofauti
katika kusikiliza huko radio huku tukiomboleza kifo cha Sharo milllionea nimegundua lifuatalo,
nyimbo za maombolezo ni chache sana (ni jambo jema sababu hatuombei maafa), so kwa sababu hiyo radio katika kuonesha kuomboleza kwao zimekuwa zikicheza rekodi za mafunzo na zile chache za maombolezo zilizotungwa wakati maafa yalipotokea
Sasa nachowaza na kunifanya niandike headingi hiyo hapo juu ni hili,
Nyimbo zote za mafunzo zilizochezwa leo (au asilimia kubwa zaidi ya 90) ni za kuanzia miaka ya 2005 na kurudi nyuma, meaning ya kwamba sanaa za leo hazifundishi lolote juu ya madhara ya ukimwi, dawa za kulevya au anasa ilopitiliza, Zaidi na zaidi wao wanasemea starehe na kuzidi kusifia ngono
kwa mwendo huu nachelea kusema sanaa ya Tanzania inaelekea kuisha au kupotea kabisa, msanii kwenye radio release zako ambazo zinatangaza album sio mbaya kuweka nyimbo ya kufunza
mfano wa hizo nyimbo ni
Swahiba - Jebi , afande Sele
Alikufa kwa ngom - Mwana FA
Shida - Remmy
Faraja - Lady Jaydee etc
Rest In Peace Sharo Millionea