Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona Haieleweki Hii au Ni Cooked? Mbona inaonyesha Sharo Alituma 10:47 PM Mon wakati ajali amepata 08:00 PM Mon?
![]()
Pumzika Kwa amani Sharo
Leo nimesikiliza radio tokea asubuhi mpaka sasa hivi, channels tofauti tofauti
katika kusikiliza huko radio huku tukiomboleza kifo cha Sharo milllionea nimegundua lifuatalo,
nyimbo za maombolezo ni chache sana (ni jambo jema sababu hatuombei maafa), so kwa sababu hiyo radio katika kuonesha kuomboleza kwao zimekuwa zikicheza rekodi za mafunzo na zile chache za maombolezo zilizotungwa wakati maafa yalipotokea
Sasa nachowaza na kunifanya niandike headingi hiyo hapo juu ni hili,
Nyimbo zote za mafunzo zilizochezwa leo (au asilimia kubwa zaidi ya 90) ni za kuanzia miaka ya 2005 na kurudi nyuma, meaning ya kwamba sanaa za leo hazifundishi lolote juu ya madhara ya ukimwi, dawa za kulevya au anasa ilopitiliza, Zaidi na zaidi wao wanasemea starehe na kuzidi kusifia ngono
kwa mwendo huu nachelea kusema sanaa ya Tanzania inaelekea kuisha au kupotea kabisa, msanii kwenye radio release zako ambazo zinatangaza album sio mbaya kuweka nyimbo ya kufunza
mfano wa hizo nyimbo ni
Swahiba - Jebi , afande Sele
Alikufa kwa ngom - Mwana FA
Shida - Remmy
Faraja - Lady Jaydee etc
Rest In Peace Sharo Millionea
mimi kila nikienda kulala huwa ninamshukuru mungu kwa kunilinda siku yote na kumuomba anilinde tena usiku na nikiamka ahsubuhi namshukuru kwa kunilinda usiku wote na kuomba tena anilinde siku yote...watu wengi hatufahamu ni bahati gani tunayopata kila siku tunapoamka tukiwa hai tunapumua...na tena mambo yanapokuwa yanakwenda vizuri ndiyo tunazidi kujisau.
Kijana ndiyo alikuwa anaelekea kwenye pinnacle ya mafanikio yake lakini kama remmy ongala alivyosema "kifo hakina huruma"
rip.
Bado wewe mwenyewe..!!Wote sisi ni marehemu watarajiwa.kwahyo usijione una muda mwing wa kuishi.Ni kuombeana kheri tu katika maisha.
There are currently 742 users browsing this thread. (73 members and 669 guests)
Hoya Nyie Guests Mnatuyeyusha Jiungeni Bwana!!!!!
Diamond anakuhusu?
Nawewe koma.
Unataka kusema kafa kwa sababu ni Sharobaro?Hatimaye usharobaro wake umeishia kumponza.
Kuendesha Opa mitaa ya Kinondoni siyo challenging and risky kama cross-country trip.
Hamna vimwana wa ku-impress na usharobaro on the highway to Muheza.
Its one-on-one between you and the machine.
diamond ni public figure!
Dah kwanini Bongo mtu akianza pata umaarufu na mafanikiotu anaondoka,Check Kanumba,Mr Ebo,Sharo,Vivian Tillya,na wengine kaibao au ndiyo uliusemi IKIVUMA SANA INAKARIBIA KUPASUKA.
R.I.P ALL.
Wame mwacha Mungu na kukimbilia uovu Mkuu. Aishie ktk uovu hadumu, maana imeandikwa mshahara wa dhambi ni mauti kuishi ni neema atupayo Mungu. Just imagine pumzi ni yake halafu uwe kinyume naye hakika utaishi maisha mafupi na ni kwa neema sana. Ni hatari sana kuishi ukitegemea akili zako mwenyewe. Mungu anatupenda lakini ukimsogelea naye anasogea, ukimwacha naye anakuacha. Matokeo yake ndio haya magonjwa na vifo vya mapema.
Tumrudie Mungu meen. Maana imeandikwa katika mithali "wamchao Bwana wataongezewa siku za kuishi". Vifo vya mapema ni mauaji na sio kwamba Mungu amemwita, bali ameuawa. Mungu hatwai kwa style hiyo na wala sio katili, hahitaji kufanya ajali au ugonjwa ili achukue Roho ya mtu. Huyo ni shetani. Shetani anapata kibali kuondoa Roho ya mtu pale mtu yule anapokuwa kinyume na Mungu. Na anaomba kwa Mungu sawa sawa na Neno lake mwenyewe, kulingana na sheria ya Mungu isemayo mshahara wa dhambi ni mauti, Mungu haendi kinyume na sheria yake mwenyewe ana-approve and one dies. Mtetezi wetu ni Bwana Yesu aliye kufa kwaajili yetu huyu ndiye husema No (seeing the future) na sisi tunapata neema ya kuishi tena katika mazingira ambavyo vinginevyo tulikuwa tufe.
Si kusudi la Mungu mtu afe mapema na wala Mungu hafurahii vifo vya mapema. Ni furaha ya Mungu sisi tunapoishi maisha marefu na kutimiza kusudi alilotuumba kwalo. Mungu ametupa kuchagua uzima na mauti baraka na laana, hivyo kufa ni choice ya mtu bila kujijua, unapoishi dhambini umejichagulia mauti. Ikukumbukwe kwamba kila mtu ana kazi ambayo alikuja duniani kuifanya (divine assignment). Ndio maana kwenye ile sala ya Bwana tunasema ....utakalo lifanyike Duniani kama Mbinguni.... ina maana tunapaswa kufanya kama vile Mbinguni walivyo amua. Hivyo napinga kwamba sio Bwana ametwaa, No.
Mrudie Muumba wako na utubu upate kuishi kwa amani. Yesu alikuja ili tuwe na uzima tena tuwe nao tele.Duniani tunapita kuna mahali tunaenda ambako tutakaa sana. Maisha hapa duniani ni kwa kitambo tu, lakini upo umilele mbele yetu we have to go for. It is my prayers that we all don't die before fulfilling what God intended us to do here and become.... in Jesus name I submit. Amen