TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

tu appreciate wasanii wetu na kazi zao, c mpaka wafariki(at least nimejifunza hilo). So sad poleni wafiwa
 
Wote tunafahamu ni ajali ya gari. Swali langu je ni alikuwa peke yake, alikuwa amelewa , speed kali, au ubovu wa barabara, ubovu wa gari , au hakuwa na uzoefu na driving. Sina maana mbaya maana kila inapotokea msiba pamoja na majonzi pia watu wanajifunza......R.I.P .
 
Muulizaji hakuwa na nia mbaya kuuliza chanzo cha kifo cha Sharobaro, linapotokea tukio kama hili kwetu pia ni fundisho kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamja na kujiandaa kiroho na ndio maana viongozi wetu kiroho hutoa wosia kwetu sisi tuliobaki. Vile vile ikiwa tutajua chanzo cha kifo ni rahisi kwetu tuliobaki kuchukua tahadhari, kwa mfano tukiambiwa chanzo ni kupasuka kwa tairi itakuwa ni vyema kujiuliza pengine marehemu alikuwa amenunua matairi yaliyotumika au kukataliwa huko ulaya ambayo kwa kweli yamekuwa yakisababisha ajali nyingi za barabarani.
 
Wote tunafahamu ni ajali ya gari. Swali langu je ni alikuwa peke yake, alikuwa amelewa , speed kali, au ubovu wa barabara, ubovu wa gari , au hakuwa na uzoefu na driving. Sina maana mbaya maana kila inapotokea msiba pamoja na majonzi pia watu wanajifunza......R.I.P .

Kutokana na mahojiano na binti ambaye alikuwa analia jana Star TV, alisema ndio alikuwa amenunua gari anamwita kuwa njoo uendeshe gari nimenunua gari, inawezekana kabisa alikuwa dereva mwanafunzi. (pamoja nakuwa unaweza kuwa hun a gari lakini unajua kuendesha). RIP
 
kwa hiyo ni ulimbukeni wa gari...mana kwanini mtu anunue gari kama kuendesha na leseni hana?
 
mtahoji saaaaaana lakini mwisho wa yote jibu ni kwamba sharo amefariki katika ajali ya gari,
 
kwa hiyo ni ulimbukeni wa gari...mana kwanini mtu anunue gari kama kuendesha na leseni hana?

Unajua na utoto! Ujana! ubishoo! etc. Tena kama ni automatic, which is very much likely to be so, hauhitaji kuwa dereva!????? Nawaona akina mama/baba wanaendesha leo leo hii toka dukani. Lakini na yote RIP.
 
Kwa nchi zilizo endelea pamoja na kuwa alikuwa pekee yake kilicho sababisha ajali kingejulikana sema tu kwa Tanzania ajali sio issue labda angekuwa mtalii kutoha Uholanzi.
 
Yaani binadamu mwenzako kapoteza uhai,unamvua kila kitu alichovaa! je ni ubinadamu huo? yaani nina hasira sana! nisaidieni! Inasemekana alipopata ajali alikuwa na pesa za mtaji kwa ajili ya kumpelekea mamake, na hapo hapo kumdhalilisha kwa kumvua nguo kwa kumuacha na boxer na singlet tu! Utu wa mwanadamu umepotea kabisa? Inasikitisha!
 
Back
Top Bottom