TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

Yaani binadamu mwenzako kapoteza uhai,unamvua kila kitu alichovaa! je ni ubinadamu huo? yaani nina hasira sana! nisaidieni! Inasemekana alipopata ajali alikuwa na pesa za mtaji kwa ajili ya kumpelekea mamake, na hapo hapo kumdhalilisha kwa kumvua nguo kwa kumuacha na boxer na singlet tu! Utu wa mwanadamu umepotea kabisa? Inasikitisha!
Sipati picha kama angekua hajavaa boxer wangemuachaje. Hawa wezi hawa kiboko. R.I.P Sharo.
 
Mie nadhani ilikuwa mwendo kasi .Gari ilikosa Control

Ukizicheki picha za gari zinajieleza zenyewe
RIP sharo milionea
 
mwendo kasi, hakufunga mkanda, hakuwa dereva mzoefu..........haya yanajieleza kwa kuangalia picha zake
 
Kusinzia, Uchovu, Usiku kutokuona vizuri, vyote vyaweza kua sababu pia
 
OGOPA KUTUMIA TAIRI SILIZOKUJA NA GARI TOKA HUKO ILIKOKUWA INATUMIKA KWA SAFARI NDEFU,UKINUNUA GARI HATA KAMA TAIRI ZINAVUTIA NA KUONEKANA NI MPYA NI BUSARA YA KAWAIDA KWA MTU ANAYEJARI MAISHA YAKE KUBADILISHA TAIRI KAMA ANATAKA KUSAFIRI SAFARI NDEFU ITAYOMFANYA AENDESHE KWA SPIDI KUBWA MUDA MREFU-Tuutunze,tuuheshimu na tuupende uhai,opgopa kutumia tairi ambazo hujui zilifungwa lini na zimekaa muda mrefu kiasi gani bila kutembea zikisubiri wewe uzinunue pamoja na gari,hii itasaidia sana kupunguza ajali na vifo vitokanavyo na ajali, JINGINE, safari ndefu zinahitaji uzoefu katika kuendesha, safari ndefu kwangu ni zaidi ya km 70,huwezi kujifunza gari hata kama ni automatic then ujipinde kuendesha safari ndefu, unjitengenezea mazingira mazuri ya ajali,sio vibaya kuomba msaada au kukodi dereva mwenye uzoefu,si kwamba yeye anakinga ya ajali lakini baadhi ya visababishi vya ajali ataviepuka kwa kuwa anao uzoefu...
 
Nadhani hata kama alikua ametekwa, kwa aina ya mzinga uliotokea, zingekutwa maiti mbili pale. Au labda awe alimpa lift Jini Mahaba.
 
Naomb KujuZwa steve Nyerere ni nani katika maswal ya Misiba ya wasanii hapa
TZ....Kwani Kila unapotokea Msiba Yeye Ndiye anathibitisha....!!!!!???

Hahahahaha sina mbavu daaaa watu hawampendi kaisa huyu jamaaa, alikula shavu lla nguvu kwenye msiba wa STEVEN KANUMBA hahaha ni mtu wangu wakaribu ndio maana
 
Hii noma ingawa ndo njia ya wote lakini inauma yaani ndo kaanza tu kuzivuna kutokana na mawindo ya mda mrefu bila kutoka kuigiza kama teja na kamata mwizi men mpaka kutoa tracs/music lakini anatutoka ghafla kama utani. Ni kweli vyema huwa havidumu bali vyenye matatizo hudumu ingawa sijui ni kwa nini e.g; mafisadi, wauaji, wachawi n.k. Mpaka kesho sijui jibu labda tusaidiane kwa hili.

kaka hao mafiisadi wanapita hapo na mav8
 
331577ce78bb35164cdf7229af1653ad.jpg
 
Back
Top Bottom