Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakuu!
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, leo tena anapanda kizimbani, Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, kwa ajili ya shauri lake la maombi ya jinai alilolifungua mahakamani hapo.
Lissu anakabiliwa na kesi ya kuchapisha taarifa za uwongo katika mtandao wa YouTube, kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao namba 14 ya mwaka 2015.
Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini imeshaanza kusikilizwa ushahidi wa upande wa mashtaka ambapo tayari shahidi mmoja ameshatoa ushahidi wake.
Kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa ushahidi, upande wa mashtaka ulifungua maombi mahakamani hapo (Kisutu) ukiomba mahakama hiyo iamuru baadhi ya mashahidi wake kutokuwekwa wazi wakati wakitoa ushahidi kwenye kesi hiyo wala taarifa za utambulisho wake kuwekwa wazi.
Lissu kupitia mawakili wake wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo ya Jamhuri waliyapinga pamoja na mambo mengine wakidai kuwa upande wa mashtaka haukutoa sababu za msingi za kuomba mashahidi wake wasiwekwe wazi.
Kwa updates zote kuhusu Kesi hii nitaziweka hapa.
Tundu Lissu amefika kwenye Ukumbi wa Mahakama
Mkurugenzi wa Habari wa CHADEMA Taifa, Brenda Rupia hii leo amefika katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam tayari kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wao wa Taifa, Tundu Lissu.
Itakumbukwa Brenda alizuiwa na mamlaka ya Uhamiaji siku ya Jumamosi ya Julai 12, 2025 alipokuwa mpakani jijini Arusha kuelekea nchini Kenya na kukamatwa na Jeshi la Polisi, aliachiwa siku ya jana Julai 15, 2025 kwa mujibu wa taarifa ya CHADEMA iliyotolewa hapo jana, Julai 16,2025.
Mwenendo wa kesi ya Tundu Lissu
Shauri la kupinga mashahidi kuficha sura kwenye kesi ya uchochezi linaendelea mbele ya Jaji Mkwizu katika Mahakama Kuu ya Dar es Salaam. Waombaji wakiongozwa na Wakili Mpoki wakisaidiana na Alute Mugwai, Mtobesya na wengine; upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Nasoro Katuga, Job Mrema, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasawa.
Mahakama imeamua kusikiliza shauri baada ya pande zote kueleza wako tayari. Mpoki ameomba Dr. Nshala aongezwe kwenye coram, na kueleza changamoto za mawasiliano kati ya Lissu na mawakili wake.
Tundu Lissu ameeleza kuwa tangu Ijumaa alizuiwa kuwasiliana na mawakili wake, akiwekwa lockup hadi saa sita bila kuruhusiwa mashauriano. Amelalamikia askari magereza kuvaa mavazi ya kijeshi na kuingilia mawasiliano ya kisheria, akisisitiza kuwa Mahakama ni ya kiraia, na mawasiliano ya mteja na wakili ni haki ya msingi isiyovunjika.
Ametaja sheria ya magereza ya mwaka 1987 na azimio la Umoja wa Mataifa la 1988 kuhusu haki ya mawasiliano ya mfungwa na wakili, akisema kinachoendelea ni dharau kwa mahakama na ukiukaji wa haki ya kusikilizwa kwa haki. Lissu amemtaka Jaji atamke kama haki hiyo ipo au la!.
Tundu Lissu alitofautiana na Askari Magereza mahakamani baada ya kuzuiwa kushikana mikono na Mawakili wake na kupeana nao nyaraka, akidai mahakama isiwe ya kijeshi.
Jaji aliwauliza Mawakili wa Serikali, ambapo Nasoro Katuga alijibu kuwa Jeshi la Magereza lina mamlaka ya kuwahifadhi wafungwa na wasiofungwa kwa mujibu wa Prisons Act Cap. 58/2023, akisisitiza kuwa hata utoaji wa vitu kama chakula unahitaji idhini ya Kamishna kwa sababu za kiulinzi.
Lissu alijibu kuwa suala si chakula bali ni haki ya mawasiliano ya mteja na wakili wake (advocate-client relationship), akisema vifungu vilivyotajwa havihusiani na hoja hiyo.
Jaji alisema uamuzi wa suala hilo utatolewa mwishoni, kisha usikilizwaji wa maombi ya msingi ukaendelea. Mpoki Mpale alieleza kuwa maombi hayo yamewasilishwa kwa mujibu wa vifungu vya 372 na 392 vya Criminal Procedure Act, yakitiwa nguvu na kiapo cha tarehe 25/06/2025 chenye sababu 4, zitakazoelezwa na mawakili Alute, Nshala, Mtobesya na Kambole.
Alute Mugwai alianza kwa kueleza kuwa Hakimu wa Kisutu alitumia judicial discretion kuamua ombi la kuficha mashahidi wa Jamhuri, lakini kesi ya Musimba Masai Masamba (2019) inaeleza kuwa judicial discretion lazima izingatie misingi ya haki na sheria.
Dr. Ruge Nshala.
Kiapo cha maandishi ni mbadala wa ushahidi utakaotolewa mahakamani. Na kiapo lazima kikidhi matakwa ya sheria. Na sheria kwa sasa ni Order XIX ya Civil Procedure Code, inayoeleza kuwa muapaji anayetegemea maelezo ya mtu mwingine lazima amtaje mtu huyo na mtu huyo naye aape ili kiapo kiwe na uzito, vinginevyo kinabaki kuwa maneno ya kusikia barabarani.
Hayo yameelezwa na Mahakama ya Rufaa katika kesi nyingi, ikiwemo Sabena Techniques na Lwitiko Mamaso. Hizi kesi zote zimeweka msingi wa jambo hili.
Mheshimiwa Jaji, kama ambavyo maombi yanavyojieleza, ukiuangalia uamuzi wa Mheshimiwa Mhini pale Kisutu, unasema sababu za kuficha mashahidi ambao si Polisi ni kwamba wako kwenye tishio la usalama kutokana na hofu ya mashabiki wa mleta maombi, yaani Tundu Lissu.
Kiapo cha Thawabu Issa, Wakili wa Serikali, kinasema mashahidi wako kwenye tishio la usalama kutoka kwa mashabiki na wafuasi wa Lissu. Lakini hakuna majina wala maelezo ya mashahidi hao ili mahakama iweze kuamini hayo. Sheria inataka mashahidi hao waape wenyewe na viapo vyao viwasilishwe.
Haiwezekani mahakama ikubali kauli ya Wakili wa Serikali kwa niaba ya mtu mwingine ambaye ndiye yuko kwenye tishio. Hayo ndiyo matakwa ya sheria kuhusu kiapo kama nilivyosema, kwani kiapo ni ushahidi.
Katika mazingira haya, tulihitaji viapo vya waliodaiwa kutishiwa ili mahakama iamue kwa msingi wa ushahidi kuwa maisha yao yako hatarini.
Pia katika kiapo chao wanasema kuwa wafuasi wa Lissu wamejaribu kutafuta majina ya mashahidi kwa lengo la kuwahujumu. Hata hivyo, ilipaswa kiapo hicho kiambatane na viapo vya watu waliosikia au kushuhudia hayo matishio.
Kifungu cha 110(1)(f) cha Penal Code kinaeleza kuwa mtu anayemtishia shahidi au kumzuia kutoa ushahidi anafanya kosa la jinai linaloambatana na kifungo cha hadi miezi sita. Lakini hakuna aliyekamatwa wala kufunguliwa mashitaka kufikia sasa.
Kiapo cha Wakili wa Serikali kinamtaja SACP Faustine Mafwele, lakini Mafwele hajaapa kokote. Wanasema ipo ripoti ya Mafwele kuhusu hali ya usalama, lakini ripoti hiyo haijawasilishwa wala haiwezi kuchukua nafasi ya kiapo kutoka kwa mtu binafsi kuhusu usalama wake.
Ni wasilisho letu kuwa hakimu hakupaswa kufanya maamuzi kwa msingi wa taarifa ambazo hazijathibitishwa kwa viapo vya kisheria. Ruling hii haiwezi kusimama kisheria na haipaswi kuachwa kama ilivyo.
Nimesoma pia kiapo kinzani cha Jamhuri ambacho kwa namna fulani kinaunga mkono maombi yetu. Kiapo chenyewe hakijabainisha wazi hata aliyeapa ni mwanamume au mwanamke. Ni viapo visivyo na umakini wa kisheria.
Kwa kumalizia, nasema hakimu alipokea maombi na viapo vya waleta maombi kule Kisutu bila kuyachambua wala kujiuliza uhalali wake wa kisheria. Hakufikiria athari wala mapungufu ya viapo hivyo, akayakubali kama yalivyo bila tahadhari yoyote.
Ndio maana tuko hapa mbele ya Mahakama hii kuiomba ipitie upya jambo hili na kurekebisha uamuzi huo."
Wakili Jebra
Wasilisho langu litakuwa kwenye msingi wa haki ya haki yakusikilizwa na kuendesha mashauri kwa haki. Ukisoma katiba yetu ibara ya 13(6)(a).
Wakati hakimu anafanya maamuzi haya hakuzingatia kwmaba uamuzi wake utamuathiri mteja wetu katika haki yake ya kusikilizwa kwa haki na kupewa nafasi ya kuona shauri lake linaendeshwa kwa uwazi.
Kwenye maamuzi yale hakufanya uchambuzi wa kwamba kuthibitisha mashtaka inapaswa kuwa beyond reasonable doubt yaani bila kuacha shaka yoyote wakati kuthibitisha kesi za jinai.
Kama angefanya proper analysis angegundua kuwa wasiwasi ulioibuliwa na Dr. NSHALA angefahamu kuwa hakukuwa na maana yoyote ya kutoa order ile aliyoitoa. Maana alishaonyeshwa hatari iliyopo mbele.
Upande wa jamhuri wanapaswa kutimiza wajibu wao wa kama kuna shahidi ametishwa wawakamate wanaowatisha. Sio wameshindwa kutimiza wajibu wao halafu aumie mteja wetu kwa kukosa haki ya kusikiliza kesi yake kwa uwazi na haki ya kuwajua mashahidi na kuwaona.
Mh. Jaji hatuna uhakika hata kama Hakimu alijiuliza hivi mashitaka yanayomkabili mteja wetu ya uchochezi hata adhabu yake ina option ya fine. Na makosa hayo sio serious offence kabisa. Sasa unasemaje kwamba mashahidi watakuwa hawako salama wakati hata mashitaka ni kusema taarifa za uongo sasa si angeweza kuja ambae anajua kuwa ukweli ni upi na kutoa clarification ya ukweli wenyewe.
Makosa hayo kwanza yangeweza kushitakiwa kwa defamation lakini pia hata mpaka sasa hatujaona athari za maneno yaliyosemwa na mteja wetu hadi leo.
Mtobesya
Ni msingi wa kisheria kwamba fair trial inahitaji mshitakiwa akutane na wanaomshitaki na mashahidi na kunakuwa na exception pale ambapo yako maombi maalumu ya kuomba kufichwa.
Mashahidi wakifichwa demeanor haitaonekana kabisa. Na yapo maamuzi ya mahakama ya rufani yanasema demeanor inaangaliwa sana na trial Court na kutokaana na shahidi alivyoonekana basi credibility yake nimeitia mashakaa hivyo ushahidi wake naitulia mashaka.
Maamuzi ya mahakama ya rufani Trazias Evarista alias Deusdedith Vs Republic kesi ya 2020
Kwanini tunasema credibility na demeanor ya shahidi ni muhimu sana. Zoezi la kuficha mashahidi linaweza kutumika kuathiri haki za mtuhumiwa. Sasa mahakama ni muhimu kuwa makini sana wakati inafanya maamuzi ya kukubali kuficha mashahidi.
Sababu za kufanya hivyo zinatakiwa kuwa ni nzito sana. Na uzito wake unapaswa kuwa umeambatanishwa na viapo vya wahusika kama vile ile report ya kiintelijensia ya MAFWELE ilipaswa kuwa imeambatanishwa na kiapo chake.
Sasa tunasubmit kwamba sababu zilizotolewa haziwezi kuondoa umuhimu wa mahakama kuwaona mashahidi na kuangalia demeanor yao.
Mtuhumiwa atashindwa kuielezea demeanor ya shahidi kuishawishi mahakama.
Wasilisho letu ni kwamba hata kama maombi yalisikilizwa exparte yaani upande mmoja tu. Mahakama ilikuwa na wajibu wa kutokukubali kila kinachosemwa na Jamhuri yaani waleta maombi katika maombi yake kule mahakama ya Kisutu.
Ilipaswa kuyasikiliza na mahakama kutumia akili yake na sio kukubali tu. Hili ni kosa la kimsingi na limesemwa na katika kesi nyingi za mahakama kuu na mahakama ya rufani.
Kwa kumalizia tunaomba kusema fair trial inataka mshitakiwa awaone mashahidi na ku access demeanor yao na ukiangalia nature ya ushahidi unaonesha mahakama haikupaswa kuondoka kwenye msingi wa kisheria wa mashahidi kuwa wazi.
Hivyo mahakama ibatilishe uamuzi ule na tuendelee kusikiliza shauri hii kwa taratibu za kawaida na mashahidi tuwaone wanavyoonekana, sura zao, sauti zao na watakayokuwa wanayasema wayaseme tukionana uso kwa uso ili tuone wana ujasiri wakuyasema au wanaona aibu au vinginevyo.
Tunaomba kumalizia hapo kwa upande wetu. Tuwaachie mawakili wa serikali.
Wakili wa Serikali Nasoro Katuga
Katika kuwajibu maombi haya tunaomba mahakama iseme je maombi haya yalipaswa kuwa appeal au revision?
Mhehsimiwa anasema mlikuwa na nafasi ya kuleta pingamizi hapo unachotaka kufanya ni nini?
Anajibu Katuga kuwa wakati wanasubmit wenzetu tumeona ushahidi wao kama una shida ndio maana tumepata hili pingamizi.
Jaji anasema sasa huu sio muda wa kufanya hili unalotaka kufanya. Wewe jibu kama ushahidi wao unashida jibu kupitia ushahidi wako hatuwezi kwenda mbele na nyuma tafadhali.
Anasimama Mtobesya pia anasema anachokifanya hiki sio utaratibu kabisa. Labda mahakama iseme tunasimama kuendelea na kusikilizwa tujadili hoja ya wenzetu.
Jaji anasema sasa maelekezo ninayotoa Jamhuri muache hayo mnayoanza endeleeni kujibu yaliyosemwa na wenzenu.
Kifungu cha 8 cha CPA R.E 2023 kinatoa wajibu kwa raia yeyote atakayeona kuna jinai inaelekea kutendeka basi anatoa taarifa kwa polisi.
Mafwele anasema mashahidi wako katika hatari kwasababu sio hearsay maana polisi akipokea taarifa akiitumia haiwi hearsay.
Kesi ya Masamba Musiba ambayo imetumiwa na wenzetu inafafanua nini maana ya utashi wa mahakama na ndio ambayo mahakama ya kisutu imefanya kama kesi hiyo inavyotaka. Na kesi zingine zote zilizoletwa na wenzetu zinaungana na kilichofanywa na mahakama ya Kisutu.
Mtobesya afanya Rejoinder kwa Niaba ya Utetezi
Baada ya submission ya upande wa Serikali iliyodaiwa kuwa ya kuchosha, Mtobesya alianza kutoa rejoinder akieleza kuwa kesi zote walizonukuu upande wa Serikali ni za madai (civil), ilhali hoja zilizopo mahakamani ni za jinai.
Alikosoa mkanganyiko wa hoja akifananisha na kuchanganya "chai na ugali", na kusisitiza kuwa wao wameleta revision si appeal, hivyo hakuna haja ya kuwasilisha grounds za appeal.
Akijibu madai kuwa mlalamikaji hakuwahi kulalamika kunyimwa haki ya kusikilizwa, alisema maombi yalikuwa ex parte, hivyo asingekuwa na pa kulalamikia.
Kuhusu taarifa za SACP Mafwele, Mtobesya alisisitiza kuwa taarifa zake hazikuwa na uzito kwani hazikuonyesha alizipata kutoka kwa nani, hivyo mahakama haiwezi kuziamini bila msingi.
Alihoji pia namna mahakama inaweza kutathmini demeanor ya shahidi asiyepo mahakamani, ilhali hiyo ni kazi ya mahakama si ya shahidi, akisema shahidi lazima awe "kwenye box" ili mahakama ione tabia na uaminifu wake.
Mtobesya alieleza kuwa wao hawakuomba kupewa majina ya mashahidi bali walitaka mahakama ijue taarifa hizo ili iweze kuamua kwa haki.
Alikosoa hoja kuwa maombi hayo si ya jinai, akieleza kuwa kama si civil basi lazima ni criminal — hakuna kesi ya "katikati".
Pia alifafanua kuwa kifungu cha Katiba 13(6) kinabeba dhana ya haki ya kusikilizwa, hivyo mashahidi wanapaswa kuwa wazi na hoja ya kutowatambua ni kinyume na misingi ya haki.
====
Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imepanga Agosti 12, 2025 kutoa uamuzi wa maombi ya mapitio yaliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu. Uamuzi huo umetolewa leo na Jaji Elizabeth Mkwizu baada ya kusikiliza hoja za pande zote.
Video: Jambo TV