Kilichonishangaza ni jinsi matangazo yalivyorushwa Kila mahali, aise hata kama mtu humpendi ndiyo umfanyie character assassination ya kiasi kile?Ni kweli hata mimi sioni suala la maadili dhidi ya Prof Sedoyeka. Kama ni ufisadi basi wangepeleka TAKUKURU.
Na masuala ya kuhamisha wafanyakazi ndani na nje ndiyo kazi ya Mkuu wa Chuo wala siyo ukiukwaji wa maadili.
Sekretarieti ya Maadili imepewa mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995 sura 398. Sheria hii ilianza kutumika tarehe 01 Julai 1995 na inatumika Tanzania Bara pamoja na Zanzibar kwa viongozi wenye madaraka katika Serikali ya Muungano.
Kuna mtu ameamua kuitumia sheria hii vibaya.