Uchaguzi 2020 Shehe alhad Mussa Salum wa DSM ataka wananchi wachague wagombea Wanawake, adai Mwanamme ni zao la mwanamke, Mdee apiga makofi!

Uchaguzi 2020 Shehe alhad Mussa Salum wa DSM ataka wananchi wachague wagombea Wanawake, adai Mwanamme ni zao la mwanamke, Mdee apiga makofi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Ni katika kongamano la Mtandao wa Jinsia lililozungumzia nafasi ya mwanamke katika uchaguzi mkuu.

Mgeni rasmi alikuwa RC Kunenge na lilihudhuriwa pia na wajumbe wa kamati ya amani mkoa wa DSM na wagombea akiwemo Halima Mdee anayegombea Kawe.

Shehe wa mkoa wa DSM alhad Musa Salum amesema nafasi ya mwanamke katika jamii haipimiki kwani bila mwanamke huwezi kumpata mwanamme, hawa ndio mama zetu.

Alhad Salum amewataka watanzania kutosita kuwachagua wanawake popote pale walipogombea, na kufuatia kauli hiyo Halima Mdee alimpigia makofi.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom