Shehe Ponda aliamsha, adai Mashehe 300 wameswekwa rumande miaka 10 bila kesi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Taarifa iliyotolewa na Shehe mwenye ushawishi mkubwa sana kwenye eneo la maziwa makuu, Ponda Issa Ponda na kunukuliwa na gazeti la Raia Mwema, anaeleza kwamba kuna zaidi ya mashehe 300 waliorundikwa rumande bila kupelekwa mahakamani kwa zaidi ya miaka 10.

Bali haijafahamika sababu hasa ya kuwakamata viongozi hao wa kiroho na kuwaweka kizuizini kwa miaka yote hiyo bila kuwasomea mashtaka yanayowakabili na wala haijulikani kama wote hao wanatuhuma zinazofanana ama la.



Chanzo: Raia Mwema
 
We have to be careful hapa, tusichukue advantage tu ya kuwa Rais huyu ni Mwisilamu basi atatoa kauli. Ninavyojuwa kazi ya She iko Msikitini kuongoza ibada mbalimbali. Mpaka uone Serikali hasa wakati wa JK Mwisilamu mwenzao akiwaweka ndani ujue taarifa zao zilikuwa za hatari.

Toka Hawa watu wawekwe ndani uchomaji makanisa na kuua mapadri kulikoma. Kama tungecheka na nyani basi hawa Alshabab wangetusumbua kama walivyoisumbia Mozambique
 
Miaka 10 nyuma mtawala alikuwa upande uleee!! Angekuwa wa upande mwingine basi yangeongeleka mengine zaidi.
 
Hao mashehe ni hatari kwa usalama nchi sio kila jambo lazima liende mahakamani..hao wamewekwa humo ili nchi ipate utulivu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Usiingie kwenye mkenge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…