DJ SEPETU
JF-Expert Member
- Apr 17, 2017
- 8,413
- 12,336
Tarehe kama ya Leo 1972, katika viunga vya kisiwandui mzalendo na rais Wa kwanza Wa Zanzibar karume alipokonywa uhai wake na wapinga mapinduzi
Karume alizaliwa 1905 huko mwera,wazazi wake mzee Amani alikuwa na asili ya Nyasaland (Malawi) mamaye Bi Amina alikuwa na asili ya Rwanda na walikutana hapo Zanzibar na kuoana.
Baada ya babaye kufariki karume hakuweza kuendelea na elimu dunia sana kwani aliishia darasa la nne.
Aliweza kujipatia elimu kubwa nje ya darasa kutokana na kusafiri nchi mbalimbali kupitia Kazi yake kama baharia.
Baadaye aliacha ubaharia na kujumuika na vijana wenzie ktk harakati za kisiasa.
Na mwaka 1957 ASP ilizaliwa.
Mwaka 1964,26,April ASP na Umma Party walifanya mapinduzi matukufu kuondoa utawala Wa kisultani Zanzibar
Mara baada ya mapinduzi karume alichaguliwa kuwa rais Wa kwanza Wa Zanzibar.
Miezi mitatu baadaye Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda Tanzania huku karume akiwa makamu Wa kwanza Wa rais
Karume atakumbukwa kwa mengi hasa kuwajali wanyonge na kupinga ubaguzi Wa rangi na kikabila.
Kuwajengea wazanzibar makazi bila tozo yoyote isipokuwa maji na umeme