Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,010
- 6,766
Thats the reason hato matusi na mgawanyiko kutoisha.Bakwata ni chombo kwa ajili ya kuwadhibiti waislamu waswahili.
Hawa ndiwo wengi Tanzania. Bakwata haijishughulishi sana na madhehebu ya Shia, Ahmadiya, Bohora, Ismailiya nk.
Wafuasi wao ni zaidi wahindi.
Taasisi za waislamu zimeagizwa na RITA kurekebisha katiba zao zitamke kwamba wako chini ya Bakwata.
Serikali isiyo na dini kwa nini inajiingiza kwenye mambo ya dini.
Hapo ndio wanapotofautiana na Wakristu. Wakristu huwezi kukuta wanatumia madhabahu na altare kushambulia dini au Imani zingine. Bali wanawashibisha Imani waamini wao lakini siku hizi naona clip za mahubiri kutoka misikitini sijui tunaelekea wapiThats the reason hato matusi na mgawanyiko kutoisha.
BAKWATA kama mamlaka ya kisheria ilipaswa kuwa Regulator tu.
Ukienda Misikiti ya bakwata ni kawaida kukuta mashambulizi ya kiimani dhidi ya Mashia, Ahmadiyya na Wahabi.
Je siyo waislamu hao??
Ni bora Bakwata iitwe Baraza la Waislamu Wa Dhehebu la Sunni Tanzania
hakuna uvunjifu wa amani hapa sababu shia wako 1000 tz nzima kadia 200 tz ibadhi 1500 walio baki wote ni sunn hayo sheikh ubwawa nisunn19 January 2023
Dar es Salaam, Tanzania
SHEIKH ABUU - HATARI INAKUJA TUSIPOTOA TAHADHARI KWA MADHEHEBU HAYA MAWILI
Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania ametoa tahadhari hiyo kwa kuwa inaweza kupelekea amani kuvunjika nchini Tanzania.
Sheikh Abuu Iddi CV (wasifu) yake imesheheni nyadhifa kadha wa kadha ktk utumishi kwa dini na jamii kwani yeye ni imamu mkuu msikiti wa Masjid Mnyamani Buguruni jijini Dar es Salaam. Pia kwa miaka 16 amekuwa akiendesha kipindi ktk kituo cha televisheni cha Channel Ten kutoa daawa na darsa, mratibu Al Risala Foundation, Mratibu wa Kudumisha Amani katika mkoa wa Dar es Salaam, Mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina Misingi 15 ya amani, mwandishi wa makala katika gazeti kubwa la Mwananchi pia ni Mshauri wa dini na jamii wa Mufti Mkuu wa Tanzania.
Sheikh Abuu Iddi ameelekeza tahadhari hii hususan kwa madhehebu ya Sunni na Shia yanayo shambuliana kupitia majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii wakiongozwa na viongozi wao.
Amewataja Sheikh Mziwanda na Samir wa upande wa Sunni huku upande wa madhehebu ya Shia kupitia Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Abdul na wenzie watatu wakijitetea.
Na pande hizi mbili za madhehebu haya yakinukuu kile wanachoamini kwamba ni sawa kwa upande wa madhehebu yao.
Pande hizo zimewekuwa zikirushiana maneno yanayotishia amani za kila aina mfano amani ya viungo, amani ya roho, kuvunjiana heshima n.k huku wote wa pande hizi mbili wakiwa na wafuasi wao hivyo kutishia amani kwa ujumla ya Tanzania maana wafuasi wa pande hizi mbili zinaweza kukabiliana kutetea pande zao na viongozi wao .
Mfumo wa uendeshaji wa mijadala hii imeleta ukakasi mkubwa huku maneno ya kutishiana uhai baina ya pande hizo yakitamkwa asema Sheikh Abuu Iddi kwa masikitiko makubwa.
Sheikh Abuu Iddi anasisitiza kuwa BAKWATA ni ya kwa ajili ya madhehebu yote na hivyo haiwezekeni dhehebu moja kuzuiwa kuja ktk shughuli za BAKWATA kama inavyochagizwa na baadhi ya waumini kuwa viongozi wa madhehebu ya Mashia watengwe......
Total contradiction.
Tatizo ni Bakwata kujifanya inawakilisha Waislamu wote. Hata katiba yake inasema mtu akiwa Muislamu moja kwa moja yeye ni mwanachama wa Bakwata.Kuna watu huwa wanajidanganya Sana . Mara oooh! dini yetu hatujagawanyika tuu wamoja maana kitabu chetu hakijachakachuliwa kimehifadhiwa mioyoni. Sasa haya madhehebu yanayokinzana yanamtoka wapi?
Ushauri mdogo. Kila mtu aamini na aendelee na jinsi anavyoabudu wewe usimkosoe Wala kulumbana naye utavunja amani. Wewe amini na wahubirie na wafundishe wale waliokubaliana na wewe. Kwenye Imani yoyote, Kila mtu ansjiona yupo sahihi na humshangaa mwenzake kuhusu Imani yake.
Chukua hii, Mungu ni Mungu wa derivasity. Angeamua kutuumba wote tuwe tunaongea lugha Moja , tuwe tuna rangi Moja, tuwe na Kila kitu sawa na tufanane kama maharagwe angeweza lakini alituumba tofauti kwanza kufikiri, lugha, jinsia, rangi ,Mila na desturi ili uwezo wake ujidhihirishe mbele ya mwanadamu. Kitendo Cha kudhani kuwa Kuna siku tutakuwa na Imani Moja na sawa ni kujidanganya na ni kinyume na mapenzi ya Mungu. Kumbuka wakati wa mnara wa babeli walijifanya wamekuwa na umoja Mungu aliwapiga kombora la lugha wakasambaana
Bakwata sii tatizo hata siku Moja. Yawezekana uwepo wa bakwata na viongozi wake wenye busara wamechangia kikubwa kwenye amani ya nchi yetu. Ninyi wenye Imani hiyo hamuwezi kuliona hilo lakini tuliyo na Imani tofauti twaweza kutoa maoni bila upendeleoTatizo ni Bakwata kujifanya inawakilisha Waislamu wote. Hata katiba yake inasema mtu akiwa Muislamu moja kwa moja yeye ni mwanachama wa Bakwata.
Dhana hii ni kinyume na katiba ya nchi inayompa kila raia uhuru wa kuchaguwa anajiunga na taasisi gani na uhuru wa kuabudu kwa Dini au madhehebu anayotaka.
Bakwata ni chombo kwa ajili ya kuwadhibiti waislamu waswahili.
Hawa ndiwo wengi Tanzania. Bakwata haijishughulishi sana na madhehebu ya Shia, Ahmadiya, Bohora, Ismailiya nk.
Wafuasi wao ni zaidi wahindi.
Taasisi za waislamu zimeagizwa na RITA kurekebisha katiba zao zitamke kwamba wako chini ya Bakwata.
Serikali isiyo na dini kwa nini inajiingiza kwenye mambo ya dini.