Sheikh Abuu: Tujihadhari, amani inaweza kuvunjika kupitia mijadala ya kimadhehebu inayoendelea

Huyo Abuu ni mnafiq mkubwa, mijadala ya kimadhebu haijawahi kuanza leo wala jana, kwanza yeye si alianzisha mjadala na Abul Fadhil je alijibu hoja au ndio anawatetea hao maraafidhwa wenzake? Hatari sana huyo shehena abuu iddi
Unamuita mwenzio mnafiki?
 
23 October 2022

JUMUIYA ya BOHORA TANZANIA WALIVYOADHIMISHA SIKU ya KUZALIWA MTUME MUHAMMAD S.A.W PBAH..


Jumuiya ya Bohora Tanzania leo hii imeadhidisha Siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad S.A.W sambamba na kuadhimisha siku ya kuzaliwa kiongozi mkuu wa Bohora Duniani Ali Cattar miaka 79 Sherehe hizo zilitanguliwa na maandamano ya Amani kutokea mtaa wa Zanaki ulipo msikiti wa Bohora kupitia barabara ya Biti Titi Mohamed na kuishia katika msikiti wao mwingine Upanga Jijini Dar es Salaam Tanzania
 
Si huwa wanasema kuwa hawajagawanyika?

Wajuzi naomba Sasa tofauti ya wale wa suruali fupi, wale wa kawaida ambao wanafunga na kusubiri mpaka waone mwezi kwa macho na Hawa wapya wanaoviringisha vitambsa kichwani
Ukweli ni kuwa wamegawanyika. Na pamoja na wote kujiita waislamu wana tafauti nyingi kwenye itikadi zao.
 
Hawa wanaojadili madhehebu ni wakumbaff ambao vichwa vyao vimejaa matope na mabaki ya ukoloni
 
Kwanini ashindwe kusema ukweli kua mashia ni wapotofu au kisa ndio marafiki zao wanaowapa sent

Mashia ni wa kupigwa vita tu hawafai ata kidogo

Kosa lao hao shia ni lipi?
 

MWAMKO WA MADHEHEBU YA USHIA TANZANIA.​



Sheikh Waziri O. Nyello
aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanzania Ithna Ashariyyah Community (T.I.C), amesema kuwa harakati za Sheikh Hemed Jalala za kutangaza Madhehebu ya Ushia zimeleta mwamko wa Ushia Tanzania, ususani sehemu za Vijijini, ukitofautisha na kipindi cha nyuma, pia amesisitiza kuwa vijana ndio chachu ya mabaliko ya aina yeyote hivyo wanatakiwa kumuunga mkono Sheikh Hemed Jalala, hili aweze kufanya kazi zaidi ya kufikisha ujumbe wa Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s).

Posted by Afroshia
 
Mashia wanawatukana maswahaba
Wamemtukana Umar,Abubakar na Uthman na maswahaba wengine kma Abuu huraira

Mtu ambae hawaamini maswahaba hawa tuna mashaka sana na imani nae pia wana vitendo vichafu na viovu vingi tu

Wewe hao wasipo waamini hao maswhiba kinachokuuma nini?au wewe ndio mlizi wa mbinguni kwamba utaazuia wasiingie. ?
 

Sababu Tano (5) za Sisi Mashia Kuwatakia Mkono wa Kheri,Baraka na Fanaka Ndugu zetu Wakristo kwa Kusheherekea Krismasi na mwaka Mpya Wao.​

​
Kiongozi wa Kiroho wa Waislamu Shia Ithnasheriya Maulana Sheikh Hemed Jalala akitoa Mkono wa Baraka, Fanaka na Kheri kwa Ndugu zetu Wakristo kwa Kusherekea Sikukuu yao ya Krismasi na Mwaka mpya, leo Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es salaam, wakati akiongea na Waandishi wa Habari.

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe Kwenu Nyote.


Sababu ya Kwanza:
Ndugu zetu Wakristo waliyopo Tanzania na waliopo Duniani kwa Ujumla tunashirikiana nao katika kuamini kwamba Mwenyezi Mungu (swt) alituma Vitabu kwa uchache Vinne hapa Duniani, Kitabu cha kwanza ni Taurat, Kitabu cha pili ni Injil, Kitabu cha tatu ni Zaburi na Kitabu cha nne ni Qur’an.
Injili ni Kitabu ambacho ndicho kipo mikononi na kukifanyia kazi na kukiamini Ndugu zetu Wakristo, lakini sisi waislamu katika Imani zetu ni kuamini Vitabu hivyo vyote, ikiwemo Taurat, Injil, Zaburi na Qur’an, kwahivyo ni wenzetu kwamba tunashirikiana nao kwa vitabu vilivyoteremshwa kutoka mbinguni kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Sababu ya Pili:
Kwanini Mkono wa Krismasi?, Kwani wa kuwapa hongera kwa kusheherekea sikukuu yao ya Krismasi?, ni kwa sababu ni Ndugu zetu. Imam Ali (a.s) anatoa maelekezo wakati akimtuma Malik Ashtar akielekea Misri, katika maelekezo alimuambia unakwenda Misri huko utakutana na Waislamu ni ndugu zako katika Dini, lakini utakutana na watu wa Dini Nyingine hao ni ndugu zako katika Uwanadamu na katika Utu, sisi sote Baba yetu ni Adamu (a.s), tuwe Waislam, tuwe Wakristo, sisi sote mama yetu ni Hawa au Eva (a.s) tuwe Waislam, Tuwe Wakristo.

Sababu ya Tatu:
Kwanini Mkono wa Kheri na baraka na pongezi kwa Krismasi kwa ndugu zetu Wakristo wa Watanzania?, ni kwa sababu ni shehemu ya Watanzania. Kila itakavyokuwa Tanzania ina Waislamu Masuni, ina waislamu Mashia, ina Mapagani, ina watu wa dini nyingine vile Wakristo nao wapo.
Kwahivyo tutaendelea kubakia kama Watanzania Waislamu, Watanzania Mashia, Watanzania Masuni, Watanzania Wakristo na Watanzania wasiokuwa na Dini, kwa hivyo tunapotoa Mkono wa kheri na baraka kwa sababu ya Krismasi ni moja ya Kuboresha mahusiano mema kwa sababu sisi sote tunakusanywa na mwamvuli wa Utanzania.

Sababu ya Nne:
ni jambo la Kuvumiliana, Qur’an inatueleza Umma wa kati na kati, yani umma unaovumiliana, moja ya sababu ya sisi kutoa mkono wa baraka na kheri ya krismasi kwa ndugu zetu Wakristo wa Tanzania, ni kwa sababu ya kutoa funzo la kuvumiliana kwa watanzania na watu wenye dini tofauti.
Na kwamba sisi tutaendelea kubakia na dini zetu, wasije wakadhania Waislam Mashia na Masuni iko siku watawabadilisha Watanzania wote watakuwa Waislamu, siku hiyo haitotokea, wala Wakristo wa Tanzania wasije wakadhania watawahubiria Waislamu Mashia na Masuni watakuwa Wakristo. Kwa hiyo tutabakia Wakristo tupo, Waislamu tupo, Mashia tupo, watu wa Twariqa tupo, kwa hiyo kubwa ni kuvumiliana tukiwa na dini zetu tofauti na Mitazamo yetu tofauti.

Sababu ya tano:
Mwisho jambo la tano muhimu na kubwa, sisi Tanzania ni watu ambao tunaishi kwa Amani, tunaishi kwa Utulivu, tunaishi kwa Kheri, Tanzania yetu haijui vita, Tanzania yetu haijui kugombana, Tanzania yetu haijui Silaha, Utulivu huu na Amani hii kuuboresha ni Wajibu wetu kama Viongozi wa Dini,ni wajibu wetu kama Wanadini.
Moja ya mambo ambayo tunaamini, yataboresha Amani ya nchi yetu, yataboresha Umoja wetu wa Wawatanzania, yataboresha kuvumiliana kwetu tuliokuwa nao Watanzania, ni Vikao kama hivi vya kutoa Mkono wa Kheri ya Krismasi na Kheri ya Mwaka mpya na baraka ya Mwaka mpya, jambo linaloishiria Umoja, Mshikamano na Kukaa Vizuri katika nchi Moja na Taifa moja.

Mwisho: Namuomba Mwenyezi Mungu (swt) Krismasi hii ya ndugu zetu Wakristo, Mwenyezi Mungu aipitishe kwa Kheri, aipitishe kwa baraka, aondoe majanga na mabalaa yote barabarani na majumbani,na aifanye ni Krismasi ya Kheri kwa ndugu zetu Wakristo wa Tanzania wote, lakini pia tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) azidi kuboresha Umoja wetu wa wawatanzania, Amani yetu ya Tanzania,Mungu aendelee kuifanya Tanzania kisiwa cha Amani,Kisiwa cha Upendo, Kisiwa cha Kuvumiliana, Asanteni Sana na Mungu awabariki.

Imetolea na:
Maulana Sheikh Hemed Jalala
Kiongozi wa Kiroho wa Waislamu Shia Ithnasheriya
25/12/2019,
 
24 December 2022
SHEIKH JALALA ATOA SALAM ZA KRISIMAS KWA WAKRISTO NCHINI

 
Kwani mtume((s.a.w) alikuwa suni au shia?
Makundi ni 73,moja la peponi, tujitathmini.
 
Wewe hao wasipo waamini hao maswhiba kinachokuuma nini?au wewe ndio mlizi wa mbinguni kwamba utaazuia wasiingie. ?
Kajifunze kuandika kwanza halafu njoo tena

Ujinga ni mzigo mzito sanaa
 
Kwani mtume((s.a.w) alikuwa suni au shia?
Makundi ni 73,moja la peponi, tujitathmini.
Asili ya madh hab ni dhahaba yaani ni mwendo na mwendo. Wingi wake ni madh hab ni mwenendo.

Kulikuwa na madh heb zaidi ya 10 na yalijulikana. Kipindi cha Taabeena wote walikuwa ni mujtahid. Wale ambao hawakuwa mujtahid walikuwa wanawafuata Imam zao.

Watu wa dasmus walikuwa wanawafuata (Maimam) Muadh ibn Jabar na Abu Dardar. Watu wa Kufa walikuwa wanawafuta Abdallah ibn Mas'oud na Ally ibn Taalib. Watu wa Madina walimfuata Imam wao Abdallah ibn Umar. Watu wa Makkah walimfuata Abdallah ibn Abbas.

Hivi ndivyo madh heb yalivyoanza na hao wote ni maswahaba wa Mtume Muhammad swallallahu alayhi wasallam. Maswahaba wa Mtume ni 124,000. Hivyo kuna wengine walikuwa ni wajuzi zaidi ya wengine kwenye elimu na baina yao kuna wengine walikuwa na sehemu ya elimu ambayo mwengine hana!

Na ndiyo maana inahimizwa tusome tusiwe watu wa kupinga pinga kisa kasema Sheikh unayemkubali wewe!

Baadhi ya Tabiina walikuwa ni wanawazuoni wakubwa walichukua elimu kutoka kwa maswahaba tofauti. Na Tab tabiina came to develop and compare and discuss. Wa kwanza alikuwa Imam Akbar Nuuman ibn Thaabit Imam Abou Hanifa. Imam Malik na madh heb mengine ni ya Sufyan Ath-thawriy nchini Iraq. Ibm Saad nchini Misri. Al Imam Al Auzairii nchini Syria n.k madh-heb ya Imam Idrisa ibn Muhammad Ashafiiy. Mpaka madh-heb ya Imam Ahamad bin Hambal.

Hivyo, mtu akiulizwa unafuata madh heb gani wanamaanisha ufahamu wako wa quran na hadithi unafuata kwa mwenendo wa nani? Maadamu huo mtiririko wa kufuata na kirithishwa elimu ndivyo yalivyopokelewa na wanafunzi wao mpaka kutufikia sisi, hivyo wa zama zetu hatuna jipya bali tumepokea elimu hii ya dini kutoka kwa miongoni mwa hao maswahaba. Kwa misingi hiyo mwenendo wangu wa mapokeo ya elimu ya dini ni ya Imam Shafii kwa maana madh-heb ya Imam Shafii kama ulivyopokelewa na wanawazuoni kama walivyowaelewa wanafunzi wa maswahaba kama maswahaba walivyomuelewa Mtume.

Ndivyo Tabiina na Tabtabiina walivyoishi na sisi ndivyo tunavyoishi. Walifuata mwenendo wa Imam zao na si tunarithi kutoka kwa wanafunzi wa hao maimam ambao ndiyo wanawazuoni wetu.

__________________

Kesi ya Shia ni kutokana na sahaba mmoja wa Mtume aliyesilimu kinafki na Mtume alimfahamu. Huyu Sahaba anaitwa Abdillahi ibn Saaba. Umar akamwambia Mtume huu ni ugonjwa na inabidi utafutiwe dawa. Na Umar akisema daawa anamaanisha inabidi wauliwe. Hoja ya Umar ni kuwa ukiachwa utaenea. Hivyo, wauliwe mara moja kabla ya hawa wanafik wakavuta kundi baina ya waislam na kuwaathiri kwa unafik wao.

Mtume akwambia hapana ewe Umar! Isije ikasemwa Muhammad amewaua masahaba zake na kufupisha histori na kwamba Ushia umeanzia kwa Abdillahi Ibn Saaba! Lakini mashia wenyewe wametofautiana kuna wengine wanafuata fiqh yetu na kuna wengine fiqh yao wanawazuoni wa sisi sunni tunafuata: Haya ni masuala ya kielimu ni mazito sana!

Tufanyaje! Sunni and Shia have lived peacefully together for centuries. Dili na imani yako, ifundishe familia na jamii yako iifahamu haki ni ipi na maadamu unampenda Mungu heshimu viumbe wake. Ikhtilafu baina yetu isiwe vurugu. Kama wao wanaamini hivyo sisi sunni tunaamini hivi. Pengine inatubidi tujue Mtume alidili vipi na watu waliyomtukana itatufungua zaidi.
 
"wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini"

👆👆👆 unaweza kuweka dalili?
 
"wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini"

👆👆👆 unaweza kuweka dalili?

Maneno mazito ya kuzingatiwa ya Mwanazuoni Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mpaka akatunikiwa kilemba cha (u- ayatollah)kuashiria kutambuliwa usomi wake katika imani yake ya dini aliyopata katika vyuo kadhaa alivyosoma kwa bidii miaka kumi na moja mfululizo.
 
Maneno mazito ya kuzingatiwa ya Mwanazuoni Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mpaka akatunikiwa kilemba cha ayatollah kuashiria kutambuliwa usomi wake katika imani yake ya dini aliyopata katika vyuo kadhaa.
Kumbe we jamaa ni shia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…