Sheikh Abuu: Tujihadhari, amani inaweza kuvunjika kupitia mijadala ya kimadhehebu inayoendelea


Maneno sawa shida vitendo,paragraph yako ya mwisho imekaa kinafiki sana miongoni mwa jamii za kiislamu.
 
Kila dhehebu lijitegemee, kwani bei gani? 🤣
 
unaweza ukawa na elimu lakini isikusaidie kitu, ndiyo maana nikaomba dalili kwanza maana hii dini haiendeshwi kwa maneno ya marja .
 
Maneno sawa shida vitendo,paragraph yako ya mwisho imekaa kinafiki sana miongoni mwa jamii za kiislamu.
Soma historia ya Uislam: Dola ya Uthumaniyya (Ottoman) ni dola ya Kiislamu. Imetawala miaka 600 duniani. Ndani ya hii dola ziliishi jamii tofauti wakiwemo hawa tunaowazungumzia hapa! Sunni na Shia. Ulisikia vita baina yao? Au vurumai ya aina yoyote baina yao?

Katika kitu ambacho dunia ya sasa imekikosa kwa waislamu na wasiyo waislamu ni huruma ya Mtume Muhammad swallallahu alayhi wasallam kwenye maisha yake yalikuwaje!

Leta taswira unampatia Muislamu wa sasa hivi zawadi ya pombe atakufanyaje?

Lakini Mtume alizawadia kwa zawadi ya pombe na sahaba yake. Mtume akamwambia; je, wajua ya kwamba pombe ni haramu? Sahaba akajibu sina taarifa hiyo! Kisha sahaba huyo akamnong'oneza msaidizi wake aliyekuja naye na kumpatia ile pombe. Mtume akamuuliza umemwambiaje? Sahaba akamjibu nimemwambia aende akaiuze. Mtume akamwambia aliyeifanya haramu kuinywa pia ameifanya haramu kuuzwa.

Ukurasa huu kwako ni mgeni, kwa nilichokifanya unaniita mimi mnafiki kwa sababu huu ukurasa haukukudirikia. Mtume alimwambia mmoja wa sahaba kama unampenda Mungu kuwa na heshima na viumbe wake.

Mtume aliulizwa na bedui ewe Muhammad umetujia na nini? Mtume akataja kwanza ni ubinadamu na mtiririko aliyoutaja dini ikawa ni ya mwisho.

Mmoja katika warithi wa Mtume, Imam Junayd Al Baghdadii anasema kabla ya kumfundisha umtu dini mfundishe kwanza tabia njema kisha ndiyo dini. Imam Malik anasema atakayesoma sharia pasipokuwa na mafunzo kujifunza masomo ya tabia njema ama malezi huyu mtu atakuwa ni fasiq. Na atakayejifunza masomo ya malezi pekee pasipo na sharia huyu mtu atakuwa ni mzandiki. Na yule atakayeyachanganya haya mawili kwa pamoja yaani elimu ya malezi ya tabia njema na sharia basi huyo mtu atakuwa katika haki. Kwa sababu Mtume hakufundisha dini tu bali na tabia njema.

Huu ukurasa hauujui ndiyo maana mimi kuweka hivyo unaniona ni mnafiki. Haufahamu kuwa the shortest way ya kufika kwa Mungu katika uislam ni mahaba/upendo. Popote nitakapo simama nasimama na upendo. Kwa sababu hata kafiri uislam haujataka umchukie bali ukafiri ndiyo uchukiwe. Kwa sababu ukafiri hata muislam mwenyewe anaweza akatumbukia humo hivyo uuchukie ila si mtu.

Roho yangu ipo mbele ya kasi ya mwili wangu inaniambia huu mwili ni mzito wa kusonga nami. Hivyo naenda! Ndipo inapoishi roho yangu, sina chuki. Nipo kwenye hali ya mimi mwenyewe. Na huwa inanifikia pahala sijihisi mwenye kupenda wala sijihisi mwenye chuki. Nipo kwenye hali ya mimi mwenyewe na Mola wangu.

Kuna mengi ila mimi naishia hapa!
 
unaweza ukawa na elimu lakini isikusaidie kitu, ndiyo maana nikaomba dalili kwanza maana hii dini haiendeshwi kwa maneno ya marja .

Shehe huyu ni mtu mzito kwa maana amejawa elimu ya dini na elimu duniya, amechota mengi toka katika mabuku, tuwe na kiasi sisi maamuma.

KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)
 
Hawa jamaa wakiwa ktk hali ya unafiki utawasikia 'waislamu wote ni ndugu' kumbe kuna fukuto kama lote!
 
26 January 2023

Sheikh Abuu Iddi : BAKWATA Ni Mwamvuli wa Kuwafunika Waislamu Wote


Awanasihi viongozi na maimamu wenziwe katika imani waache kushindana na Mufti ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Tanzania. Lugha za khutuba za viongozi na maimamu ziwe za sawasawa yaani zisiwe za kama zinazotumika ktk mipasho au vijiweni.

Sheikh Iddi ambaye ni mshauri wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania atoa angalizo kwa wanaoishambulia BAKWATA na asisitiza ubaguzi wa kimadhehebu hautakiwi


Sheikh Abuu Iddi anasisitiza haki ya waumini wa madhehebu mbalimbali kuwa na itikadi zao pia wasibaguliwe awaasa waumini kuwa na uvumilivu.

Sheikh Abuu Idd aelezea kwa kina katiba na muundo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania yaani BAKWATA na ni kina nani wana sifa za kuwa viongozi kwa mujibu wa katiba ya BAKWATA kuanzia ngazi za msikiti hadi Taifa pia muda wa viongozi kukaa katika uongozi na jinsi ya kuondoka ktk uongozi ikiwemo kujiuzulu n.k n.k

Sheikh Abuu Iddi mbali ya kuwa kiongozi pia ni mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina : Nasaha kumi kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Mzee Mohamed Said anaweza akaelezea kwa historia mwanzo haikuwepo BAKWATA kulikua na EAMWS sikumbuki ndio ilikua inaendeshwa na waislamu baadae Hayati JK NYERERE akaiua EAMWS akaunda BAKWATA, kwa hio mvurugano ukaibuka hapo mpaka sasa mvurugano haujaisha na sababu ni Mali za BAKWATA yaan EAMWS zinazomilikiwa na watu BINAFSI kwa manufaa yao BINAFSI sio manufaa ya BAKWATA mtufuano ndio upo hapo, Mzee Mohamed Said au nimesema uongo hapo?
 
Ndugu yangu Hammaz, kuna kitu katika comment yako nakirekebisha. Kwanza hakuna Swahaba wa Mtume aliyesilimu kinafki. Hakuna Swahaba wa Mtume aliyekuwa mnafiki. Inabidi urejee tena kusoma ni nani Swahaba wa Mtume. Wanafiki walikuwa wanajulikana na walikuwa ni wachache na hawahesabiwi kama maswahaba wa Mtume. Hakuna Swahaba wa Mtume alikuwa mnafiki. Rejea maana ya Swahaba. Na ni katika itikadi yetu kuwa Maswahaba wote (Radhi za Allah ziwe juu yao wote) walikuwa ni waadilifu na hakuna hata mmoja wao alikusudia kusema uongo. Na kuwapenda wao ni Imani na kuwachukia ni unafiki.

Pili 'Abdullah Ibn Saba Myahudi alidhihiri wakati wa Khalifa wa tatu, 'Uthmaan ibn 'Affan. Hakuwa swahaba wala hakuwa tabi'i. Na kwake yeye ndio yakawa asili ya ushia.

Tatu, hakuna tunachokutana na mashia katika dini hii (Uislam). Kuanzia misingi kabisa mambo ya 'Aqidah ndio tofauti inapoanzia, kabla ya kwenda kwenye mambo ya kifiqhi.



Mimi naona niishie hapa.

Kisai Kazakh destroyer
 

Ingekua waisalm wana upendo kama wewe hakika dunia ingekua mahali salama pakuishi. Ila tatizo sasa ni mwendo wa magaidi kila kona yakiua na kuumiza kwa jina la mungu wenu.
 
Sisi hatufanyi vurugu dhidi ya Mashia. Masheikh zetu wanakifanya kile unachoshauri kwamba wawafundishe watu haki ni ipi. Ndicho wanachokifanya na ndicho walichokifanya wanachuoni wetu tokea mwanzo huko. Jaribu tu kuangalia wanasema nini wanachuoni kuhusu Shia kuanzia wanachuoni tokea zama pote hili lilipodhihiri. Angalia maImam wanne walisema nini kuhusu wao na kadhalika.

Halafu pia usifananishe zile tofauti kati ya Sunni na Shia na ikhtilafu za kimadhehebu mfano madhehebu nne. Hii si sawa. Utofauti wa Shia na Sunni (Waislam) ni mkubwa mno kiasi kwamba hawawezi kukutana katika lolote ndani ya dini ya UISLAM. Wala sio ikhtilaf tu za kimadhehebu. Maswahaba wote walikuwa na Itikadi moja (hawakutofautiana katika misingi) na walioifuata njia yao ikiwemo MaImam wanne hawakutofautiana katika misingi. Na ndio maana wote ni wanachuoni wa Ahlus Sunnah. Tofauti ni katika masuala ya kifiqhi tu. Hii ni tofauti na Ushia kwetu sisi. Ushia kwetu sisi sio kama tofauti ya Madh-hab ya Shaafi'i na Madh-hab ya Hanbali, bali Ushia ni dini nyengine kabisa inayojitegemea.

Sunni and Shia have lived peacefully together for centuries.
labda ufafanue vizuri kauli yako hiyo. Tukiitazama historia kuna mengi, lakini turudi katika huko kuishi peacefully baina yetu kuliwezekana kwa kule Mashia kufanya mambo yao bila kuwabughudhi Waislam. Hata kwenye miji yetu, hawa Mashia wa humu walikuwa wakiishi wenyewe kwa Taqiyya wakificha itikadi zao na kufanya mambo yao wenyewe bila kuwaingilia ingilia Waislam (wakati huo Mashia walikuwa ni jamii za wahindi).

Ila walipokuja hawa waswahili wenzetu walioingizwa katika Ushia na kwa kuchochewa na mapinduzi ya Iran wakaanza kuzigusa gusa itikadi za Ahlus Sunnah, wakitafsiri baadhi ya vitabu vinavyoshambulia itikadi zetu kwa lugha ya Kiswahili na kuanza kuwasema vibaya Maswahaba (Radhi za Allah ziwe juu yao wote) kiufupi wakaanza kudhihirisha baadhi ya itikadi zao ambao wanazo siku zote ila huwa wanazificha (wanafanya Taqiyya) , ndipo walipoibuka baadhi ya masheikh na kuanza kuitetea itikadi ya Ahlus Sunnah kiufupi wakafanya kile unachokishauri kwamba
ifundishe familia na jamii yako iifahamu haki ni ipi
Ndicho wanachokifanya masheikh zetu sisi. Hawawezi kukaa kimya kwa kisingizio eti cha umoja. Lakini wanapoongea wanaonekana wanaleta vurugu.

Kisai
 
Huyo Abuu ni mnafiq mkubwa, mijadala ya kimadhebu haijawahi kuanza leo wala jana, kwanza yeye si alianzisha mjadala na Abul Fadhil je alijibu hoja au ndio anawatetea hao maraafidhwa wenzake? Hatari sana huyo shehena abuu iddi

BAKWATA ni taasisi kubwa, tamko lao huchukuliwa kwa uzito na wadau wote .

Tanzania - Local threat​


Due to local threat in Tanzania from Friday 27 January up to and including Monday 30 January 2023, some of our flights to, from or via Dar-es-Salaam (DAR), Kilimanjaro (JRO) and Zanzibar (ZNZ) may be disrupted. We are doing our very best to help you on your way again - KLM
 
Duh hii mada ya moto na sikuwa nimeiona ngoja nianze page ya kwanza, shukran kwa wito mkuu.
 
Kwa madini haya itakuwa utovu wa adabu mimi kuongezea lolote.
 
Swali, muundo wa bakwata unawajumuisha madhehebu yote?
 
muundo wa bakwata unawajumuisha madhehebu yote

Swali zuri, kwa mujibu ya Sheikh Abuu ni kuwa BAKWATA lazima iingozwe na Sunni ingawa kama mwamvuli BAKWATA ni ya madhehebu yote.

Sababu ya katiba ya BAKWATA kutamka kuwa lazima viongozi wake wawe Sunni, ni kuwa dhehebu hilo ni wengi zaidi kwa mujibu wa Sheikh Abuu.
 
Reactions: Auz
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…