Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo sheikh wa Dar es Salaam, Mussa Alhadi kabla hajaomba dua kwenye hafla iliyomjumuisha Rais Samia, alitoa salamu za kamati ya amani kumshukuru kwa kutimiza maombi yao ya kumuachilia huru Mbowe na wenzake kutoka kwenye kesi ya ugaidi.
Sheikh Alhadi: Napenda nitoe salam za kamati kukushkuru wewe mheshimiwa Rais, hivi karibuni uliwapa heshma kubwa viongozi wetu wa dini kukutana nao Ikulu.
Katika jumla ya mambo pia walikushauri namna ya kuangalia mienendo ya kesi za watuhumiwa mbalimbali hata wale ambao walituhumiwa kwenye mambo ya ugaidi, mheshimiwa Rais vyombo vyako kwa haraka sana vikashughulikia kesi hizo na tukaona tukashuhudia kama watanzania baadhi ya ndugu zetu ambao sasa wamekuwa huru na wamerudi kuchanyika na watanzania wenzao.
Jambo hili ni jambo jema ambalo mheshimiwa Rais tunakushukuru sana wana-amani na wana-maridhiano kwa usikivu mkubwa na kusikiliza rai, ushauri na maoni ya viongozi wetu wakuu wa dini na wanzetu hawa kuwa huru sasa.