TANZIA Sheikh Doga amefariki Dunia

Inna lillah wainna ilaihyi rajiun.

Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake, amfutie adhabu kabri na amjaalie PEPO "Jannat Firdaus"
 
Namkumbuka akijibu maswali kiufasaha kabisa kwenye kipindi cha Maswali na majibu ya dini ya kiislam RTD enzi hizo
 
إنا لله و إنا إليه راجعون
 
Adhabu ya kaburi ndiyo nini?
Ni adhabu wanazoadhibiwa makafiri na waovu wengine kaburini kabla ya kufufuliwa siku ya kiyama. Sasa kwa sababu hakuna binadmu aliyekamilika, anapokufa muislamu mwenzetu tunamuombea kwa Allaah kama mwislamu huyu aliteleza akafanya dhambi ambayo yapasa kwa dhambi hiyo kuadhibiwa kaburini basi Allaah AMSAMEHE na amuepushe na adhabu ya kaburi. SWALI LAKO LIMEJIBIWA.
 
Allah ampe shufaa
 
Allah akuepushe na adhabu ya kaburi
Hiyo dua wachimba makaburi hawaipendi huwa wanasema wao huwa hawaombewi hiyo dua wakichimba makaburi

Je ina maana wao adhabu ya kaburi inawahusu? Ndio maana huwa hawaombewi Allah awaepushe na adhabu ya kaburi wanapochimba?
 
Namuombea kwa Allah amuweke mahali pema kwenye pepo ya daraja la juu,ila Natoa rai kwa wanazuoni wa Kiislamu waache kujitoa fahamu wanakuwa mbele ya viongozi wa serikali na CCM kwa kushindwa kukemea maovu yanayotendwa na viongozi hao au watendaji wa serikali kwa sababu ya maslahi machache ya kidunia mfano kwenye sakata linaloendelea hivi sasa nchini la binti aliyefanyiwa ukatili wapo kimya wameshindwa kutoa kauli hata ya kulaani tu.
Nawasikitikia sana.
 
Kumbe mtu anakufa na dhambi maombi kwa mola yanamuepusha na adhabu!
 
R.IP
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…