Si kweli. Chanjo ya Covid-19 ni hiari ya mtu binafsi. Hakuna usajili wa misimamo ya jamii za kidini, kikabila wala kisiasa.
Kinachopambaniwa hapa ni LEGACY ilyohujumiwa kwa kukubali uwepo wa Covid-19 nchini, kutelekeza nyungu na juisi ya ukwaju+tangawizi halafu (the unforgivable insult), kuleta chanjo na kuipigia chapuo la nguvu nchini.
Sasa uamuzi ni wako: ni ama uko na SISI au uko na LEGASI.
Ukiwa na sisi utaijua kweli nayo itakuweka huru: utakuwa huru kweli kweli kuamua uachanje au usichanje.
Ukishikamana na legasi, hakika utavutwa chini na nguvu za sumaku ya kielektroniki hadi kwenye jukwaa linalochambua na kuchuja mkorogo wa chanjo, 5G, muhuri wa mpinga kristo, chapa ya 666, vinasaba vya DNA na RNA…
It’s a non-issue; a non-discourse. Just a futile venture into idiocy.