MJINI CHAI
JF-Expert Member
- Dec 12, 2010
- 2,202
- 1,228
Rivieler Gadern School.............Ilikuwa shule gani mkuu!?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rivieler Gadern School.............Ilikuwa shule gani mkuu!?
Mkuu, ukikubali kusoma shule ya wakatoliki ukubali na utamaduni na shelia zao, kabisa mtu anaweza kuamini kuwa wakatoliki wanaweza kuwatengea madrasa ili muendeleze dini yenu. Hivi Morogoro Muslimi University unaweza ukasoma mkristo na ukafuata tamaduni za kikristo? Jibu ni hapana! Kama ilivyo kwenye shule za missionaries hata kwenye vyuo/shule za muslim suala la ibada ni lazima. Sasa mbona Wengine hawalalamikii hili! Jambo la msingi ni kwamba ukikubali kuingia kwenye chuo cha MMU huku unajua msingi wa chuo hicho unajengwa na uislam then ukalalamika kuwa tunalazimishwa kwenda msikitini wewe ndio utakuwa una tatizo na shule zilizojengwa kwenye misingi ya kanisa vivyo hivyo,Uongo siyo Mzuri hata kidogo Ndugu yangu................mimi ni mwenye asili ya Kilwa na nimesomea huko shule ya msingi......Mzazi wangu ''Mungu ampunguzie Adhabu za Kabri'' Alinibadilisha Jina na kunipa jina la KIBANTU ili kuficha UISLAM wetu na hatimae nilipofika form 6 nilikuwa tunafuga Nguruwe.......yote hiyo ni kutaka kujua Mtu ana DINI gani........!!!!????? nimeshika mpaka Chetezo la Ubani KANISANI siku ya misa kama Mtoto wa kanisa la RC............!!!
Ukifuatilia utakuta hata jaji Augustino Ramadhani nae ilikuwa hivyohivyo.nakumbuka babu yangu ilibidi abadili jina kutoka athumani hadi joseph ili tu aweze kupangwa shule kwa kipindi hicho nyingi zikimilikiwa na wamisionari,
bila good enough alibadili jina ila imani yake haikutetereka R.I.P babu
Unapo quote Hivi umejijaribu kujishughulisha japo kusoma post zilizotangulia ili kupata Maudhui ya jambo linalozungumzwa....???!!! Au shuleni ulienda kusoma Ujinga...............???? si kila jambo unaweza changiaa.......! mengine yamekuzidi kimo Mjukuu wangu............ yasome tu........Mkuu, ukikubali kusoma shule ya wakatoliki ukubali na utamaduni na shelia zao, kabisa mtu anaweza kuamini kuwa wakatoliki wanaweza kuwatengea madrasa ili muendeleze dini yenu. Hivi Morogoro Muslimi University unaweza ukasoma mkristo na ukafuata tamaduni za kikristo? Jibu ni hapana! Kama ilivyo kwenye shule za missionaries hata kwenye vyuo/shule za muslim suala la ibada ni lazima. Sasa mbona Wengine hawalalamikii hili! Jambo la msingi ni kwamba ukikubali kuingia kwenye chuo cha MMU huku unajua msingi wa chuo hicho unajengwa na uislam then ukalalamika kuwa tunalazimishwa kwenda msikitini wewe ndio utakuwa una tatizo na shule zilizojengwa kwenye misingi ya kanisa vivyo hivyo,
Miaka hiyo,hali hiyo ilikuwa ni ya kawaida sana. Kuna brother wangua likuwa anaongoza darsa lao, Jina likampoza. Akarudia kwa jina ja John, akafauru. NOwdays tushukuru hizi namba za mitihani, kidogo hutusaidia.
Sheikh Hamisi Mataka
Shule ya Msingi Mchikichini sikupata kushika zaidi ya nafasi tatu za juu muda wote wa miaka saba hapo shuleni. Kwa kuwa nilianza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 11 ule moja wa miaka mine ambayo ningekuwa shule ya msingi iliniwezesha kumiliki chuo changu mwenyewe yaani madrasa, nikiwa mwalimu mkuu katika umri mdogo wa miaka 15.
Nilipoanza shule darasa la kwanza katika huo umri wa miaka 11 ambao ni mkubwa kwa kuanza darasa la kwanza pale Shule ya Mchikichini nilikuwa pia mwalimu wa dini kwa wenzangu.
Kwa ajili ya makuzi yangu ya Kiislam nilikuwa nikilitoka eneo la shule tu nilivaa kanzu yangu juu ya sare kwa kuwa sikujisikia kuvaa kaptula mitaani kwani uchi wa mwanmme unaanza juu ya magoti yake.
Mwalimu wangu wa Historia Mzee Kasunsumo alipata kuniambia: '’Sheikh Khamis, pamoja na uwezo wako wa kielimu hutochaguliwa kwenda sekondari na kinachokuponza ni huu ualimu wako wa Dini ya Kiislamu.'’
Hakika na kweli ikawa hivyo badala ya kuchaguliwa kwenda sekondari nikapelekwa Chuo Cha Ufundi Chang'ombe kusomea Usukaji Mota. Uhodari wangu wa masomo na tabia yangu nzuri hazikutazamwa. Kilichoangaliwa ni ule Uislam wangu.
Sikukaa sana pale Chuo Cha Ufundi na kwa hakika moyo wangu ulikuwa ukiniuma nikiwaona wale ambao mimi nikiwapita katika masomo wako sekondari wanasoma na mimi nimepelekwa Chuo Cha Ufundi nikiwa muhitimu wa darasa la saba. Kilichofuatia ni kuwa nikaacha katikati na kujiunga na Chuo Cha Biashara ambapo nilichukua Basic Book-Keeping Certificate (BBC) na kufanya vizuri sana.
Katika mitihani ya ndani, '’’I was first out of 67 candidates,’’ yaani nilikuwa mwanafunzi wa kwanza nikiongoza katika wanafunzi 67. Huu ndiyo ulikuwa uwezo wangu mimi mwanafunzi niliyotokea shule ya msingi Mchikichini na maalim wa madras mtoto.
Nilipokabidhiwa cheti cha BBC taarifa ya ufaulu ilinizuia kuendelea na NABOCE kwa ibara hii: '’If you are Standard Seven you will be eligible to sit for NABOCE Exams after you have completed formal Form Four Education.’’ Bahati mbaya ilikuwa inazidi kuniandama.
Wakati huo umaskini wa familia ulinilazimisha kufanya kazi za kutafuta riziki halali mbali ya kuendelea kufundisha dini katika chuo change. Baba yangu Sheikh Saidi Mnuta Mataka akinilazimisha kuoa mapema ili amuone mjukuu wa jina lake kabla hajafa.
Nilioa.
Sasa kwa ajili ya kizingiti kile cha kuwa na cheti cha kidato cha nne nililazimika kuitafuta elimu ya sekondari kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (National Correspondence Institute) na nikafaulu QT (NECTA) Mtihani wa Kidato cha Nne na nikaweza kurudi chuoni CBE kuendelea na masomo ya NABOCE huku nikipata ajira ya kudumu ya Mfasiri wa Lugha za Kiarabu, Kiingereza na Kiswahili katika moja ya balozi nchini.
Laahawla! chuoni sikuikuta tena NABOCE bali mtaala mpya wa ATEC I na II nami nikazisoma kozi husika nikafaulu na nikaweka cheti kibindoni. Lakini ajira mpya ya Ubalozi haikuendana na mambo ya uhasibu nikalazimika kubadili upepo na nikasoma Lugha ya Kiingereza na kufanikiwa kutunukiwa Diploma ya Lugha (Kiingereza).
Muhimu leo nikuandikiapo haya nimeweza kupata vyeti hivi vifuatavyo hapo chini:
1. B.A. (Philosophy, Religious Studies & Kiswahili) - OUT.
2. Post Graduate Diploma (Education) - UDSM.
3. M.A. (Education) - UDSM.
4. Post Graduate Diploma (Management) - IGNOU/UDSM under Pan African E-Network (African Union/Government of India) through Tele-Conference facility.
5. Post Graduate Diploma (Human Resource Management)- IGNOU/UDSM.
Hapa nilipo sasa In Shaa Allah nasubiri MBA (HRM) baada ya kuwasilisha tasnifu yangu juu ya Time Management kupitia utafiti nilioufanya IFM, Dar es Salaam chini ya Dr. Adam Jamal kwa anuani hii: ‘’Managing Time Effectively: A Case of Lecturers in the Higher Learning Institutions.’’
Sasa hivi ni mwanafunzi wa LLB anayefikiria kuja kufanya Comperative Study kati ya Islamic Law na Conventional Law (Common Law and Others).
Kinachofurahisha siku ya Graduation wale walioungaunga elimu na waliounganisha husimama mstari mmoja kutuzwa.
HM
Era aliyosoma Nyerere na era aliyosoma Sheikh ni tofauti. Hivyo si ajabu Nyerere kuchelewa kuanza kusoma kwani umuhimu wa elimu haukufahamika nyakati zile tofauti na kipindi cha Sheikh.Mag3,
Sheikh Hamisi Mataka alianza shule ya msingi akiwa na miaka 11.
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alianza shule ya msingi 1934 akiwa na miaka 12.
Usikae kimya nitafurahi kama ukirejea Majlis na kuzungumza.
Wewe ndio haujaelewa mada, ila una khaliba ya kuhisi kuwa uko sawa, mada na mtoa mada kaweka reference ya shule ya mchikichini ambayo siyo ya dini, ni haki yake ku claim kwa manyanyaso kiimani. Wewe umeleta habari sijui za seminary simply umetoka out of content, nimekwambia unaweza ku claim haki ya kiimani kwenye shule/Chuo cha uma lakini sio kwenye shule ya taasisi ya dini. Kabla ya kejeli zako rudi kwenye mada uone ulivyo desa.Unapo quote Hivi umejijaribu kujishughulisha japo kusoma post zilizotangulia ili kupata Maudhui ya jambo linalozungumzwa....???!!! Au shuleni ulienda kusoma Ujinga...............???? si kila jambo unaweza changiaa.......! mengine yamekuzidi kimo Mjukuu wangu............ yasome tu........
Hongera sana Sheikh Mataka. Na pole kwa madhila yaliyokukuta, lakini umetufundisha mengi kupitia historia hii: Ustahimilivu na Jitihada bila kurudi nyuma. Kwa hakika umehamasisha hata wengine waliokosa fursa kwa sababu yoyote iwayo, wala wasikate tamaa na kunung'unika tu, tunasema siku hizi "wajiongeze".
Sheikh Hamisi Mataka
Shule ya Msingi Mchikichini sikupata kushika zaidi ya nafasi tatu za juu muda wote wa miaka saba hapo shuleni. Kwa kuwa nilianza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 11 ule moja wa miaka mine ambayo ningekuwa shule ya msingi iliniwezesha kumiliki chuo changu mwenyewe yaani madrasa, nikiwa mwalimu mkuu katika umri mdogo wa miaka 15.
Nilipoanza shule darasa la kwanza katika huo umri wa miaka 11 ambao ni mkubwa kwa kuanza darasa la kwanza pale Shule ya Mchikichini nilikuwa pia mwalimu wa dini kwa wenzangu.
Kwa ajili ya makuzi yangu ya Kiislam nilikuwa nikilitoka eneo la shule tu nilivaa kanzu yangu juu ya sare kwa kuwa sikujisikia kuvaa kaptula mitaani kwani uchi wa mwanmme unaanza juu ya magoti yake.
Mwalimu wangu wa Historia Mzee Kasunsumo alipata kuniambia: '’Sheikh Khamis, pamoja na uwezo wako wa kielimu hutochaguliwa kwenda sekondari na kinachokuponza ni huu ualimu wako wa Dini ya Kiislamu.'’
Hakika na kweli ikawa hivyo badala ya kuchaguliwa kwenda sekondari nikapelekwa Chuo Cha Ufundi Chang'ombe kusomea Usukaji Mota. Uhodari wangu wa masomo na tabia yangu nzuri hazikutazamwa. Kilichoangaliwa ni ule Uislam wangu.
Sikukaa sana pale Chuo Cha Ufundi na kwa hakika moyo wangu ulikuwa ukiniuma nikiwaona wale ambao mimi nikiwapita katika masomo wako sekondari wanasoma na mimi nimepelekwa Chuo Cha Ufundi nikiwa muhitimu wa darasa la saba. Kilichofuatia ni kuwa nikaacha katikati na kujiunga na Chuo Cha Biashara ambapo nilichukua Basic Book-Keeping Certificate (BBC) na kufanya vizuri sana.
Katika mitihani ya ndani, '’’I was first out of 67 candidates,’’ yaani nilikuwa mwanafunzi wa kwanza nikiongoza katika wanafunzi 67. Huu ndiyo ulikuwa uwezo wangu mimi mwanafunzi niliyotokea shule ya msingi Mchikichini na maalim wa madras mtoto.
Nilipokabidhiwa cheti cha BBC taarifa ya ufaulu ilinizuia kuendelea na NABOCE kwa ibara hii: '’If you are Standard Seven you will be eligible to sit for NABOCE Exams after you have completed formal Form Four Education.’’ Bahati mbaya ilikuwa inazidi kuniandama.
Wakati huo umaskini wa familia ulinilazimisha kufanya kazi za kutafuta riziki halali mbali ya kuendelea kufundisha dini katika chuo change. Baba yangu Sheikh Saidi Mnuta Mataka akinilazimisha kuoa mapema ili amuone mjukuu wa jina lake kabla hajafa.
Nilioa.
Sasa kwa ajili ya kizingiti kile cha kuwa na cheti cha kidato cha nne nililazimika kuitafuta elimu ya sekondari kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (National Correspondence Institute) na nikafaulu QT (NECTA) Mtihani wa Kidato cha Nne na nikaweza kurudi chuoni CBE kuendelea na masomo ya NABOCE huku nikipata ajira ya kudumu ya Mfasiri wa Lugha za Kiarabu, Kiingereza na Kiswahili katika moja ya balozi nchini.
Laahawla! chuoni sikuikuta tena NABOCE bali mtaala mpya wa ATEC I na II nami nikazisoma kozi husika nikafaulu na nikaweka cheti kibindoni. Lakini ajira mpya ya Ubalozi haikuendana na mambo ya uhasibu nikalazimika kubadili upepo na nikasoma Lugha ya Kiingereza na kufanikiwa kutunukiwa Diploma ya Lugha (Kiingereza).
Muhimu leo nikuandikiapo haya nimeweza kupata vyeti hivi vifuatavyo hapo chini:
1. B.A. (Philosophy, Religious Studies & Kiswahili) - OUT.
2. Post Graduate Diploma (Education) - UDSM.
3. M.A. (Education) - UDSM.
4. Post Graduate Diploma (Management) - IGNOU/UDSM under Pan African E-Network (African Union/Government of India) through Tele-Conference facility.
5. Post Graduate Diploma (Human Resource Management)- IGNOU/UDSM.
Hapa nilipo sasa In Shaa Allah nasubiri MBA (HRM) baada ya kuwasilisha tasnifu yangu juu ya Time Management kupitia utafiti nilioufanya IFM, Dar es Salaam chini ya Dr. Adam Jamal kwa anuani hii: ‘’Managing Time Effectively: A Case of Lecturers in the Higher Learning Institutions.’’
Sasa hivi ni mwanafunzi wa LLB anayefikiria kuja kufanya Comperative Study kati ya Islamic Law na Conventional Law (Common Law and Others).
Kinachofurahisha siku ya Graduation wale walioungaunga elimu na waliounganisha husimama mstari mmoja kutuzwa.
HM
Hii nondo kali sana.k
ni bora kuwa na dini yetu waafrika maana hizi dini zilizoletwa kwetu zimetujengea hali ya kuwa inferior sana. mimi ukiniita kafiri sawa. ukiniita mkristo sawa ukiiniita muislamu nisiye ujua uislamu tutaelimishana kama ni biblia au quran. ila huwa sikubaliani na upuuzi ,unafiki na mioyo dhaifu.
Hujuwi historua ya nchi hii kama kapuni, u knowkuna jamaa zangu mara nyingi husema wewe gudume si muislamu.. utakuwa mkristo au kafiri. mimi huwakubalia kwa kuwa ni mtizamo wao. kumekuwa na tatizo la waumini wa dini flani, watu wa kabila flani au asili flan(hasa sisi waafrika weusi) kuwa walalamishi. hii ni ishara ya udhaifu mkubwa sana. mimi nilikuwa nakuwa wa pili au watatu mitihani yote kuanzia darasa la 4 mpaka la saba. matokeo yalipokuja kutoka sikufanikiwa kuendelea kusoma kidato cha kwanza shule za serikali. na si mimi tu walikuwepo jamaa wengine wawili pia walikumbwa na mkasa huo. kila mwanafunzi alishangazwa na jambo hilo. sana.
bahati nzuri mbaya zaidi aliyekuwa wa kwanza kwa mitihani mingi pale shuleni alikuwa ni dini ya kikristo.huyu jamaa naye alikosa nafasi ya kuingia kidato cha kwanza. huyu alikuwa ni "kichwa" hasa... nami ambaye nilikuwa nashika nafasi ya pili ya tatu nilikumbwa na hilo. sikunyong'onyea. nikaenda jiunga shule ya sekondari binafsi. leo hii nina Degree Mbili na wala sikuwah kulia lia... haya mambo hayahusiani na dini sema kama tumeshajiona wanyonge na watu wa kulia lia kila siku tunaonesha udhaifu na hii hali itasababisha sasa watu watuoneee kweli kweli maana tumeshatangaza udhaifu.
waislam tuna shule gani ambazo tulianzisha ukilinganisha na wakristo? nyerere kama asinge taifisha shule nadhani kwa sasa hali yetu ingekuwa mbaya zaidi. tuangalie tu shule nyingi zinazofanya vizuri zinamilikiwa na akina nani? mbona kuna shule zinamilikiwa na wakristo na wanaofanya vizuri waislamu wapo? mbona huu ulalamishi wa kitoto unafikia hatua unatudhalilisha sasa. ustaadhi wangu kupata tu masters kaja kutangaza hapa katafuta sababu ya kutangazia kudai alikoseshwa kusoma na wakristo wakati wapo waislamu kadhaa wengi wamesoma shule za kikristo. mimi nimesoma shule ya mission ilikuwa wakichinja nguruwe wanapika jiko lingine ili kwa waislamu na wasabato wasibughudhiwe.. hi shule ilikuwa inaongozwa na maburuda. na aliyekuwa kaka mkuu wa shule alikuwa muislamu .ijumaa madarasa yalikuwa yanaisha saa tano na nusu. jamani kwa nini tunakuwa hivi?
ni bora kuwa na dini yetu waafrika maana hizi dini zilizoletwa kwetu zimetujengea hali ya kuwa inferior sana. mimi ukiniita kafiri sawa. ukiniita mkristo sawa ukiiniita muislamu nisiye ujua uislamu tutaelimishana kama ni biblia au quran. ila huwa sikubaliani na upuuzi ,unafiki na mioyo dhaifu.
Hujuwi historua ya nchi hii kama kapuni, u know
nothing
Chief,Era aliyosoma Nyerere na era aliyosoma Sheikh ni tofauti. Hivyo si ajabu Nyerere kuchelewa kuanza kusoma kwani umuhimu wa elimu haukufahamika nyakati zile tofauti na kipindi cha Sheikh.
Sijaghafilika Sheikh. Nimezungumzia kwa ujumla wake. Sijasema kuwa vipindi vya nyuma havikuwa kabisa na watu walioelewa maana au umuhimu wa kusoma. Sasa niambie hao wote uliowataja walianza kusoma wakiwa na miaka mingapi? Kwani hii ndio issue ya mjadala.Chief,
Unasema hivyo kwa kuwa hujui historia ya elimu katika pwani ya Afrika ya Mashariki.
Krapf amefika kwa Chief Kimweri katikati ya 1800 kawakuta watu wa Kimweri Vuga
wanasoma na kuandika na kupiga hesabu.
Huwa nashauri sana watu kusoma kabla ya kuja hapa kujadili.
Hebu tafuta historia ya Muyaka bin Haji (1776 - 1840) mshairi bingwa wa zaidi ya
miaka 150 iliyopita labda itakufungua macho.
Muyaka kaacha hazina tunatumia hadi leo.
Hadi leo mimi huandika vipande vya Muyaka bin Haji, ''Mbona unaghafiilika kwa jambo
lisilo na shaka?''
Wewe unasema watu walikuwa hawajui elimu.
Ukisoma historia ya Wamishionari wao watakuambia kuwa wao ndiyo walioelta elimu
nchi petu.
Babu yangu mzaa mama Sheikh Mohamed Mvamila Mzaramo wa Mkamba 1900s ni
sheikh akisomesha Musoma na kuandika kwa hati za Kiarabu.
Huyu somo yangu hakusomeshwa na Wamishionari na alikweda Musoma kusomesha dini.
Tuna historia na tunaijua vizuri sana.
Dah! Pole mkuu! Lakini bado nadhani hakukuwa na ulazima wa kujishikisha vitu unavyoamini ni vya haramu. Waislamu wamesoma shule za kikristo tangu kabla ya ukoloni na hawakulazimishwa kubadili dini (naamini kwa kiasi fulani walishawishiwa, lakini siyo kulazimishwa). Nina wazee mtaani hapa wamesoma St Francis College Pugu ya zamani, na ni waislamu tangu zamani hadi leo. Cha ukweli kabisa ambacho hata wazee wangu mtaani wananiambia ni kwamba wazazi wao walikuwa hawapendi huo ushawishi, hasa ukizingatia kuwa wanaoshawishiwa ni watoto. Kupambana na hali hiyo, wazee wao walikuwa wanahakikisha mtoto amepata elimu ya kutosha ya madrasa ya kiislamu kabla hajajiunga shule hizo ili kumuongezea uimara wa kutoshawishika. Nina marafiki na majirani waislamu ambao watoto wao wanasoma shule za English medium za kikristo, wananiambia wanahakikisha kila siku mtoto akitoka shule jioni lazima aingie chuo apate maarifa ya kiislamu ili asiyumbe (japo nina uhakika shule za kikristo za siku hizi huwa hawashawishi mtu yeyote kubadili dini).Uongo siyo Mzuri hata kidogo Ndugu yangu................mimi ni mwenye asili ya Kilwa na nimesomea huko shule ya msingi......Mzazi wangu ''Mungu ampunguzie Adhabu za Kabri'' Alinibadilisha Jina na kunipa jina la KIBANTU ili kuficha UISLAM wetu na hatimae nilipofika form 6 nilikuwa tunafuga Nguruwe.......yote hiyo ni kutaka kujua Mtu ana DINI gani........!!!!????? nimeshika mpaka Chetezo la Ubani KANISANI siku ya misa kama Mtoto wa kanisa la RC............!!!