Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,828
- 3,579
Hapana, hii ya jaji na wakristo wengine hasa waanglikana wa Zanzibar ni tofauti sana. Hawa babu wa babu zao waligombolewa pale soko la watumwa kwa kununuliwa na wamishenari kutoka kwa waarabu waliokuwa wanauza watumwa. Wengine waliachiwa huru utumwani wakatunzwa na kusaidiwa na hao wamishenari, ndipo walipobatizwa lakini wakatunza pia na majina yao ya awali.Ukifuatilia utakuta hata jaji Augustino Ramadhani nae ilikuwa hivyohivyo.
Wengine kutokana ufinyu wa Elimu ya dini walijikuta wanazamia hukohuko.
Niwakumbushe tu kuwa majina mengi ya watumwa hayakuwa majina yao halisi, walipewa tu na slavemasters kama sisi wengine tunavyowapa ng'ombe wetu majina. Asilimia kubwa ya hawa watumwa hawakuwa na hizi dini za kigeni walipokamatwa. Walikuwa na majina yao ya kiyao, kinyamwezi, kimakonde nk, lakini mabosi waliamua kuwapa majina ambayo ni rahisi kwao mabosi kukumbuka, wakawakatia tu majina Ali, Juma, Omari, almuradi majina rahisi. Hata hao wamarekani weusi mnaosikia wana majina ya kizungu, hayo hayakuwa majina yao, walikatiwa majina na wazungu kwa sababu wazungu walishindwa kutamka majina ya kibantu na pia wangeshindwa kuyakumbuka. Surnames nyingi za black Americans ni majina ya owners wao au ya mitaa au mashamba au biashara walikotumika (utasikia watu weusi wanaitwa Baker, Tailor, Rivers, Mason, Blackwell etc)