Sheikh Hamisi Mataka: Nilivyokoseshwa elimu ya Sekondari

Mkuu, ukikubali kusoma shule ya wakatoliki ukubali na utamaduni na shelia zao, kabisa mtu anaweza kuamini kuwa wakatoliki wanaweza kuwatengea madrasa ili muendeleze dini yenu. Hivi Morogoro Muslimi University unaweza ukasoma mkristo na ukafuata tamaduni za kikristo? Jibu ni hapana! Kama ilivyo kwenye shule za missionaries hata kwenye vyuo/shule za muslim suala la ibada ni lazima. Sasa mbona Wengine hawalalamikii hili! Jambo la msingi ni kwamba ukikubali kuingia kwenye chuo cha MMU huku unajua msingi wa chuo hicho unajengwa na uislam then ukalalamika kuwa tunalazimishwa kwenda msikitini wewe ndio utakuwa una tatizo na shule zilizojengwa kwenye misingi ya kanisa vivyo hivyo,
 
Upuuzi kama huu aliwahi kufanyiwa pia marehemu Dr.Amani Walidi Kabourou,tofauti ni kuwa yeye hakuwa mwalim wa madrasa tu.
 
nakumbuka babu yangu ilibidi abadili jina kutoka athumani hadi joseph ili tu aweze kupangwa shule kwa kipindi hicho nyingi zikimilikiwa na wamisionari,

bila good enough alibadili jina ila imani yake haikutetereka R.I.P babu
Ukifuatilia utakuta hata jaji Augustino Ramadhani nae ilikuwa hivyohivyo.

Wengine kutokana ufinyu wa Elimu ya dini walijikuta wanazamia hukohuko.
 
Unapo quote Hivi umejijaribu kujishughulisha japo kusoma post zilizotangulia ili kupata Maudhui ya jambo linalozungumzwa....???!!! Au shuleni ulienda kusoma Ujinga...............???? si kila jambo unaweza changiaa.......! mengine yamekuzidi kimo Mjukuu wangu............ yasome tu........
 
Hatari inayokuja hapa ni kwamba pamoja na kupata elimu iliyotukuka bado fikra zile za darasa la saba zimetaraki!kwamba alipelekwa shule ya ufundi tu kwa sababu alikuwa ni muislam!ni wazi kuna kila sababu ya kumsaidia kufanya utafiti.
Hivi kuna kundi la watu wana kaa na kupanga kumkwamisha mtu kwasababu ya uislamu wake!au alitumia mwamvuli wa uislamu kueneza ajenda za shetani?hizi dini pamoja na kwamba tuliletewa na watu waliokuwa na makusudio yao maalumu lakini kwa bahati mbaya zinaweza kutuvuruga.
Kwani huyu angezaliwa kule Nkasi angekuwa dini gani?mazingira yametufanya tuwe na hizi dini tunapaswa kufuata yaliyo mema na yanayo mpendeza Mungu.
Kwa upande wa Elimu mfumo wa zamani uliathiri watu wengi wenye vipaji na kupoteza uelekeo jambo ambalo kwa kipindi hiki itabaki kuwa historia.
 
Miaka hiyo,hali hiyo ilikuwa ni ya kawaida sana. Kuna brother wangua likuwa anaongoza darsa lao, Jina likampoza. Akarudia kwa jina ja John, akafauru. NOwdays tushukuru hizi namba za mitihani, kidogo hutusaidia.
Ubaguzi haukuweza kuwaacha salama.
 
Mag3,
Sheikh Hamisi Mataka
alianza shule ya msingi akiwa na miaka 11.
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alianza shule ya msingi 1934 akiwa na miaka 12.

Usikae kimya nitafurahi kama ukirejea Majlis na kuzungumza.
Era aliyosoma Nyerere na era aliyosoma Sheikh ni tofauti. Hivyo si ajabu Nyerere kuchelewa kuanza kusoma kwani umuhimu wa elimu haukufahamika nyakati zile tofauti na kipindi cha Sheikh.
 
Wewe ndio haujaelewa mada, ila una khaliba ya kuhisi kuwa uko sawa, mada na mtoa mada kaweka reference ya shule ya mchikichini ambayo siyo ya dini, ni haki yake ku claim kwa manyanyaso kiimani. Wewe umeleta habari sijui za seminary simply umetoka out of content, nimekwambia unaweza ku claim haki ya kiimani kwenye shule/Chuo cha uma lakini sio kwenye shule ya taasisi ya dini. Kabla ya kejeli zako rudi kwenye mada uone ulivyo desa.
 
Kuna jamaa zangu mara nyingi husema wewe gudume si muislamu.. utakuwa mkristo au kafiri. mimi huwakubalia kwa kuwa ni mtizamo wao. kumekuwa na tatizo la waumini wa dini flani, watu wa kabila flani au asili flan(hasa sisi waafrika weusi) kuwa walalamishi. hii ni ishara ya udhaifu mkubwa sana. mimi nilikuwa nakuwa wa pili au watatu mitihani yote kuanzia darasa la 4 mpaka la saba. matokeo yalipokuja kutoka sikufanikiwa kuendelea kusoma kidato cha kwanza shule za serikali. na si mimi tu walikuwepo jamaa wengine wawili pia walikumbwa na mkasa huo. kila mwanafunzi alishangazwa na jambo hilo. sana.

Bahati nzuri mbaya zaidi aliyekuwa wa kwanza kwa mitihani mingi pale shuleni alikuwa ni dini ya kikristo.huyu jamaa naye alikosa nafasi ya kuingia kidato cha kwanza. huyu alikuwa ni "kichwa" hasa... nami ambaye nilikuwa nashika nafasi ya pili ya tatu nilikumbwa na hilo. sikunyong'onyea. nikaenda jiunga shule ya sekondari binafsi. leo hii nina Degree Mbili na wala sikuwah kulia lia... haya mambo hayahusiani na dini sema kama tumeshajiona wanyonge na watu wa kulia lia kila siku tunaonesha udhaifu na hii hali itasababisha sasa watu watuoneee kweli kweli maana tumeshatangaza udhaifu.

Waislam tuna shule gani ambazo tulianzisha ukilinganisha na wakristo? nyerere kama asinge taifisha shule nadhani kwa sasa hali yetu ingekuwa mbaya zaidi. tuangalie tu shule nyingi zinazofanya vizuri zinamilikiwa na akina nani? mbona kuna shule zinamilikiwa na wakristo na wanaofanya vizuri waislamu wapo? mbona huu ulalamishi wa kitoto unafikia hatua unatudhalilisha sasa. ustaadhi wangu kupata tu masters kaja kutangaza hapa katafuta sababu ya kutangazia kudai alikoseshwa kusoma na wakristo wakati wapo waislamu kadhaa wengi wamesoma shule za kikristo. mimi nimesoma shule ya mission ilikuwa wakichinja nguruwe wanapika jiko lingine ili kwa waislamu na wasabato wasibughudhiwe.. hi shule ilikuwa inaongozwa na maburuda. na aliyekuwa kaka mkuu wa shule alikuwa muislamu .ijumaa madarasa yalikuwa yanaisha saa tano na nusu. jamani kwa nini tunakuwa hivi?

Ni bora kuwa na dini yetu waafrika maana hizi dini zilizoletwa kwetu zimetujengea hali ya kuwa inferior sana. mimi ukiniita kafiri sawa. ukiniita mkristo sawa ukiiniita muislamu nisiye ujua uislamu tutaelimishana kama ni biblia au quran. ila huwa sikubaliani na upuuzi ,unafiki na mioyo dhaifu.
 
Hongera sana Sheikh Mataka. Na pole kwa madhila yaliyokukuta, lakini umetufundisha mengi kupitia historia hii: Ustahimilivu na Jitihada bila kurudi nyuma. Kwa hakika umehamasisha hata wengine waliokosa fursa kwa sababu yoyote iwayo, wala wasikate tamaa na kunung'unika tu, tunasema siku hizi "wajiongeze".
Sijui ni mwaka upi ulimaliza darasa la saba, pengine ni enzi ya ukoloni, na ubaguzi kama huo ni miongoni mwa sababu hasa za kutaka tujiawale. Lakini kama hili jambo lilitokea baada ya uhuru, huyo mwalimu ulipaswa kumripoti kwa malalamiko rasmi kabisa na hatua zichukuliwe. Nakumbuka hata miaka niliyosoma mimi shule ya sekondari (1980s mwanzoni) nafasi za kuchaguliwa shule za sekondari zilikuwa haba sana. Kijijini kwetu nilikosoma tarafa nzima tulikuwa wakristo watupu, lakini kata yetu iliyokuwa na shule saba za msingi ni shule tatu tu zilipata waliochaguliwa kwenda sekondari, tena ni kati ya watatu na wanne kila shule. Na si kwamba hatukuwa na uwezo darasani, mitihani ya mock ya tarafa tulifanya vizuri sana, na ushahidi zaidi ni kuwa wengi waliojiunga shule za binafsi na za TAPA baadaye walisonga mbele hadi vyuo vikuu, wengine sasa hivi ni maprofesa.
Kwa ujumla nasikitika kuwa mwalimu wako huyo alikukatisha tamaa kwa kutumia maneno ya kibaguzi, lakini alijichumia dhambi bure, fursa za sekondari zilikuwa adimu hata kwa hao ambao huyo mwalimu alidhani anawapendelea.
 
Hii nondo kali sana.
 
Hujuwi historua ya nchi hii kama kapuni, u know
nothing
 
ni tatizo kubwa sana pale mtu anapodhani anajua kumbe hajui. ungenyamaza wala tusingejua kuwa hujui kitu ila unadhani unajua. ni aibu kama nikisema nikae kukuelimisha maana huwezi elewa umeshakumbatia hali flani ambayo huwezi toka hapo..... hata iweje.
Hujuwi historua ya nchi hii kama kapuni, u know
nothing
 
Hongera kwa kusoma na kuhitimu pamoja na changamoto nyingi za maisha. Ila hii stori ya kunyimwa nafasi kwa sababu ya uislamu sidhani kama in ukweli wowote.
 
GuDume,
Gas State hakutaka kukueleza mengi ila kusema "hujui" kwa sababu ungelijua historia ya nchi yetu na juhudi walizofanya Waislam katika kupigani uhuru (1954 - 1961) kisha kuitisha Muslim Congress mbili 1962 na 1963 kuweka mikakati ya elimu na kazi ikaanza kujenga shule za msingi, sekondari na Chuo Kikuu na jiwe la msingi likawekwa, usingesema hayo maneno uliyosema.

Sasa ushauri wangu kwako ni huu.
Fanya utafiti wako mwenyewe ujue na ujiridhishe kwa kuelewa nini kilifanyika hadi Waislam wakazuiwa kutimiza maazimio yao yote ya kujipatia elimu.

Kwa nini shule na Chuo Kikuu zilisimama kujengwa na taasisi yao iliyokuwa ikiratibu na kufanya kazi zote hizo ikapigwa marufuku kama taasisi isiyo halali.

Ukifanya haya utakuwa umejielimisha na hutoonekana mtu usiyejua kitu lakini unataka kufanya mjadala katika hali ya ujinga.

Samahani kwa kutumia neno hilo.
 
Era aliyosoma Nyerere na era aliyosoma Sheikh ni tofauti. Hivyo si ajabu Nyerere kuchelewa kuanza kusoma kwani umuhimu wa elimu haukufahamika nyakati zile tofauti na kipindi cha Sheikh.
Chief,
Unasema hivyo kwa kuwa hujui historia ya elimu katika pwani ya Afrika ya Mashariki.

Krapf amefika kwa Chief Kimweri katikati ya 1800 kawakuta watu wa Kimweri Vuga
wanasoma na kuandika na kupiga hesabu.

Huwa nashauri sana watu kusoma kabla ya kuja hapa kujadili.

Hebu tafuta historia ya Muyaka bin Haji (1776 - 1840) mshairi bingwa wa zaidi ya
miaka 150 iliyopita labda itakufungua macho.

Muyaka kaacha hazina tunatumia hadi leo.

Hadi leo mimi huandika vipande vya Muyaka bin Haji, ''Mbona unaghafiilika kwa jambo
lisilo na shaka?''

Wewe unasema watu walikuwa hawajui elimu.

Ukisoma historia ya Wamishionari wao watakuambia kuwa wao ndiyo walioelta elimu
nchi petu.

Babu yangu mzaa mama Sheikh Mohamed Mvamila Mzaramo wa Mkamba 1900s ni
sheikh akisomesha Musoma na kuandika kwa hati za Kiarabu.

Huyu somo yangu hakusomeshwa na Wamishionari na alikwenda Musoma kusomesha dini.
Tuna historia na tunaijua vizuri sana.
 
Sijaghafilika Sheikh. Nimezungumzia kwa ujumla wake. Sijasema kuwa vipindi vya nyuma havikuwa kabisa na watu walioelewa maana au umuhimu wa kusoma. Sasa niambie hao wote uliowataja walianza kusoma wakiwa na miaka mingapi? Kwani hii ndio issue ya mjadala.
 
Tunaanza kusoma tukiwa na miaka saba maana hui ndiyo umri wa kuanza kusali na huwezi kusali bila kujua kusoma.

Sheikh Mataka kaanza kusoma akiwa na miaka 7 akisoma na kuandika kwa Kiarabu.

Shule Mchikichini ndipo alipoanza kusoma Kizungu na miaka 11.

Sisi sote huanza na alif, be, te kisha ndiyo tukaja kusoma a, b, c...
 
Dah! Pole mkuu! Lakini bado nadhani hakukuwa na ulazima wa kujishikisha vitu unavyoamini ni vya haramu. Waislamu wamesoma shule za kikristo tangu kabla ya ukoloni na hawakulazimishwa kubadili dini (naamini kwa kiasi fulani walishawishiwa, lakini siyo kulazimishwa). Nina wazee mtaani hapa wamesoma St Francis College Pugu ya zamani, na ni waislamu tangu zamani hadi leo. Cha ukweli kabisa ambacho hata wazee wangu mtaani wananiambia ni kwamba wazazi wao walikuwa hawapendi huo ushawishi, hasa ukizingatia kuwa wanaoshawishiwa ni watoto. Kupambana na hali hiyo, wazee wao walikuwa wanahakikisha mtoto amepata elimu ya kutosha ya madrasa ya kiislamu kabla hajajiunga shule hizo ili kumuongezea uimara wa kutoshawishika. Nina marafiki na majirani waislamu ambao watoto wao wanasoma shule za English medium za kikristo, wananiambia wanahakikisha kila siku mtoto akitoka shule jioni lazima aingie chuo apate maarifa ya kiislamu ili asiyumbe (japo nina uhakika shule za kikristo za siku hizi huwa hawashawishi mtu yeyote kubadili dini).
Nadhani ni utaratibu mzuri kujitahidi kuhakikisha mwanao anafuata misingi bora ya dini yako, si tu kujikinga dhidi ya ushawishi wa watu wa dini nyingine, bali zaidi kujikinga dhidi ya maovu. Maovu hayana dini. Waovu wote hawafuati dini zao (ndio maana wanafanya maovu), kwa hiyo tunapaswa kupambana na maovu hata au niseme hasa yanapotendwa na walewale wanaojinasibu kuwa ni waumini wenzetu wa dini tunazofuata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…