Sheikh Hamisi Mataka: Nilivyokoseshwa elimu ya Sekondari

Ukifuatilia utakuta hata jaji Augustino Ramadhani nae ilikuwa hivyohivyo.

Wengine kutokana ufinyu wa Elimu ya dini walijikuta wanazamia hukohuko.
Hapana, hii ya jaji na wakristo wengine hasa waanglikana wa Zanzibar ni tofauti sana. Hawa babu wa babu zao waligombolewa pale soko la watumwa kwa kununuliwa na wamishenari kutoka kwa waarabu waliokuwa wanauza watumwa. Wengine waliachiwa huru utumwani wakatunzwa na kusaidiwa na hao wamishenari, ndipo walipobatizwa lakini wakatunza pia na majina yao ya awali.
Niwakumbushe tu kuwa majina mengi ya watumwa hayakuwa majina yao halisi, walipewa tu na slavemasters kama sisi wengine tunavyowapa ng'ombe wetu majina. Asilimia kubwa ya hawa watumwa hawakuwa na hizi dini za kigeni walipokamatwa. Walikuwa na majina yao ya kiyao, kinyamwezi, kimakonde nk, lakini mabosi waliamua kuwapa majina ambayo ni rahisi kwao mabosi kukumbuka, wakawakatia tu majina Ali, Juma, Omari, almuradi majina rahisi. Hata hao wamarekani weusi mnaosikia wana majina ya kizungu, hayo hayakuwa majina yao, walikatiwa majina na wazungu kwa sababu wazungu walishindwa kutamka majina ya kibantu na pia wangeshindwa kuyakumbuka. Surnames nyingi za black Americans ni majina ya owners wao au ya mitaa au mashamba au biashara walikotumika (utasikia watu weusi wanaitwa Baker, Tailor, Rivers, Mason, Blackwell etc)
 
Wewe hujuwi kuna mengi juu ya Elimu, mitihani na watoto wetu wa Kitanzania, you were too young to know. Pepa katunga Kudume na marker ni Gudume y mtoto mwenye jina linaloelekea kufanana na Gudume asifaulu. Huu mfumo wa Namba umewaharibia sana kina Gudume thats y mwanzilishi wake (Kigoma) alilaaniwa sana na hakupendwa kabisa na kina Gudume. Njoo Gudume utetee mana naamini ulibebwa na mfumo ule dhalimu so unalipa fadhila, bila kubebwa kwa kuangalia jina lako usingekuwa ulipo. Kaulize NECTA mratibu wa pepa za masomo ya Imani alikuwa ni nani na jee kwa kuwa masomo hayo yapo mengi huyo mtu alikuwa na knowledge za Imani zingine ambazo nazo zikipiga pepa.
Narudia wewe hujuwi historia ya Elimu yetu kaa kimya kama tulivyokaa sie, usilazimishe tufukue makaburi.
 
tatizo kubwa ni pale unapodhani unajua... tatizo linaanzia hapo unataka watu maamuma ambao watawaza kama wewe unavyowaza. sijajua umetumia kigezo gani kudhani una umri mkubwa kuliko mimi..lakini ashakum si matusi . lets say una umri mkubwa. basi ni dhahili kuwa ukubwa wa pua si wingi wa makamasi. haya malalamiko sis wengine tumeyachoka... yamekuwepo tangu na tangu hayajawahi kutusaidia zaidi ya kujenga tu roho ya ulalamishi na inferiority complex... tukianza kujiamini tutacha malalamiko ya kipuuzi. hakuna watu waliowah kuendelea kwa kulalamika kipuuzi. tujenge shule na vyuo .. tuacheni kulishana ujinga .... boko haram ndo akili zetu kwa kiasi kikubwa.

unadhani unajua ila una prove hujui kitu... ni maamuma tu kama wengine.

 
Hii habari ya namba ni uongo mtupu. Nimefanya mtihani wa darasa la saba mwaka 1981, tulitumia namba siyo majina. Waziri wa Elimu wakati huo alikuwa Mama Tabitha Siwale kama sijasahau. Nilifanya mtihani wa form four mwaka 1985, waziri wa elimu alikuwa Jackson Makweta, na tulitumia namba za mitihani, siyo majina. Cheti changu cha Form 4 kimesainiwa na A. Modesti na N.A. Kuhanga. Kighoma Malima alikuja kuwa waziri wa elimu baadae, na wala siye aliyeasisi mfumo wa namba za mtihani.
 
aiseeee
 
Hapa hatuandiki tu kufurahisha watu au Kupump post za watu Please hebu chukua MAUDHUI ya Post then njoo ulete mchango wako..........Eboooooooooo...........!!!! Tusichoshane Asubuhi hiii.....!!!!
hahaaa
 
Nafikiri ungeaza kujibu hivi tangu zamani wala uzi huu usingekuwa mrefu kwani unaelezea kwa nini Sheikh alichelewa kuanza darasa la kwanza.
 
hahaas
 
Kuna mada zingine lakini zinachosha. Sasa unataka kusema nini au unasema nini
Tumpongezeeeee au tumshangae maana hata hueleweki
Okay mpe hongera zetu
Well done!
 
Chief,
Bahati mbaya ikiwa nimechelewa kuja na taarifa hizi.
 
Hujuwi historua ya nchi hii kama kapuni, u know
nothing
wewe unayeijua sasa sindio uanzishe Uzi wako ....ili watu wengine ..
wapate kuifahamu ....au utaendelea kubaki nayo tu kama siri """ huku unasubiri watu wakitoa michango yao"" uishie kuwaambia kuwa hawajui ,,,,,,, historian ya nchi hii tu basii'' mkuu unahisi hilo ni sawa ''''
 
ASNTE SANA KWA HII ELIMU """ NILIWAHI KUISOMA MAHALI """",,.. LEO NIMEIKUTA TENA ...KWAKO NASHUKURU UMENIBUST UPYA ..."''
 
mkuu hayo makaburi ndio mazuri ...yafukue tu baba """ ili wengine tupate kuelimika na tujue pakushika haswaa""" ukikaa Kimya tutaendelea kuwa wajinga ,..""
 
mkuu hayo makaburi ndio mazuri ...yafukue tu baba """ ili wengine tupate kuelimika na tujue pakushika haswaa""" ukikaa Kimya tutaendelea kuwa wajinga ,..""
Hearly,
Nami nitasaidia katika kueleza yale ambayo yameonekana katika Wizara ya Elimu kuhusu shutuma za ubaguzi na kufanya upendeleo.

Naingia Maktaba In Shaa Allah.
 
Hearly,
Nami nitasaidia katika kueleza yale ambayo yameonekana katika Wizara ya Elimu kuhusu shutuma za ubaguzi na kufanya upendeleo.

Naingia Maktaba In Shaa Allah.
haya ukirejea """ usisahau ahadi yko
 
nilivyoelewa mimi yeye ameelezea historia ya elimu yake
na haya aliyo andika hapo ndiyo alivyopitia

hata kauli ya kutochaguliwa
kwa sababu ya ualimu wake wa madrasa
huo haukua mtazamo wake
bali ulikua mtazamo wa mwalimu wake
na yeye katika kuandika historia hii
kamnukuu alivyomweleza mwalimu wake
na kweli ikatokea vilevile

Katika hali kama bila shaka anaefahamu undani wa kwa nini
mtu mwenye haiba kama ya sheikh mataka
ilikua vigumu kuchaguliwa kwenda sekondar
ni mwalimu wake

yeye kaandika historia na hilo tukio kalinukuu kama lilivyotokea.
 
Hata huko kwa wajita wanalalamika kuna miaka Nyerere aliwabania wajita kwenda sekondari. Sina uhakika ila kwa hadithi zao mkoa wa Mara walichaguliwa wengi kutoka makabila ambayo bado walikuwa hawakuwa na muamko wa elimu wakati ule.
Haya historia iendelee kuandika.
 
Kuna kipindi waislam tulipata shida sana kielimu,yaani ilikua ni marufuku kufaulu,sitaki hata kukumbuka aiee
Wenzetu hayakuwakuta sio rahisi kuelewa maumivu yetu.Nilikuwa nafanya vizuri sana darasani shule ya msingi lkn jinamizi la kutochaguliwa lilinikumba.Ajabu karibu wote tuliokuwa na akili lakini hatuchaguliwi ni waislamu tu.Nakumbuka nimeishafanya mtihani wa darasa la saba nasubiri matokeo kaka yangu aliniambia maadamu jina lako liko wazi la kiislamu usitegemee kuchaguliwa,sikumuamini lakini ndivyo ilivyo tokea.Jamani acheni uchungu ule mpaka leo naupata.
 

Usemayo Mkuu Ralph Tyler ni kweli ingawa wewe na Mkuu mmjasiliaupeo mnatakiwa kujua Maudhui ya Mtoa mada hapa siyo kusoma tu shule ya DIni au Serikali NO NO NO Tatizo wenye mamlaka kwa wakati huo wakijua kuwa wewe wa Dini fulani hatakama umefaulu unafelishwa iwe ya Serikali au Dini...........That is the Line if not the Point.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…