Sheikh Hamisi Mataka: Nilivyokoseshwa elimu ya Sekondari

Sheikh Hamisi Mataka: Nilivyokoseshwa elimu ya Sekondari

Unajua haya mambo ukweli ni kwamba islam mliwekeza sana kwenye madrassa na hii elimu ya kawaida mliichukulia kama ya wakristo, nimeishi sana lindi na mtwara naelewa kitu nachozungumza kilwa kisiwani nilikuta shule kubwa ya madrassa wanafunz wanaenda asubuhi wanarud jioni huo mda wa kwenda kusoma physics wanaupata wapi? Kwa hiyo wazee wenu aliinyapapaa elimu dunia na wamisionary waliwekeza kwenye elimu dunia, na hii dhana hadi leo ipo ndio mikoa waliokaa sana waarabu kiwango chao cha elimu ni kidogo
Sizonje umemaliza
 
Mzee wangu sioni ajabu mwanzfunzi kutokuchaguliwa japo alikuwa anaongoza darasani.
Siku hazifanani na huwezi kufanya vizuri kila siku.
Je hata alifanya vibaya siku ya mtihani wa mwisho achaguliwe?
Binafsi nimeona wanafunzi wengi walioongoza kuanzia la kwanza hadi la 7 hawakuchaguliwa bali ambao walifanya vizuri wastani wakachaguliwa mtihani wa mwisho.
Elgibo,
Kwanza, darasa la saba hakukuwa na kufaulu na matokeo hayakuwa
yakiwekwa hadharani kama ilivyo sasa.

Paliambiwa kuwa wanaofaulu ni wengi lakini nafasi za sekondari ni
chache na zinagawanywa kwa uwiano wa kitaifa.

Hivyo, kulikuwa na kuchaguliwa na si kufaulu Mtihani wa Darasa la Saba. Baada ya mtihani uchaguzi wa wanafunzi uliwapeleka Sekondari, Ufundi na Ualimu (UPE).
 
Mzee Mohamedi ningependa kujua umri tafadhali najua ni irrelevant hapa lakini ukipenda nijalie umri wako.
 
Hata ivyo shukuru Mungu umefka hapo ulipo.

Shekhe mkuu nmeskia amekataza maandamano shekkhe, ni kwel?
 
Hata kama ni radi imepiga na wengi wa waliokufa/umia ni waislam, yeye Mohamed Said atasema radi imeua kwa ubaguzi kwa kuwaonea waislam.
Nanren,
Mtu akisema uongo mara moja huwa katika Uislam hana haki ya kutoa
ushahidi maisha yake yote.

Ulipata kumsingizia babu yangu uongo huu na nakunukuu:
''...na kibaya zaidi, baba wa mwandishi huyu, aliwahi kuwekwa rumande
na serikali ya Nyerere baada ya kuleta chokochoko za kidini zilizoanzishwa
na AMNUT.''

Nilikupa jibu kuhusu uongo ule na nakuwekea na jibu lenyewe hapo chini:
Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu Salum Abdallah.

Hakuwekwa kwa ajili ya dini.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955 Kasanga
Tumbo
akiwa katibu.

TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.

Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.

Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh Kenya.

Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya KAR
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.

Kuwekwa kwao ndani ilikuwa Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.

Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu Mwalimu Nyerere kwa
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa
wakisikilizwa na wananchi.

Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962 Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.

Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.

Nyerere hakufurahishwa na yeye.

Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na
kilimo cha tumbuku Urambo.

Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.

Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.

Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.

Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.

Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.


Hii nyaraka hapo chini ambayo inasema kuwa viongozi wa wafanyakazi akiwamo
babu yangu walihusika katika maasi, kesi ilipofikishwa mahakamani hakuna hata
kiongozi mmoja wa wafanyakazi alishtakiwa.

Viongozi hawa walibakia wameshikiliwa katika jela tofauti kisha wakaachiwa bila
ya mashtaka.

Nanren,
Naona sasa unakuja na mzaha mwingine.
 
Mzee wangu sioni ajabu mwanzfunzi kutokuchaguliwa japo alikuwa anaongoza darasani.
Siku hazifanani na huwezi kufanya vizuri kila siku.
Je hata alifanya vibaya siku ya mtihani wa mwisho achaguliwe?
Binafsi nimeona wanafunzi wengi walioongoza kuanzia la kwanza hadi la 7 hawakuchaguliwa bali ambao walifanya vizuri wastani wakachaguliwa mtihani wa mwisho.
Elgibo,
Tungepata majibu kutoka Wizara ya Elimu ingekuwa raha sana.
 
Astaghfirullah! Ulianza darasa la kwanza ukiwa na umri wa miaka 11 tena jijini Dar es Salaam! Nikiwa na umri wa miaka 11 nilikuwa niko darasa la 6 tena kijijini! Ngoja nikae kimya.
Tuko tofauti.

Mimi nikiwa na miaka 11 ndio darasa la 2. Tena kijijini kama wewe.
 
Mimi nashindwa kuelewa ina maana la saba huko NECTA walikuwa wanajua uislam wako na ualimu wako wa madrasa wakaona wakufelishe? Wewe kubali kuwa ulifail kwa sababu ya kuchanganya mambo ukiwa mdogo na hata hizo elimu zako ulizomention zinaonesha experience zako za kuvuruga mambo maana umesoma ma vitu mengi yasiyo na ushirikiano na inaelekea kichwani kwako kupo hivo hivo yaani papo vurugu vurugu
 
Bujibuji,
Naona kisa hiki kimekushughulisha sana.
Hilo swali ungewauliza Wizara ya Elimu.

Stori kama hizi ninazo nyingi sana.
 
Unajua haya mambo ukweli ni kwamba islam mliwekeza sana kwenye madrassa na hii elimu ya kawaida mliichukulia kama ya wakristo, nimeishi sana lindi na mtwara naelewa kitu nachozungumza kilwa kisiwani nilikuta shule kubwa ya madrassa wanafunz wanaenda asubuhi wanarud jioni huo mda wa kwenda kusoma physics wanaupata wapi? Kwa hiyo wazee wenu aliinyapapaa elimu dunia na wamisionary waliwekeza kwenye elimu dunia, na hii dhana hadi leo ipo ndio mikoa waliokaa sana waarabu kiwango chao cha elimu ni kidogo
Uongo siyo Mzuri hata kidogo Ndugu yangu................mimi ni mwenye asili ya Kilwa na nimesomea huko shule ya msingi......Mzazi wangu ''Mungu ampunguzie Adhabu za Kabri'' Alinibadilisha Jina na kunipa jina la KIBANTU ili kuficha UISLAM wetu na hatimae nilipofika form 6 nilikuwa tunafuga Nguruwe.......yote hiyo ni kutaka kujua Mtu ana DINI gani........!!!!????? nimeshika mpaka Chetezo la Ubani KANISANI siku ya misa kama Mtoto wa kanisa la RC............!!!
 
Astaghfirullah! Ulianza darasa la kwanza ukiwa na umri wa miaka 11 tena jijini Dar es Salaam! Nikiwa na umri wa miaka 11 nilikuwa niko darasa la 6 tena kijijini! Ngoja nikae kimya.
Mkuu mimi kijijini nilianza na miaka 10 1989 Lushoto juzi juzi tu hapa
 
Back
Top Bottom